Sitetei chochote kuhusu yaliyojiri kumhusu mh Membe yakimhusisha mmiliki wa magazeti ya Tanzanite kumdhalilisha mh Membe kwa kumchafua, ila naiona tamaa kubwa isiyo na mantiki kutoka kwa mh Bernard Membe ya kutaka ujira mkubwa usiolingana na kile wengi wanakiita ni kudhalilishwa
Hata tungelimshirikisha asiye na akili kuhusu madai hayo ya bilioni 9 kwa kosa tu la kuandikwa vibaya Mh Membe kwenye gazeti, nina hakika angelicheka kwa huzuni na mshangao
Naamini pia hata watoto wake ikiwa wana utu tu wa mbaali kabisa, wanaishangaa hii hukumu na tamaa iliyopitiza kiwango!
Msiba anayo makosa makubwa na hahitaji kutetewa, lakini bilioni 9 kwa kosa hilo, ni tamaa ya mlipwaji na inamdhalilisha mlipwaji
J.mosi njema
KAma haya ni maoni yako uko sahihi lakini kwa Mujibu wa sheria haupo sawa.
Unapopeleka shauri mahakamani kwamba umechafuliwa lazima uonyeshe athari ulizopata na makahama inapima athari za muda mfupi, wa kati na muda mrefu kisha ndio inaamua kiwango cha fidia.
Pili Membe alikua kiongozi mkubwa lakini pia ni balozi (mwanadiplomasia) hadhi ambayo imejengwa kwa muda mrefu kisha unamchafua maana yake mbele ya jamii ya wanadiplomacia anaonekana mchafu kwa jinsi alivyofanywa na Msiba.
Tatu, Membe aligombea Urais nafasi ya juu kabisa katika nchi alikosa ushiawish labda kwa sababu ya uchafuzi uliofanywa na Musiba. Hivyo alikosa nafasi ya kuwa mkuu wa nchi kwa sababu ya kuharibiwa sifa yake.
Nne, Membe alifukuzwa kwenye chama kutokana na tuhuma hizo, akakosa sifa za kuemdelea kuwa kwenye chama chake alichokitumikia kwa muda zaidi ya 20yrs.
Sifa yake mbele ya wapiga kura wa jimbo lake iliharibiwa.
Membe alizalilishwa mbele ya familia yake, na jamiii kwa ujumla.
Mwisho hadhi yake kimataifa imeshushwa haaminiki kwa lolote na yeyote na hata taasisi mbalimbali, hivyo anakosa sifa kufanya kazi ambazo alikua anafanya kutokana na hadhi yake aliyokuwa nayo.
Hayo na mengine hutumika kama kigezo cha tozo au faini mchafuaji hupaswa kuilipa. Na kuna vigezo maalumu hutumika kwa kila jambo mwisho huamuliwa kiasi cha kulipa.
Tumeona Musiba pia anadaiwa 6billion na Fatma Karume. Vigezo ni jivyo hivyo lakini Fatuma Karume ni 6Billion wakati Membe ni 9 Billion.
Tambua unapotaka kumchafua mtu jua thamani yake kabla ya kumchafua ili yasikukute la Musiba.