Sitetei chochote kuhusu yaliyojiri kumhusu mh Membe yakimhusisha mmiliki wa magazeti ya Tanzanite kumdhalilisha mh Membe kwa kumchafua, ila naiona tamaa kubwa isiyo na mantiki kutoka kwa mh Bernard Membe ya kutaka ujira mkubwa usiolingana na kile wengi wanakiita ni kudhalilishwa
Hata tungelimshirikisha asiye na akili kuhusu madai hayo ya bilioni 9 kwa kosa tu la kuandikwa vibaya Mh Membe kwenye gazeti, nina hakika angelicheka kwa huzuni na mshangao
Naamini pia hata watoto wake ikiwa wana utu tu wa mbaali kabisa, wanaishangaa hii hukumu na tamaa iliyopitiza kiwango!
Msiba anayo makosa makubwa na hahitaji kutetewa, lakini bilioni 9 kwa kosa hilo, ni tamaa ya mlipwaji na inamdhalilisha mlipwaji
J.mosi njema
Mtoa mada sababu huna akili na hujapenda kushughulisha akili yako na hujapenda kujipanga ngoja tukupange sasa.. Iko hivi
Fine ya 9B kwa Musiba dhidi ya Bwana Membe ni kubwa kweli tena kubwa sana sana na hii imetolewa kwa kuweka sawa Musiba ili akutane na kifungo jela
Kwa taarifa yako ni kwamba Bwana Musiba atashindwa kulipa deni la 9B hata kama watauza mali zak zote,wakiuza mali zake zote na deni likabaki, itapigwa hesabu ni kiasi gani kimebaki cha deni ili Bwana Membe amulipie Bwana Musiba gharama za Tshs 5,000/= kwa siku aende gherezani.
Na ndiyo mchongo uliopo hapa, hela za mali zake zitakazouzwa, ndiyo zitatumika hizo hizo kumpeleka gerezani.. Kwenye hili naunga mkono na miguu juu, ili iwe fundisho kwa watu wajinga aina ya Musiba kuweka akili kabatini nakutumia makalio kuwaza
Musiba kawatukana sana watu na Serikali ilikua kimya tu, wale kina Makamba,Kinana,January,Nape,Ngeleja,Membe walidukuliwa maongezi yao, kitu ambacho ni kosa sana kudukuwa faragha za watu..
Mbaya zaidi alimtukana hadi brother men, mtoto wa mjini.. Mr tabasamu! Musiba ache akawe chakula cha watu huko Segelea