Tumeshudia Rais Magufuli akitukanwa kwa sababu zisizo za msingi kabisa,tena wakati mwingine kwa kufanya mambo ya msingi ambayo kama nchi tunayahitaji.Tumeshuaudia pia akibezwa na kudharauliwa.Lakini ni akina nani hasa wanahusika na vitendo hivi ambavyo si vya kiungwana kabisa, vyenye nia ovu ya kumkatisha Rais tamaa?Nimewagawanya watu hawa kwenye makundi mbali mbali. Makundi hayo na sababu ni kama ifuatavyo:-
1.Watu hao inawezekana kabisa kuwa ni vibaraka wa mabepari na nchi za magharibi,waliotumwa kukejeli na kujifanya wanadharau kila jambo jema,ili serikali ya awamu ya tano,ionekane si lolote si chochote,na hatimaye kudharaulika na wananchi.Watu wa aina hii serikali inapofanikiwa katika jambo lolote,wanaona kama hawajafanikiwa katika kazi waliyotumwa kuifanya.Lakini naomba tukumbuke kwamba mti kwenye matunda ndio unaopigwa mawe,kwa hiyo Magufuli ana matunda!
2.Lakini wapo pia watu wa vyama vya upinzani,hasa CHADEMA.Hawa kama vibaraka,nao wanatetea matumbo yao,so ni lazima wakosoe kila kitu,ili kuhalalisha uwepo wao.Wasipo onyesha kwamba serikali inakosea na haina inachofanya,kwa hiyo tunahitaji mabadiliko,uwepo wao utakuwa hauna maana.
3.Wengine ni watu ambao wameguswa moja kwa moja na utendaji wa Magufuli kwa njia moja au nyingine,ambayo imechangia maslahi yao ya kiuchumi kuathirika.Hapa yako makundi mengi,na si rahisi kuyataja yote.Hata hivyo naomba nitaje makundi machache tu.
i).Hawa wanaweza kuwa wana CCM ambao walikuwa wanafaidika na mihela ya mafisadi waliokuwa wanaifadhili CCM.
ii).Watu waliokuwa na vyeti feki ambao walienguliwa katika kazi zao.
iii).Wafanyibiashara ambao walikuwa hawalipi kodi inavyotakiwa. iv).Wafanyabiashara waliokuwa wanafanya biashara zenye utata na zisizo halali kama Bureau de Change,na sasa biashara zao zimeathirika au kufutiliwa mbali.
v).Watumishi waliokuwa wanaiibia serikali kwa mbinu zozote zile,na mbinu hizo sasa hazipo tena.
vi).Wauza madawa ya kulevya kwa sababu zilizo wazi.
vii).Watumishi wazembe na wasio na weledi.Hawa wanaona maisha ya kazi katika zama za Magufuli ni taabu sana.No wonder watumishi wengi wanatamani muda wao wa kustaafu ufike haraka.
viii)Watumishi waliohamishiwa Dodoma na kuacha miradi na majumba yao Dar es Salaam.
ix)Wafanyabiashara wa malori makubwa na mabasi hasa wa ukanda wa Dar-Kigoma,Dar-Mwanza,Dar-Arusha,Tanga-Arusha.Hawa wanahofia biashara zao kuathirika baada ya ujio wa SGR na kuboresha kwa reli ya Dar-Arusha na Tanga-Arusha.
x)Ndugu wa makundi hayo hapo juu.
4.Wafuata upepo wasiokuwa na mawazo yao original,kwa vile hawana ufahamu wa kutosha,kwa hiyo wanadakia kila wazo hata baya,na hivyo kupotosha umma.
Nimesema si rahisi kutaja makundi yote,itoshe tu kusema kwamba hayo kwa leo yanatosha.