James Gatz
JF-Expert Member
- Sep 21, 2022
- 301
- 319
Mimi nina nadharia kuwa Mbuwane na Plantan hawakuwa wameupokea Uislam wakati wakipigana kama mercenaries wa Wajerumani. Ila ni nadharia tu, naamini Mohamed Said atakuwa na uelewa zaidi kuhusu jambo hili.Utaona kuwa umekazia ushiriki wa wakristu katika vita ya Maji Maji wakiwa upande wa wajerumani lakini umekaa kimya kuhusu ushiriki wa waislamu wakina Mbuwane na Plantan wakiwa upande wa wajerumani.
Thanks a lot!British American Tobacco, Kampuni ya sigara iliyokuwepo kabla ya kutaifishwa na kuanzishwa TCC.
Mkuu, hauna link ya huo uzi?Tusianzishe mjadala juu ya mjadala,kama una uwezo wa ku-access profile yake ingia tafuta ktk mijadala aliyo-post humu tafuta thread aliyoianzisha siku Mzee Mkapa amekufa utajua nazungumza nini.
Abbas alikabidhiwa kazi gani hasa? Naomba kueleweshwa hapa.Mwalimu hakuchanja "vaccination" kwa hofu ya hujuma za Waingereza.
Kazi hii Abdul alimkabidhi mdogo wake Abbas.
Swali lilikuwa ni nani alilipia tiketi ya Mwalimu na sio suala la "vaccination". Ila hata hapo sijui Mwalimu aliwezaje kuingia Marekani bila kuthibitisha kuwa amechanjwa. Labda useme alipewa cheti cha kufoji. Tiketi ililipiwa kwa kiasi kikubwa na John Rupia. Hilo linakuwia ugumu kulikiri.Fundi...
Unaghadhibika.
Hakuna sababu ya kutumia lugha kali za "mazuzu."
Mimi nimeeleza safari ya Mwalimu ilivyokuwa.
Ikiwa hutaki basi hatuna sababu ya kugombana.
Mipango yote ya safari ilikuwa ikipangwa nyumbani kwa Abdul Sykes ambako Nyerere alikuwa akitoka Pugu kuja mjini anafikia.
Mwalimu hakuchanja "vaccination" kwa hofu ya hujuma za Waingereza.
Kazi hii Abdul alimkabidhi mdogo wake Abbas.
Kweli unaweza kufananisha historia hii na...
Ipo tofauti kubwa.
Kulia Haruna Taratibu, Saadan Abdu Kandoro, Julius Nyerere, Sheikh Mohamed Ramia na Iddi Faiz Mafungo, Dodoma Train Station 1950s
View attachment 2468827
Kushoto: Rashid Sisso, Robert Makange, Zuberi Mtemvu, Iddi Faiz Mafungo, Julius Nyerere, John Rupia, Titi Mohamed wanamsindikiza Nyerere uwanja wa ndege safari ya kwanza UNO 1955
View attachment 2468830
Kulia: Chiku bint Said Kikusa, Titi Mohamed na Kulia ni Tatu bint Mzee na kati ni wanamsindikiza Julius Nyerere safari ya kwanza UNO 1955
Kama hakuchanja lakini alipata cheti cha kuthibitisha kuwa amechanja basi kazi hiyo ilikuwa ya kupata cheti cha magumashi! Na biashara ya vyeti hivi waliendelea nayo hata baada ya uhuru.Abbas alikabidhiwa kazi gani hasa? Naomba kueleweshwa hapa.
Champ...Maisha yote ya Mohamed Said yameegemea kwenye usahihi wa stori alizopewa na Sykes. Yaani ameshupaza shingo miaka yote hii kwa stori za kusimuliwa ambazo ni kinyume na taarifa rasmi.
Waislamu nendeni shule acheni longolongo hapo hamtalazimika kuwachukia wakristo mnapoachwa nyuma. Duka linaonesha bidhaa kibao wewe unalazimisha ni mafuta ya taa na coca cola.
Hakika, ukizingatia na majina yao. Plantan, Shneider, Sykes, Kleist...Mimi nina nadharia kuwa Mbuwane na Plantan hawakuwa wameupokea Uislam wakati wakipigana kama mercenaries wa Wajerumani. Ila ni nadharia tu, naamini Mohamed Said atakuwa na uelewa zaidi kuhusu jambo hili.
Gagnija,Hakika, ukizingatia na majina yao. Plantan, Shneider, Sykes, Kleist...
Gagnija,Hakika, ukizingatia na majina yao. Plantan, Shneider, Sykes, Kleist...
Fundi...Kama hakuchanja lakini alipata cheti cha kuthibitisha kuwa amechanja basi kazi hiyo ilikuwa ya kupata cheti cha magumashi! Na biashara ya vyeti hivi waliendelea nayo hata baada ya uhuru.
Amandla...
Natumia browser mkuu nashindwa kupandisha link hapa kama unatumia Jamiiforums App ingia kwenye profile yake tafuta ktk post alizozianzisha utaukuta.Mkuu, hauna link ya huo uzi?
Fundi...Nimetumia
Swali lilikuwa ni nani alilipia tiketi ya Mwalimu na sio suala la "vaccination". Ila hata hapo sijui Mwalimu aliwezaje kuingia Marekani bila kuthibitisha kuwa amechanjwa. Labda useme alipewa cheti cha kufoji. Tiketi ililipiwa kwa kiasi kikubwa na John Rupia. Hilo linakuwia ugumu kulikiri.
Nimesema unatuonaje kutokana na namna unavyoleta hicho unachoita ushahidi. Kwanza ulibandika picha ya wakina mama wa kiislamu kuthibitisha kuwa ni wao ndio waliomsindikiza airport. Sasa umeongeza nyingine ikionyesha kuwa wakina Robert na John nao walikuwapo! Na wote tunajua kuwa mara nyingi wanaopiga picha ni wachache katika kundi kubwa linalomsindiliza mtu wao. Utaona uliowataja ni saba tu wakati kwenye hiyo picha wako wengi zaidi ya hao. Kwa sababu hiyo kutumia hizi picha kama ushahidi kuwa ni waislamu peke yao ndio waliochangia ukuaji wa TANU ni kutaka kutupotosha.
Hauwezi kumfuta mtu kama Rupia kwa sababu tu jina lake ni John na ukawakuza wakina Iddi na Chiku juu yake. Hiyo sio sahihi. Hauwezi kutenda haki kama lengo lako ni kuwaenzi waislamu wenzako tu. Utakuwa hauna tofauti na wale unaodai hawakutaka kutambua mchango wa wakina Abdul katika mafanikio ya Julius.
Amandla...
James...BAT ni nini?
Waandishi wa hizi historia wengi na ni tofauti,mada zako nyingi zinazungumzia kupondisha historia.Kolola,
Kipande muhimu kimerukwa kukosa kutaja kuwa Mwalimu alikaa kwa Abdul Sykes Mtaa wa Stanley.
Akiwa hapo Mama Maria akafungua duka la mafuta ya taa Mtaa wa Mchikichi.
Haikuelezwa kuwa walipohamia Magomeni Maduka Sita Mama Maria akapewa nafasi ya kuweka duka lake la mafuta nyumbani kwa Ali Msham.
Hii ni historia ya wazee wangu na ni jukumu langu kuhakikisha kuwa inahifadhiwa sawasawa.
Tatizo ukiona umezidiwa hoja unakimbilia mambo ya adabu. Nimemsoma fundi mchundo sijaona adabu aliyokukosea. Mzee wetu siku moja weka wazi kwamba unapigania dini yako na wazee wako wa Kariakoo badala ya kujificha kwenye historia Nyerere huku ukipotosha mambo mengi.Fundi...
Unajua mimi nataabika mjadala unapokosa adabu.
Nakusihi ndugu yangu.
N
Mzee Mohamed Said ulikuwa na miaka 10 mwaka 1962. Kila kitu unachoandika ni kwa kusimuliwa. Katika muktadha huo wewe sio source ya kuaminika kwasababu kwanza uko biased kwenye dini yako lakini pili maelezo yako asilimia kubwa umeyatoa kwa waislamu wenzio ambao mwalimu aliwaweka kando kwasababu walikuwa weupe kichwani.Champ...
Tuchunge lugha na heshima zetu tufanye mjadala wa kupendeza.
Iko siku miaka mingi sisi hatupo watakaokuja kutusoma waseme, "Hakika walipita watu."
Hii si taarifa ya mimi kupewa.
Mimi nimeishi nyakati hizo lau nilikuwa mtoto, baba na babu yangu wameishi nyakati hizo na nimewadiriki wengi ninaowataja hapa.
Wengine nimejuananao kwa karibu sana.
Kitabu cha Abdul Sykes hakina mfano wake katika vitabu vilivyoandikwa kuhusu TANU na historia ya uhuru wa Tanganyika.
Kamsome Listowel (1963) Kimambo na Temu (1969), Uloto (1971), Kivukoni (1981) na Shivji at al (2020) utaona tofauti.
Ndugu yangu si kama najisifu nataka nikuzindue utoke ujingani.
Unatuambia Waislamu twende shule wewe una elimu ya kutosha kufanya mjadala wa mada hiyo?
Ushamsoma Ishumi? (sikumbuki mwaka).
Fungua uzi nitakuja kutoa darsa.
Nisome kwa utulivu na njoo kwangu kwa mjadala kwa adabu na heshima.
Mjadala huu si mahali pa lugha "longolongo."
Hapa nipo kwa kuamini pana heshima.
Mama...Tatizo ukiona umezidiwa hoja unakimbilia mambo ya adabu. Nimemsoma fundi mchundo sijaona adabu aliyokukosea. Mzee wetu siku moja weka wazi kwamba unapigania dini yako na wazee wako wa Kariakoo badala ya kujificha kwenye historia Nyerere huku ukipotosha mambo mengi.
Zeusi,Waandishi wa hizi historia wengi na ni tofauti,mada zako nyingi zinazungumzia kupondisha historia.
Anaepindisha ni nani hasa,je ni makusudi au kutokua historia vizuri?