Makosa ya Musiba, hayalingani na tamaa ya Membe!

Makosa ya Musiba, hayalingani na tamaa ya Membe!

I strongly believe kuwa sio sahihi Membe kulipwa kiasi hicho cha pesa. Haya mambo ya kupqta hela kirahisi kirahisi ndio yanafanya wagi wengi wasipende kufanya kazi na badala yakec kufanya misheni tauni. Ni bora mtu akitiwa hatiani afungwe miezi sita kuliko anayedai kukashifiwa kulipwa mamilioni bika jasho.

Mahakama huwa zinakosea ndio maana kuna rufaa na reviews.
Turudi kwenye suala hili la Musiba hoja yako bado haieleweki, kwamba ulifikiri ni kiasi gani alichotakiwa kulipwa au Musiba hakutakiwa kulipa?

Kwa ufahamu wako wa sheria hakuna kosa la defamation?

Unazungumzia uhalisia wa sheria au hisia zako kwa mapenzi yako kwa Musiba?

Ifike wakati tuheshimu sheria, tuthamini utu wa watu huwezi kutukana watu sababu una godfather rais. Haya fanya review kuonyesha mahakama imekosea na Musiba yuko sawa
 
Sitetei chochote kuhusu yaliyojiri kumhusu mh Membe yakimhusisha mmiliki wa magazeti ya Tanzanite kumdhalilisha mh Membe kwa kumchafua, ila naiona tamaa kubwa isiyo na mantiki kutoka kwa mh Bernard Membe ya kutaka ujira mkubwa usiolingana na kile wengi wanakiita ni kudhalilishwa

Hata tungelimshirikisha asiye na akili kuhusu madai hayo ya bilioni 9 kwa kosa tu la kuandikwa vibaya Mh Membe kwenye gazeti, nina hakika angelicheka kwa huzuni na mshangao

Naamini pia hata watoto wake ikiwa wana utu tu wa mbaali kabisa, wanaishangaa hii hukumu na tamaa iliyopitiza kiwango!

Msiba anayo makosa makubwa na hahitaji kutetewa, lakini bilioni 9 kwa kosa hilo, ni tamaa ya mlipwaji na inamdhalilisha mlipwaji

J.mosi njema
KAma haya ni maoni yako uko sahihi lakini kwa Mujibu wa sheria haupo sawa.

Unapopeleka shauri mahakamani kwamba umechafuliwa lazima uonyeshe athari ulizopata na makahama inapima athari za muda mfupi, wa kati na muda mrefu kisha ndio inaamua kiwango cha fidia.

Pili Membe alikua kiongozi mkubwa lakini pia ni balozi (mwanadiplomasia) hadhi ambayo imejengwa kwa muda mrefu kisha unamchafua maana yake mbele ya jamii ya wanadiplomacia anaonekana mchafu kwa jinsi alivyofanywa na Msiba.

Tatu, Membe aligombea Urais nafasi ya juu kabisa katika nchi alikosa ushiawish labda kwa sababu ya uchafuzi uliofanywa na Musiba. Hivyo alikosa nafasi ya kuwa mkuu wa nchi kwa sababu ya kuharibiwa sifa yake.

Nne, Membe alifukuzwa kwenye chama kutokana na tuhuma hizo, akakosa sifa za kuemdelea kuwa kwenye chama chake alichokitumikia kwa muda zaidi ya 20yrs.

Sifa yake mbele ya wapiga kura wa jimbo lake iliharibiwa.

Membe alizalilishwa mbele ya familia yake, na jamiii kwa ujumla.

Mwisho hadhi yake kimataifa imeshushwa haaminiki kwa lolote na yeyote na hata taasisi mbalimbali, hivyo anakosa sifa kufanya kazi ambazo alikua anafanya kutokana na hadhi yake aliyokuwa nayo.

Hayo na mengine hutumika kama kigezo cha tozo au faini mchafuaji hupaswa kuilipa. Na kuna vigezo maalumu hutumika kwa kila jambo mwisho huamuliwa kiasi cha kulipa.

Tumeona Musiba pia anadaiwa 6billion na Fatma Karume. Vigezo ni jivyo hivyo lakini Fatuma Karume ni 6Billion wakati Membe ni 9 Billion.

Tambua unapotaka kumchafua mtu jua thamani yake kabla ya kumchafua ili yasikukute la Musiba.
 
Mimi kwa mtazamo wangu musiba atume wazee kwa mh membe wakae wazungumzie hiyo bili ya mahakama waombane radhi huenda yakaisha huu ndio mtizamo wangu
IMG_20230425_193317_285.jpg
 
Kesi ya defamation unaweza lipishwa hata billion 900, unakumbuka ile kesi ya Mengi na Manji km sijakosea Mengi aliombwa kulipwa cent 5 tu sio shilling cent 5 na Kesi iliishia hapo, defamation unaiomba Mahakama ulipwe kutokana na damage ulizozipata baada ya kuchafuliwa hata billion 900 ikiwezekena
Yes there you are!!
 
Hoja zangu ziko clear.

Ila ninachoamini sio haki Mtu yeyote kudai alipwe kiasi hicho bure bure. Musiba hakumtia hasara yeyote Membe. Malumbano katika siasa ni kawaida na kama kuna mwqnasiasa hataki kuchafuliwa basi asiwe mwanasiasaa. Sio vizuri kutumia mahakama kumkomoa hasmu wako kisiasa.

Hizo mahakama zinaweza kuwa abused sana,, ripoti ya rushwa ya Warioba moja ya taasidi zilizolalamikiwa kwa rushwa ni mahakama.

KUomba radhi kabla ya hukumu ni hiyari, ila baada ya mahakamac kumtia mtu hatiani inaweza kuagiza mhusika aombe radhi hafharani na hapo ndoo huwa lazima.
Nenda mkuu kasome tena, mchafue mtu unayeweza kumlipa vinginevyo gharama ya kumchafua mtu ni kubwa sana. Vipo vigezo vinavyotumiwa na mahakama kufikia thamani ya malipo. Kwa membe hiyo ndio hadhi yake.
 
Hivi ww kwa akili yako nani mkorofi kati ya Membe na Musiba?
Kaambiwa amuombe Membe samahani mara ngapi kashupaza shingo?
Lakini wewe ukizushiwa jambo na kudhalilishwa utamfanyeje alokufanyia hayo?
Ok Fatma Karume wakina Mbowe Sufiani na wengineo wote hao ndo wakorofi tu?
Kwani usalama wa taifa hawapo kulinda usalama wa nchi Musiba ndo alikuwa sahihi kuzushia watu mambo?
Jeuri na kiburi ndo shida ya Musiba na mimi nasema kiasi alichoamriwa kulipa ni kidogo sana!
 
KAma haya ni maoni yako uko sahihi lakini kwa Mujibu wa sheria haupo sawa.

Unapopeleka shauri mahakamani kwamba umechafuliwa lazima uonyeshe athari ulizopata na makahama inapima athari za muda mfupi, wa kati na muda mrefu kisha ndio inaamua kiwango cha fidia.

Pili Membe alikua kiongozi mkubwa lakini pia ni balozi (mwanadiplomasia) hadhi ambayo imejengwa kwa muda mrefu kisha unamchafua maana yake mbele ya jamii ya wanadiplomacia anaonekana mchafu kwa jinsi alivyofanywa na Msiba.

Tatu, Membe aligombea Urais nafasi ya juu kabisa katika nchi alikosa ushiawish labda kwa sababu ya uchafuzi uliofanywa na Musiba. Hivyo alikosa nafasi ya kuwa mkuu wa nchi kwa sababu ya kuharibiwa sifa yake.

Nne, Membe alifukuzwa kwenye chama kutokana na tuhuma hizo, akakosa sifa za kuemdelea kuwa kwenye chama chake alichokitumikia kwa muda zaidi ya 20yrs.

Sifa yake mbele ya wapiga kura wa jimbo lake iliharibiwa.

Membe alizalilishwa mbele ya familia yake, na jamiii kwa ujumla.

Mwisho hadhi yake kimataifa imeshushwa haaminiki kwa lolote na yeyote na hata taasisi mbalimbali, hivyo anakosa sifa kufanya kazi ambazo alikua anafanya kutokana na hadhi yake aliyokuwa nayo.

Hayo na mengine hutumika kama kigezo cha tozo au faini mchafuaji hupaswa kuilipa. Na kuna vigezo maalumu hutumika kwa kila jambo mwisho huamuliwa kiasi cha kulipa.

Tumeona Musiba pia anadaiwa 6billion na Fatma Karume. Vigezo ni jivyo hivyo lakini Fatuma Karume ni 6Billion wakati Membe ni 9 Billion.

Tambua unapotaka kumchafua mtu jua thamani yake kabla ya kumchafua ili yasikukute la Musiba.

Umechambua vizuri sana mleta mada kazi kwako kumtetea huyo Musiba kwamba kosa haliendani na kiasi alichoomba Membe na useme ni kiasi gani kinafaa
 
Umechambua vizuri sana mleta mada kazi kwako kumtetea huyo Musiba kwamba kosa haliendani na kiasi alichoomba Membe na useme ni kiasi gani kinafaa
Nakubaliana na KICHAPO kwa uchambuzi makini kuhusu madai hayo

Na pia nakubaliana na maoni ya wengi tu hapa, nami sipangani na adhabu yoyote kumhusu Msiba

Swali langu ni kwamba, gharama ya kulipa utu wa mtu hua haupo, utatoa kiasi gani kulipia utu wa mtu? Ni hakuna,

Utu utabaki kuwa hauna malipo kufikia gharama zake, shida yangu ni mdai kuamini B 9 ndio kipimo haswaa cha kulipia utu!
 
Turudi kwenye suala hili la Musiba hoja yako bado haieleweki, kwamba ulifikiri ni kiasi gani alichotakiwa kulipwa au Musiba hakutakiwa kulipa?

Kwa ufahamu wako wa sheria hakuna kosa la defamation?

Unazungumzia uhalisia wa sheria au hisia zako kwa mapenzi yako kwa Musiba?

Ifike wakati tuheshimu sheria, tuthamini utu wa watu huwezi kutukana watu sababu una godfather rais. Haya fanya review kuonyesha mahakama imekosea na Musiba yuko sawa
Na mimi nikuulize hivi thamani ya Membe ni bilioni 9? Katika utumishi wake mapato yake halalI yanafikia hata 20 % ya hiyo anayodai?

Je kama wewe ni mkristo unaweza kuapa kuwa mahakama zetu hazoko biased kama zile za Ulaya?
MImi binafsi naheshimu sheria lakini kinachofanyika kwenye vyombo vya sheria hata wewe unajua.

Yule mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi zanzibar na Membe nani aliathiriiwa zaidi na kashfa? Watu wangeamini kashfa ile huoni ingeweza kusababisha umwagaji mkubwa wa damu zanzibar? Mbona mahakama iliiamuru Mwenyekiti yule wa Tume alipwe milioni 30 tu na Lipumba?

Malumbano katika siasa ni kitu cha kawaida.
 
Back
Top Bottom