Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
-
- #141
Mama...Kimsingi uliamua tu kukosoa uonekane wewe ndo unajua kuliko hao waandishi wengine kwa bahati nzuri ukafeli vibaya kusudio lako. Siku nyingine kosoa ukiwa na uhakika.
Were ni mwandishi wa hovyo kweli Mr Mohammed. Leo umenithibitishia kuwa historia yako ya kuinga unga. .Fundi...
Unanitilia maneno yako kinywani mwangu.
Sijasema popote unanichukia.
Sijapata kusema nataka niaminiwe kwa haya niyajuayo.
Hiyo ni khiyari ya mtu sina uwezo wa kulazimisha.
Hilo la kuwa hakuna mtu ajuaye historia ya Nyerere kunishinda maneno hayo kasema Prof. Shivji baada ya kufanya mahojiano na mimi wakati wanatafiti Nyerere Biography.
Hakuishia hapo katika Nyerere Biography wameandika kuwa Maktaba yangu ni kati ya maktaba 3 kubwa katika historia ya Nyerere.
Maktaba zingine 2 ni ya Dr. Salim Ahmed Salim na ya Brig. General Hashim Mbita.
Historia inasema Mama Maria biashara yake ilikuwa mafuta ya taa sikupata kusikia popote kuwa alikuwa anauza na bidhaa zingine.
Hata Nyerere Biography inasema hivyo.
Kuhusu nyumba aliyoishi Mwalimu baada ya kuacha kazi Nyerere Biography inasema alikaa kwa Ally Sykes na chanzo cha taarifa hii ni Abbas Sykes.
Abbas Sykes ndiye aliyehamishwa nyumba ili Nyerere aingie.
Abbas huyo huyo Nyerere Biography inasema Mwalimu aliishi nyumbani kwa Ally Sykes Mtaa wa Kipata.
Hapa ndipo ilipo starehe na raha ya historia ya Mwalimu Nyerere.
Kuhusu marafiki wa Kikatoliki wa Mama Maria siwezi kukataa kuwa alikuwanao lakini historia ya Mama Maria inaeleza marafiki wake wanaofahamika walikuwa jamaa zake Abdul Sykes - Bi. Chiku bint Said Kisusa mke wa Sharif Abdallah Attas, na watoto wao Sakina na Fatna.
Ukipenda wajumuishe Bi. Titi Mohamed, Tatu bint Mzee, Hawa bint Maftah na Halima bint Khamis akina mama mstari wa mbele TANU.
Unasema unapinga historia ya Abdul Sykes kupewa uzito.
Sawa una haki ya kufanya hivyo.
Lakini kitabu cha Abdul Sykes kinakwenda sasa toleo la 5 na kipo sasa robo karne na kinasomwa na kujadiliwa kila siku.
Hapa leo mwaka mpya tumeamka na Abdul Sykes.
Tunatofautiana hapo unaposema uliandika historia ya kweli ya TANU na Tanganyika. Unachokiandika wewe ni mchango wa familia ya wakina Sykes na waislamu wa Dar es Salaam katika kujenga TANU na kugombea uhuru wa Tanganyika. Historia hiyo haiwezi kuwa kamilifu isipotoka nje ya mipaka uliojiwekea.Fundi...
Kwangu mimi faraja yangu ni kuwa angalau kitabu cha Abdul Sykes kimefungua mjadala leo tunayazungumza haya hadharani.
Makala yangu ya kwanza iliyochapwa na Africa Events kueleza historia ya kweli ya TANU na uhuru wa Tanganyika gazeti lote toleo zima lilikusanywa na kutolewa kwenye mzunguko.
Makala ile iliwataja Abdul na Ally Sykes na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika katika historia ya kupambana na ukoloni.
Mwandishi akatukanwa na kutishwa asithubutu kutia mambo ya Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika katika TANU.
Aliyenitisha mwaka ule wa 1988 ni yule kiongozi wa jopo la Chuo Cha CCM Kivukoni waliokuwa mwaka wa 1981 wanaandika historia ya TANU aliyehakikisha kuwa historia ya Sykes haiandikwi kwenye kitabu cha TANU.
Iko siku In Shaa Allah nitamweleza Prof. Malima.
Fundi...Sio lugha kali aliyotumia mtetezi wako, ni matusi. Kumuita mtu "bugger" ni tusi la nguoni.
Ninacho tofautiana na wewe ni pale unapowafuta watu wa dini nyingine na kutaka waonekane waislamu peke yao. Haiingii kichwani kuwa familia ya Nyerere ilikuwa inahudumiwa na Ali Msham peke yake wakati yeye na mke wake walikuwa na marafiki wengi tu wenye uwezo wakristu. Kuna wakina Rupia, Pombeah, Kunambi na wengine. Kuna wale aliokuwa anasali nao. Kuna watu wa kabila lake. Kuna aliofanya nao kazi Msimbazi Centre. Wote hao wamuachie Ali Msham peke yake awe anawasaidia? Na kwa kiburi cha Nyerere unadhani angekubali familia yake ibebwe na mtu mmoja? Unaposema Ali Msham alimfungulia duka, unamaanisha ndie aliyempa mtaji wa kufungua hilo duka?
Tukirudi kwenye suala la duka la Magomeni. Unatuambia kuwa kuna mtu fulani ndie alikuwa anampelekea soda. Tunachojua soda zilikuwa zinaletwa kutoka kiwandani, sasa huyo unaesema alikuwa akimpelekea alikuwa anafanya hivyo kama nani? Kama wakala wa Cocacola, dereva wa gari la Cocacola au nani? Na je ni yeye peke yake ndie aliyekuwa anampelekea hizo soda au alikuwa mmoja katika waliokuwa wakimpelekea?
Amandla...
Fundi...Tunatofautiana hapo unaposema uliandika historia ya kweli ya TANU na Tanganyika. Unachokiandika wewe ni mchango wa familia ya wakina Sykes na waislamu wa Dar es Salaam katika kujenga TANU na kugombea uhuru wa Tanganyika. Historia hiyo haiwezi kuwa kamilifu isipotoka nje ya mipaka uliojiwekea.
Nitalisubiri andiko lako kuhusu Kighoma Malima ingawa najua tayari ni nini utakachoandika.
Amandla...
Gill,Were ni mwandishi wa hovyo kweli Mr Mohammed. Leo umenithibitishia kuwa historia yako ya kuinga unga. .
Kama mwandishi una nafasi ya kwend kumuoji Mama Nyerere. Siamini kama leo unabishana kuhusu biashara ya mama Nyerere as if its important wakati sio kitu cha umuhimu.
Una nafasi ya kwenda kumuhoji mama Maria kama mwandishi ila unabishana tu mtandaoni vitu ulivyosimuliwa. Mwandishi wa Hovyo sana na bure kabisa. .
Aliyemlipia faini Mwalimu alikuwa nani? Aliyemlipia kwa kiasi kikubwa nauli ya kwenda UN alikuwa nani? Mchango wa Pombeah hujui?Fundi...
Kuna mambo ambayo wazee wetu walifanyiana kwa hisani mimi siwezi kuyazungumza.
Hapana haja hiyo.
Wenyewe hata juu ya changamoto zilizokuja na uhuru hawakusema.
Lakini ninaloweza kusema na hili linafahamika ni kuwa wafadhili wa TANU Dar es Salaam wanafahamika.
Hao wengine uliowataja hawakupatapo hata siku moja kuwa na Nyerere ubavu kwa ubavu.
Angalia picha za kudai uhuru Nyerere kazungukwa na watu gani?
Nyerere safari ya UNO mkusanyaji fedha za safari ni Iddi Faiz Mafungo na waliokuwa wakipita nyumba kwa nyumba kuchangisha sumni sumni ni Bantu Group akina Juma "Mlevi" Selemani.
Akina mama waliomsindikiza uwanja wa ndege siku ya safari ni Bi. Chiku bint Said Kisusa, Tatu bint Mzee, Titi Mohamed.
Hafla ya kumuaga ilifanyika jengo la Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.
Hii ndiyo historia ya uhuru.
Ukweli kuwa Mama Maria Nyerere aliuza mafuta ya taa tu au na vitu vingine unaweza kupatikana kwa kumuuliza muhusika mwenyewe.
Huyu mama bado yupo hai, na anafikika kwa njia yoyote ambayo mtaona ni sawia kwenu na yeye.
Nilikuwa nashauri tu ili Kuweka kumbukumbu sahihi. Uzee siyo ugonjwa.
Mzee Mohamed Said heshima yako sana.Algore,
Sawa hapana neno.
Habari ya chombo cha serikali (gazeti la Nationalist) kilichokuwa chini ya Mkapa kuegemea upande mmoja kwenye mgogoro wa EAMWS iliandikwa na Mohamed wakati Mkapa akiwa bado hai.Nitakushangaa pamoja na huyu mama kupewa umri mrefu ila still unashindwa kwenda kufanya nae mjadala wowote then siku hayupo duniani uje kuandika tena vitu vya kusadikika kama ulivyofanya kwa Hayati Mkapa hakika nitakutoa maanani.
Kama hilo moja umekiri kukosea kwamba ulikuwa hujui unadhani ni rahisi kukuamini kwa historia zako zingine kuhusu Mwalimu? Kuna mambo mengi tu utakuwa unadanganya watu.Mama...
Hapana sijafeli popote.
Nimeshaeleza mara kadhaa kuwa biashara ya Mama Maria iliyokuwa inafahamika duka liko Mtaa wa Mchikichi kisha duka liko nyumbani kwa Ali Msham ilikuwa ni kuuza mafuta ya taa.
Hata kitabu cha Nyerere (2020) kinaeleza hivyo.
Haya ya kuwa alikuwa anauza na Coca-Cola tumeyajua hivi tuko katika mjadala huu.
Unakusudia niwe na uhakika upi zaidi ya huo hapo juu?
Wewe ulikuwa unaijua historia hii ya Mama Maria niliyokuwekeeni hapa?
Tusianzishe mjadala juu ya mjadala,kama una uwezo wa ku-access profile yake ingia tafuta ktk mijadala aliyo-post humu tafuta thread aliyoianzisha siku Mzee Mkapa amekufa utajua nazungumza nini.Habari ya chombo cha serikali (gazeti la Nationalist) kilichokuwa chini ya Mkapa kuegemea upande mmoja kwenye mgogoro wa EAMWS iliandikwa na Mohamed wakati Mkapa akiwa bado hai.
Tujaribu kuwa balanced.
Ngoja nifafanue kidogo baadhi ya michango ya wamisheni katika kujenga TANU na maisha ya Nyerere. Rafiki mkubwa wa Nyerere alikuwa Andrew Tibandebage ambae walishibana kiasi cha kumpa jina lake mtoto wake wa kwanza. TANU ilipoanzishwa, mweka hazina wake alikuwa John Rupia ambae kwa miaka ya mwanzo alitoa msaada mkubwa wa pesa na mali kwa TANU. Hata safari ya Nyerere ya kwenda UN mwaka 1955 ilifadhiliwa kwa kiasi kikubwa na John Rupia. Mwalimu alipoacha kazi mwaka 1955 ya kufundisha Pugu na kurudi Butiama ni wamisheni wa Maryknoll Fathers ndio walimsaidia kwa kumpa kazi za kutafsiri na kufundisha. Oscar Kambona alipokuwa Katibu Mkuu wa TANU alishiriki sana katika kukikuza chama. John Mwakangale alikuwa mmoja wa viongozi waliojenga TANU katika mikoa ya Kusini. Mchaga Eliufoo alikijenga sana TANU kwa kupitia chama chake cha Chaga Democratic Party. Kuna wakina Kirilo Japhet. Mwalimu alikuwa rafiki mkubwa wa Lady Marion Chesham, settler wa kimarekani. Shilingi 590,408 kati ya shilingi 1,575,981 zilizokusanywa na TANU kati ya Oktoba 1958 na Januari 1960 zilitoka Usukumani halafu unataka kutuambia ni wazee wako wa Gerezani peke yao ndio wanaostahili sifa ya kupigania uhuru wetu? Wangapi wanajua majina ya hao waliochanga hizo pesa?Fundi...
Kuna mambo ambayo wazee wetu walifanyiana kwa hisani mimi siwezi kuyazungumza.
Hapana haja hiyo.
Wenyewe hata juu ya changamoto zilizokuja na uhuru hawakusema.
Lakini ninaloweza kusema na hili linafahamika ni kuwa wafadhili wa TANU Dar es Salaam wanafahamika.
Hao wengine uliowataja hawakupatapo hata siku moja kuwa na Nyerere ubavu kwa ubavu.
Angalia picha za kudai uhuru Nyerere kazungukwa na watu gani?
Nyerere safari ya UNO mkusanyaji fedha za safari ni Iddi Faiz Mafungo na waliokuwa wakipita nyumba kwa nyumba kuchangisha sumni sumni ni Bantu Group akina Juma "Mlevi" Selemani.
Akina mama waliomsindikiza uwanja wa ndege siku ya safari ni Bi. Chiku bint Said Kisusa, Tatu bint Mzee, Titi Mohamed.
Hafla ya kumuaga ilifanyika jengo la Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.
Hii ndiyo historia ya uhuru.
Fundi...Aliyemlipia faini Mwalimu alikuwa nani? Aliyemlipia kwa kiasi kikubwa nauli ya kwenda UN alikuwa nani? Mchango wa Pombeah hujui?
Unataka kutuambia kuwa Mwalimu alisindikizwa uwanja wa ndege na wanawake wa kiislamu peke yao?
Unataka kutuambia aliagwa na waislamu peke yao? Rafiki zake wakina John Rupia, Patrick Kunambi, Andrew Tibandebage , Oscar Kambona na wengine walimuangalia tu akiondoka?
Mbona Mohammed unataka kutufanya wote mazuzu?
Amandla...
Kwanini unadhani kuwa hata angeifahamu historia ya Nyerere kuwekewa sumu asingeiandika?hata ungeifahamu hakika usingeiandika
Dr. Wilbert KleruuIkaamuliwa Abdul aandike historia hiyo na msaidizi wake akawa Dr. Wilbard Kleruu.
.
BAT ni nini?Waeleze wasiojua hapa jinsi Colmore alivyotaka kumtumia mmoja wa wazee wenu kwa ukaribu wake na Nyerere kupata uwakala wa BAT.
Sio Coca Cola tu, nadhani ingekuwa vizuri kama ungetumia neno soda. Naliona tangazo la Fanta pia katika hiyo picha uliyoweka.Algore,
Mama Maria ni mtu mzima sana.
Pana haja gani ya kumuhangaisha na jambo dogo kama hili la mafuta ya taa na Coca-Cola?
1. 32% + 30% + 37% = 99%. What about the 1%?But the 1967 census the total figures for Tanzania Mainland are 32% Christian, 30% Muslim and 37% local belief. This shows Pagans as a leading majority.
Kwani ili mtu aonekane alichangia lazima awe anaonekana yupo na mwalimu kila sehemu ikiwemo hiyo kupiga nae picha? Mzee wetu agenda yako ya udini haiwezi kufanikiwa hata siku moja. Huu uzi wako wa leo ni ushahidi usiotia shaka kwamba wewe ni mzushi na mpotoshaji.Fundi...
Kuna mambo ambayo wazee wetu walifanyiana kwa hisani mimi siwezi kuyazungumza.
Hapana haja hiyo.
Wenyewe hata juu ya changamoto zilizokuja na uhuru hawakusema.
Lakini ninaloweza kusema na hili linafahamika ni kuwa wafadhili wa TANU Dar es Salaam wanafahamika.
Hao wengine uliowataja hawakupatapo hata siku moja kuwa na Nyerere ubavu kwa ubavu.
Angalia picha za kudai uhuru Nyerere kazungukwa na watu gani?
Nyerere safari ya UNO mkusanyaji fedha za safari ni Iddi Faiz Mafungo na waliokuwa wakipita nyumba kwa nyumba kuchangisha sumni sumni ni Bantu Group akina Juma "Mlevi" Selemani.
Akina mama waliomsindikiza uwanja wa ndege siku ya safari ni Bi. Chiku bint Said Kisusa, Tatu bint Mzee, Titi Mohamed.
Hafla ya kumuaga ilifanyika jengo la Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.
Hii ndiyo historia ya uhuru.
British American Tobacco, Kampuni ya sigara iliyokuwepo kabla ya kutaifishwa na kuanzishwa TCC.BAT ni nini?