Makundi mbalimbali ya Watanzania wanaoichukia serikali ya Rais Magufuli na kwanini wanaichukia...

Makundi mbalimbali ya Watanzania wanaoichukia serikali ya Rais Magufuli na kwanini wanaichukia...

adolay,
You know what I am talking about, usijaribu kupotosha watu.
 
Unamfukuza kazi Polisi, mwalimu, daktari na askari magereza lakini unamuacha mwanajeshi mwenye vyeti feki kisa akirudi mtaani atakuwa jambazi. Hawa watu utawalaumu bure lazima watakuchukia tu kwasababu sheria imepindishwa. Yule mkuu mkoa watu walilalamika sana kuwa anatumia cheti cha mtu lakini majibu yalikuwa hivi "Ukuu wa mkoa hautaji vyeti ni utendaji kazi tu" Sheria inasemaje ukiwa una vyeti feki? Zoezi nililipenda sana ila liliendeshwa kwa chuki na ubaguzi.

Mfano:
Ni marufuku kuingia hotel hii ukiwa umevaa tshirt na jeans. Wewe umevaa na kiongozi fulani kavaa sasa mnafika kwenye hiyo hotel, yeye anaruhusiwa ila wewe unarudishwa. Utajisikiaje? Ni makosa ila kitakachokuuma zaidi, kwanini yeye aruhusiwe wakati mna makosa yanayofanana.
ii).Watu waliokuwa na vyeti feki ambao walienguliwa katika kazi zao.
 
McMahoon,
Naamini huna ushahidi usio shaka kwamba wapo Askari Polisi na Wanajeshi ambao wana vyeti fake.
 
1. Hilo zoezi la vyeti feki lilifika JWTZ?
2. (A) Raisi, wabunge, mawaziri, madiwani, wenyekiti, wakuu wa mikoa na wilaya ni watumishi wa umma? kama jibu ni ndiyo kwanini zoezi halikupita kwao?
(B) Wao si watanzania mpaka zoezi lisifike kwao?
3. Kama mtu amefanya kazi miaka 6 utasema hana ujuzi wowote kwasababu ana vyeti feki?
Kama yeye aliamua atumbue baadhi ya watu na wengine kuwaacha, sioni umuhimu wa wewe kuumia kisa kuna makundi ya watu wanaomchukia na serikali yake.
Naamini huna ushahidi usio shaka kwamba wapo Askari Polisi na Wanajeshi ambao wana vyeti fake.
 
Nadhani kundi lako wewe ni hili,"4.Wafuata upepo wasiokuwa na mawazo yao original,kwa vile hawana ufahamu wa kutosha,kwa hiyo wanadakia kila wazo hata baya,na hivyo kupotosha umma."
 
Nadhani kundi lako wewe ni hili,"4.Wafuata upepo wasiokuwa na mawazo yao original,kwa vile hawana ufahamu wa kutosha,kwa hiyo wanadakia kila wazo hata baya,na hivyo kupotosha umma."

Wewe bwana wewe

Usidhani you're better than others
 
areafiftyone,
Waza haya...
1. Unategemea aliyekuwa anauza mbaazi shilingi 3,000/- kwa kilo, na leo hii, kilo hiyo hiyo ya mbaazi auze kwa Tshs 150/- ATAMPENDA?

2. Yule ambaye hadi leo bado halipwa korosho zake zilizokopwa na serikali, unategemea ampende?

3. Unategemea mtu aliyelipa kodi, halafu aje aambiwe 1.5T hazijulikani zilipo, atampenda?

4. Unategemea familia, ndugu, jamaa na marafiki wa Ben Saanane, watampenda? Wa Lissu je? Wa Azoli? Wa Akwilina nao?

5. Unategemea familia, ndugu, jamaa na marafiki wa Kangi ALIYETUMBULIWA KWA KEBEHI KWA KOSA LA KUFANYA MAMBOI BILA KUPITIA BUNGEA WATAMPENDA WAKATI NA YEYE ZILE NDEGE, UWANJA WA CHATO, SGR etc vyote hivyo havijapita bungeni..!!??

6. Unategemea waliofukuzwa kazi kwa kosa la vyeti feki huku wakimuona "YUSUPH" aiendelea na kazi, watampenda?
 
areafiftyone,
Ndugu..
Ukishakuwa mkandamizaji wa demokrasia na haki za binadamu kama anavyofanya Magufuli hata ufanye jema vipi huwezi kukubalika..
Magufuli kuna watu wapo mahabusu kwasababu tu wamemkosoa..kuna viongozi wa vyama vya upinzani kwa kesi za kubambikiwa kwa amri zake..
Huyu anaendesha Nchi kwa double standard huyu anafanya kosa haguswi huyu anafanya kosa lile lile anakamatwa..
Unataka Kiongozi wa namna hiyo akubalike kwa lipi..??
 
Huyo Rais wako:

1.Kaua sekta binafsi - Biashara, elimu na uwekezaji.

2. Kaua ajira rasmi na zisizo rasmi.

3. Katumia madaraka yake kwa ulevi wa kupindukia kwa kuvunja na Kuidharau katiba katika nyakati tofauti tofauti.

3. Kalemaza mihimili ya nchi kwa kutengeneza bureaucratic competition na kuwafanya wakuu wa mihimili kufanya kazi kwa hofu na kutegemea kupewa fadhila.

4.Katengeneza mfumo wa kidikteta ambapo yeye ndiye mungu mkuu na matamko yake ni sheria kwa kila mtu!

5. Kawapuuza watumishi wa umma kuhusu madai yao na nyongeza za mishahara.

6. Katumia mabilioni ya fedha bila ridhaa ya bunge kufanya manunuzi ya toys bila kujali vipaumbele muhimu vya nchi kama vile ajira kwa vijana.

7.Kaishusha hadhi ofisi ya Rais kwa ushamba na kutoelewa fundamentals za namna Rais anapaswa kutenda!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
GODZILLA,
Angalau angekuja hapa na kuyakanusha uliyoandika tungejua kuwa kweli anamsimamo madhubuti kuhusu hayo aliyoandika mleta mada.
Lakini tunajua watu kama hawa ni wachumia tumbo tu hawana lolote wanalolisimamia.
 
Kwahiyo fisiemu wakituma polisi wachukue sanduku la kura wakimbie nalo
Tuwapigie makofi

Wakiuwa watu tushangilie

Wakiteka watu tuseme asante

Wakisaini mikataba ya kijambazi tuwape kongole

Wakimuua Akwilina tusiwakemee

Wakivamia Clouds tuwavumilie

Hatuwezi kuwa na uzalendo kwa sisiemu na kwa Magufuli, sisi ni wazalendo kwa Tanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waza haya...
1. Unategemea aliyekuwa anauza mbaazi shilingi 3,000/- kwa kilo, na leo hii, kilo hiyo hiyo ya mbaazi auze kwa Tshs 150/- ATAMPENDA?

2. Yule ambaye hadi leo bado halipwa korosho zake zilizokopwa na serikali, unategemea ampende?

3. Unategemea mtu aliyelipa kodi, halafu aje aambiwe 1.5T hazijulikani zilipo, atampenda?

4. Unategemea familia, ndugu, jamaa na marafiki wa Ben Saanane, watampenda? Wa Lissu je? Wa Azoli? Wa Akwilina nao?

5. Unategemea familia, ndugu, jamaa na marafiki wa Kangi ALIYETUMBULIWA KWA KEBEHI KWA KOSA LA KUFANYA MAMBOI BILA KUPITIA BUNGEA WATAMPENDA WAKATI NA YEYE ZILE NDEGE, UWANJA WA CHATO, SGR etc vyote hivyo havijapita bungeni..!!??

6. Unategemea waliofukuzwa kazi kwa kosa la vyeti feki huku wakimuona "YUSUPH" aiendelea na kazi, watampenda?
'Areafifty' alibadili 'avatar' akidhani tendo hilo litamwongezea akili kichwani, kumbe ndio anazidi kudidimia kabisa.
 
Back
Top Bottom