Makosa ya Musiba, hayalingani na tamaa ya Membe!

Turudi kwenye suala hili la Musiba hoja yako bado haieleweki, kwamba ulifikiri ni kiasi gani alichotakiwa kulipwa au Musiba hakutakiwa kulipa?

Kwa ufahamu wako wa sheria hakuna kosa la defamation?

Unazungumzia uhalisia wa sheria au hisia zako kwa mapenzi yako kwa Musiba?

Ifike wakati tuheshimu sheria, tuthamini utu wa watu huwezi kutukana watu sababu una godfather rais. Haya fanya review kuonyesha mahakama imekosea na Musiba yuko sawa
 
KAma haya ni maoni yako uko sahihi lakini kwa Mujibu wa sheria haupo sawa.

Unapopeleka shauri mahakamani kwamba umechafuliwa lazima uonyeshe athari ulizopata na makahama inapima athari za muda mfupi, wa kati na muda mrefu kisha ndio inaamua kiwango cha fidia.

Pili Membe alikua kiongozi mkubwa lakini pia ni balozi (mwanadiplomasia) hadhi ambayo imejengwa kwa muda mrefu kisha unamchafua maana yake mbele ya jamii ya wanadiplomacia anaonekana mchafu kwa jinsi alivyofanywa na Msiba.

Tatu, Membe aligombea Urais nafasi ya juu kabisa katika nchi alikosa ushiawish labda kwa sababu ya uchafuzi uliofanywa na Musiba. Hivyo alikosa nafasi ya kuwa mkuu wa nchi kwa sababu ya kuharibiwa sifa yake.

Nne, Membe alifukuzwa kwenye chama kutokana na tuhuma hizo, akakosa sifa za kuemdelea kuwa kwenye chama chake alichokitumikia kwa muda zaidi ya 20yrs.

Sifa yake mbele ya wapiga kura wa jimbo lake iliharibiwa.

Membe alizalilishwa mbele ya familia yake, na jamiii kwa ujumla.

Mwisho hadhi yake kimataifa imeshushwa haaminiki kwa lolote na yeyote na hata taasisi mbalimbali, hivyo anakosa sifa kufanya kazi ambazo alikua anafanya kutokana na hadhi yake aliyokuwa nayo.

Hayo na mengine hutumika kama kigezo cha tozo au faini mchafuaji hupaswa kuilipa. Na kuna vigezo maalumu hutumika kwa kila jambo mwisho huamuliwa kiasi cha kulipa.

Tumeona Musiba pia anadaiwa 6billion na Fatma Karume. Vigezo ni jivyo hivyo lakini Fatuma Karume ni 6Billion wakati Membe ni 9 Billion.

Tambua unapotaka kumchafua mtu jua thamani yake kabla ya kumchafua ili yasikukute la Musiba.
 
Yes there you are!!
 
Nenda mkuu kasome tena, mchafue mtu unayeweza kumlipa vinginevyo gharama ya kumchafua mtu ni kubwa sana. Vipo vigezo vinavyotumiwa na mahakama kufikia thamani ya malipo. Kwa membe hiyo ndio hadhi yake.
 
Hivi ww kwa akili yako nani mkorofi kati ya Membe na Musiba?
Kaambiwa amuombe Membe samahani mara ngapi kashupaza shingo?
Lakini wewe ukizushiwa jambo na kudhalilishwa utamfanyeje alokufanyia hayo?
Ok Fatma Karume wakina Mbowe Sufiani na wengineo wote hao ndo wakorofi tu?
Kwani usalama wa taifa hawapo kulinda usalama wa nchi Musiba ndo alikuwa sahihi kuzushia watu mambo?
Jeuri na kiburi ndo shida ya Musiba na mimi nasema kiasi alichoamriwa kulipa ni kidogo sana!
 

Umechambua vizuri sana mleta mada kazi kwako kumtetea huyo Musiba kwamba kosa haliendani na kiasi alichoomba Membe na useme ni kiasi gani kinafaa
 
Umechambua vizuri sana mleta mada kazi kwako kumtetea huyo Musiba kwamba kosa haliendani na kiasi alichoomba Membe na useme ni kiasi gani kinafaa
Nakubaliana na KICHAPO kwa uchambuzi makini kuhusu madai hayo

Na pia nakubaliana na maoni ya wengi tu hapa, nami sipangani na adhabu yoyote kumhusu Msiba

Swali langu ni kwamba, gharama ya kulipa utu wa mtu hua haupo, utatoa kiasi gani kulipia utu wa mtu? Ni hakuna,

Utu utabaki kuwa hauna malipo kufikia gharama zake, shida yangu ni mdai kuamini B 9 ndio kipimo haswaa cha kulipia utu!
 
Na mimi nikuulize hivi thamani ya Membe ni bilioni 9? Katika utumishi wake mapato yake halalI yanafikia hata 20 % ya hiyo anayodai?

Je kama wewe ni mkristo unaweza kuapa kuwa mahakama zetu hazoko biased kama zile za Ulaya?
MImi binafsi naheshimu sheria lakini kinachofanyika kwenye vyombo vya sheria hata wewe unajua.

Yule mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi zanzibar na Membe nani aliathiriiwa zaidi na kashfa? Watu wangeamini kashfa ile huoni ingeweza kusababisha umwagaji mkubwa wa damu zanzibar? Mbona mahakama iliiamuru Mwenyekiti yule wa Tume alipwe milioni 30 tu na Lipumba?



Malumbano katika siasa ni kitu cha kawaida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…