Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
-
- #121
Fundi...Huu hapa ushahidi. Na ulilalamika kuhusu mimi kukuita muongo ndio maana najua uliisoma. Lakini hauwezi kukubali kuwa mmisheni Fundi Mchundo ndie aliyekufungua macho!
Amandla...
Mkuu hata mimi nimejiuliza kuhusu hilo bango la Cocacola na mengine ambayo hayasomeki vizuri kwanini yawepo hapo wakati ni duka la mafuta taa tu? Nadhani huyu Mzee wetu akaongezee maelezo zaidi kuthibitisha hiki anachosema.Uzuri umeweka picha ambayo ina bango la kuwa ni mawakala wa mafuta ya taa ya Shell Crown. Lakini pia kuna bango la Cocacola na pembeni kuna lingine ambalo bidhaa zake hazionekani vizuri. Kwa picha hiyo ni dhahiri kuwa alikuwa anauza bidhaa zaidi ya mafuta ya taa. Sasa kama kwenye hili unasema uongo kwa nini tukuamini kwenye mengine?
Amandla.....
Nguruvi3 JokaKuu
Amekubali kuwa alikosea.Mkuu hata mimi nimejiuliza kuhusu hilo bango la Cocacola na mengine ambayo hayasomeki vizuri kwanini yawepo hapo wakati ni duka la mafuta taa tu? Nadhani huyu Mzee wetu akaongezee maelezo zaidi kuthibitisha hiki anachosema.
Kama umepata taarifa mpya kwamba alikuwa akiuza na Cocacola huoni kwamba uzi wako huu ni batili na unapaswa kufutwa?Fundi...
Nimepokea taarifa kuwa Mama Maria pamoja na mafuta ya taa alikuwa akiuza Coca-Cola:
"SALESMAN ALIEKUWA ANAMPELEKEA SODA ZA COCA-COLA NI MAREHEMU AMAL BAFADHIL. NI SHEMEJI YAO KINA MOHAMED BAHADORY WA MKUNGUNI STREET."
Ukoo wa Bahadory ni maarufu Dar es Salaam ya miaka ile.
Hapana sababu ya sisi kuvutana na historia ya Abdul Sykes kama unaikubali au la.
Kuwa kulikuwa na wengine ni kweli lakini hawakutajwa popote hadi pale mimi nilipowataja ndani ya kitabu cha Abdul Sykes.
Watu hushangaa ninaandika TANU kadi no. 5 ni ya Denis Phombeah Mnyasa wa Nyasaland, no. 6 Dome Okochi Budohi Mluya kutoka Kenya kisha nikaweka na picha nimepiga na yeye Nairobi 1972 nikiwa na umri wa miaka 20.
Naona hukupenda mimi kujumuishwa na Dr. Salim Ahmed Salim na Brig. Hashim Mbita kuwa ni wenye maktaba kubwa iliyosheheni taarifa za Mwalimu.
Mimi hili pia limenishtusha sana.
Unasema ni la kwangu.
Hapana hili si la kwangu hili ni la taifa lililopoteza historia yake sasa wanaikusanyq upya.
Prof. Shivji anatoka Kigoda Cha Mwalimu Nyerere.
CCM wameniomba niwapatie baadhi ya Nyaraka za Sykes.
Mwakilishi wa Ford Foundation aliwasilana na mimi ili nitoe msaada kwa Nyerere Foundation.
Kuna mambo hujuzuia kusema.
Nina nyaraka za Mwalimu yeye hana na alipata miaka mingi iliyopita kuziomba kwa Ally Sykes.
Baadhi ya nyaraka hizi nimewapa watafiti waliozihitaji na baadhi zipo Library of Congress, Washington DC na vyuo vingi Marekani.
Unajua katika miaka ya 1980 Mwakilishi wa Library of Congress Tanzania alikuwa Ahmed Rashaad Ali.
Mimi huyu ni baba yangu.
Nadhani umenielewa.
Mimi sina kawaida ya kumuita mtu muongo wala kumtukana mtu au kumkejeli mtu katika mnakasha.
Humchukulia kuwa hajui na wajibu wangu ni kumfunza na ikiwa hataki hapana ugomvi.
Nakuwekea picha ya mmoja wa watoto wa Mzee Bahdoury - Ismail ''Gigi'' Bahdoury.
Hili jina la Gigi ni kwa ajili alikuwa na kipaji kikubwa sana cha kucheza mpira katika vijana wa Dar es Salaam.
Gigi lilikuwa jina la mchezaji wa Italy Luigi ''Gigi' Riva katika miaka ya 1960s.
View attachment 2465812
Ismail ''Gigi' Bahdoury Muscat 1999.
View attachment 2465820
Kushoto: Ahmed Rashaad Ali, Dr. Harith Ghassany na Mwandishi
View attachment 2465823
Library of Congress, Washington DC
Mama...Mkuu hata mimi nimejiuliza kuhusu hilo bango la Cocacola na mengine ambayo hayasomeki vizuri kwanini yawepo hapo wakati ni duka la mafuta taa tu? Nadhani huyu Mzee wetu akaongezee maelezo zaidi kuthibitisha hiki anachosema.
Mama...Kama umepata taarifa mpya kwamba alikuwa akiuza na Cocacola huoni kwamba uzi wako huu ni batili na unapaswa kufutwa?
Mzee hayo mambo mengine uliyoyataja kwenye comment yako umeyaongezea wewe ila kwenye uzi ulioandika umewakosoa waandishi wengine kwamba kulikuwa hakuuzwi kitu kingine zaidi ya mafuta taa. Fundi mchundo alivyouliza kulingana na alichoona kwenye picha ndo baadae ukaja na taarifa kwamba umeambiwa pia kulikuwa na Cocacola. Hadi hapo huoni hata wewe mwenyewe umewakosoa waandishi wengine huku ukiwa na uhakika?Mama...
Batili ni neno zito sana.
Ukisoma historia ya Mwalimu Nyerere na kusikiliza simulizi za wale aliokuwa nao wote watakueleza kuhusu duka la mafuta ya taa la Mtaa wa Mchikichi wakati Mwalimu anaishi na Abdul Sykes na mkewe Mama Daisy.
Halikadhalika katika kitabu cha maisha ya Mwalimu ''Nyerere Biography,'' kinaeleza duka la mafuta ya taa la Maduka Sita halitajwi la Mtaa wa Mchikichi wala lile nyumbani kwa Ali Msham Mtaa wa Jaribu.
Nashangaa sana kuwa huu wa ubishi wa Mama Maria kuuza mafuta ya taa na Coke-Cola umepewa umuhimu mkubwa usiostahili.
Nashangaa vipi hatujadili kuhusu duka la Mama Maria alilofungua Mtaa wa Mchikichi na LIvingstone wala la Mtaa wa Jaribu.
Wala hatuulizi huyu Ali Msham aliyempa Mama Maria nafasi nyumbani kwake Magomeni kuweka duka lake la mafuta ya taa ni nani?
Haya kwao hayana umuhimu.
Wala hawataki kujua kwa nini duka la Mchikichi la Mama Maria ambalo ndilo duka lake la kwanza la mafuta ya taa halikutajwa wala hili la pili?
Kinachowahangaisha ni kuwa Mohamed kasema anauza mafuta ya taa lakini tunaona bango la Coca-Cola.
Katika vijana wa Ali Msham yuko mmoja yeye alipewa kazi ya kumsindikiza Mama Maria Maduka Sita kwa kuwa alikuwa anafunga duka lake maghrib na kiza kishaingia.
Siku zile kutoka hapo Mtaa wa Jaribu kwenda Maduka sita kulikuwa na nyumba chache na sehemu kubwa ni miembe na mikorosho kiza kitupu.
Huyu kijana aliyekuwa anamsindikiza Mama Maria nyumbani kila siku bado yu hai na sasa ni mtu mzima.
Mngependa kujua jina lake?
View attachment 2468333
Abdul Sykes na mkewe Mama Daisy
View attachment 2468336
Kulia wa kwanza ni Ali Msham na Julius Nyerere ni huyo aliyekaa kwenye meza wapo Mtaa wa Jaribu hiyo meza na viti Ali Msham alitengeneza na kuabidhi Nyerere kwa matumizi ya ofisi yake New Street.
Sherehe ya kukabidhi ilifanyika kwenye tawi la TANU alilofungua nyumbani kwake Mtaa wa Jaribu kulikokuwa pia na duka la Mama Maria
Mama . ..Mzee hayo mambo mengine uliyoyataja kwenye comment yako umeyaongezea wewe ila kwenye uzi ulioandika umewakosoa waandishi wengine kwamba kulikuwa hakuuzwi kitu kingine zaidi ya mafuta taa. Fundi mchundo alivyouliza kulingana na alichoona kwenye picha ndo baadae ukaja na taarifa kwamba umeambiwa pia kulikuwa na Cocacola. Hadi hapo huoni hata wewe mwenyewe umewakosoa waandishi wengine huku ukiwa na uhakika?
Pamoja na coca hata bidhaa zingine pia nafkiri zilikuwepo.Kuna bango la CocaKola hapo huenda soda zilikua zinauzwa dukani hapo.
Gagnija,Ndugu Mohamed,
Katika andiko lako "ISLAM AND POLITICS IN TANZANIA" nimesoma kuwa baada ya sakata la EAMWS jaji Musa Kwikima alihamishwa toka Dar kupelekwa Mwanza kuwa hakimu mkazi.
Huku ni kushushwa cheo ambako hakujawahi kushuhudiwa. Ni kweli hili lilitokea?
Nimeuliza kwa nia njema kabisa ili nipate ufafanuzi, ambao nashukuru umeutoa, kwani awali sikuwa nimeisikia habari hii.Gagnija,
Sijui kwa nini kila unapokuja kwangu unakuja umeghadhibika.
unakuja na kibri na kejeli.
Mimi si mtu wa kughadhibika haraka lakini nafikiria kuacha mjadala na wewe.
Nimejaribu kuwa na subira kama sijatoa hoja inayofanana na hii,,swali zuri mkuu.Uzuri umeweka picha ambayo ina bango la kuwa ni mawakala wa mafuta ya taa ya Shell Crown. Lakini pia kuna bango la Cocacola na pembeni kuna lingine ambalo bidhaa zake hazionekani vizuri. Kwa picha hiyo ni dhahiri kuwa alikuwa anauza bidhaa zaidi ya mafuta ya taa. Sasa kama kwenye hili unasema uongo kwa nini tukuamini kwenye mengine?
Amandla.....
Nguruvi3 JokaKuu
Kuna mambo yanayotakiwa kupata ufafanuzi. Kwanza, ni je Jaji anaruhusiwa kuwa katika nafasi ya uongozi katika taasisi ya kidini? Je Jaji anaweza kuwa mchungaji? Najua Marehemu Augustino Ramadhani aliingia kwenye uongozi wa dini baada ya kustaafu. Sababu kubwa ni kuwa Jaji anatakiwa kuonekana "neutral" katika utoaji wa hukumu. Pili, je Rais alikuwa ana mamlaka ya kumuondoa mtu katika ujaji? Ninavyojua ni kuwa Jaji anaondolewa baada ya jopa la majaji wenzake kutoka Jumuia ya Madola kuridhia kuwa anastahili kufukuzwa. Rais mamlaka yake yanaishia kwenye kumsimamisha na sio kumfukuza. Lakini inawezekana kabisa kuwa yanayomkuta akaona kuwa amefanyiwa hivi kwa sababu ya dini yake.Gagnija,
Sijui kwa nini kila unapokuja kwangu unakuja umeghadhibika.
Ghadhabu inapunguza uwezo wako kufikiri na kutafakari.
Hili swali zuri lakini umeliharibu kiasi naona aibu kukujibu kwani nitashusha heshima yako.
Ulitakiwa uniulize hivi: "Kwa nini unasema Mussa Kwikima kashushushwa cheo kwa kuwa Hakimu Mkazi?"
Badala yake unakuja na kibri na kejeli.
Mimi si mtu wa kughadhibika haraka lakini nafikiria kuacha mjadala na wewe.
Bora hivyo uko hapa umejificha sura yako na jina lako hujulikani.
Jibu lako.
Mussa Kwikima alichaguliwa kuwa Jaji na Rais Nyerere na baada ya kuvunjwa kwa EAMWS mwaka wa 1968 Kikwima akavuliwa cheo cha Ujaji.
Sababu ya kuondolewa katika nafasi hiyo ni kuwa alikuwa Katibu wa Kamati ya Waislam iliyokuwa inajaribu kutafuta sulhu katika mgogoro wa EAMWS.
Inaonekana kipindi hicho kulikuwa ni mikorogano mingi.Kuna mambo yanayotakiwa kupata ufafanuzi. Kwanza, ni je Jaji anaruhusiwa kuwa katika nafasi ya uongozi katika taasisi ya kidini? Je Jaji anaweza kuwa mchungaji?
Kimsingi uliamua tu kukosoa uonekane wewe ndo unajua kuliko hao waandishi wengine kwa bahati nzuri ukafeli vibaya kusudio lako. Siku nyingine kosoa ukiwa na uhakika.Mama . ..
Ni kweli usemayo na sababu ni kuwa umaarufu wa Mama Maria ulikuwa duka la mafuta ya taa.
Hayo ya Coke-Cola ndiyo tumeyajua sasa.
Wakati Kighoma Malima alikuwa Waziri wa Elimu chini ya Rais Mwinyi baadhi ya viongozi wakristu waliondolewa katika nafasi zao. Inawezekana waliondolewa kutokana na mapungufu yao lakini wengi waliamini kuwa waliondolewa kwa sababu walikuwa wakristu. Hauwezi kuandika kuwa Kighoma Malima alikuwa mdini kwa kutegemea kitu ulichoambiwa na mmoja aliyeathirika bila kufanya utafiti kuthibitisha kuwa alikuwa na agenda hiyo. Ukifanya hivyo utakuwa unamuonea Kighoma Malima. Hivyo hivyo kuhusu Mwalimu na huyu Jaji.Inaonekana kipindi hicho kulikuwa ni mikorogano mingi.
Tewa Said alikuwa waziri serikalini akiwa pia rais wa EAMWS. Akafanya ziara nchi za kiarabu kutafuta fedha kujenga chuo kikuu cha kiislamu.
Kilikuwa kipindi kigumu sana kwa serikali.
Gagnija,Nimeuliza kwa nia njema kabisa ili nipate ufafanuzi, ambao nashukuru umeutoa, kwani awali sikuwa nimeisikia habari hii.
Kama nimekukwaza kwa namna yoyote naomba unisamehe. Sikusukumwa na kibri wala chuki kuuliza nilichouliza.
Nakuomba ukiondoe kitisho cha kusitisha kujadiliana nami; sioni kama zipo tofauti baina yetu za kuweza kutufikisha huko.
Fundi...Wakati Kighoma Malima alikuwa Waziri wa Elimu chini ya Rais Mwinyi baadhi ya viongozi wakristu waliondolewa katika nafasi zao. Inawezekana waliondolewa kutokana na mapungufu yao lakini wengi waliamini kuwa waliondolewa kwa sababu walikuwa wakristu. Hauwezi kuandika kuwa Kighoma Malima alikuwa mdini kwa kutegemea kitu ulichoambiwa na mmoja aliyeathirika bila kufanya utafiti kuthibitisha kuwa alikuwa na agenda hiyo. Ukifanya hivyo utakuwa unamuonea Kighoma Malima. Hivyo hivyo kuhusu Mwalimu na huyu Jaji.
Amandla...