Makundi mbalimbali ya Watanzania wanaoichukia serikali ya Rais Magufuli na kwanini wanaichukia...

Makundi mbalimbali ya Watanzania wanaoichukia serikali ya Rais Magufuli na kwanini wanaichukia...

Tumeshudia Rais Magufuli akitukanwa kwa sababu zisizo za msingi kabisa,tena wakati mwingine kwa kufanya mambo ya msingi ambayo kama nchi tunayahitaji.Tumeshuaudia pia akibezwa na kudharauliwa.Lakini ni akina nani hasa wanahusika na vitendo hivi ambavyo si vya kiungwana kabisa, vyenye nia ovu ya kumkatisha Rais tamaa?Nimewagawanya watu hawa kwenye makundi makuu manne Makundi hayo na sababu ni kama ifuatavyo:-

1.Watu hao inawezekana kabisa kuwa ni vibaraka wa mabepari na nchi za magharibi,waliotumwa kukejeli na kujifanya wanadharau kila jambo jema,ili serikali ya awamu ya tano,ionekane si lolote si chochote,na hatimaye kudharaulika na wananchi.Watu wa aina hii serikali inapofanikiwa katika jambo lolote,wanaona kama hawajafanikiwa katika kazi waliyotumwa kuifanya.Lakini naomba tukumbuke kwamba mti kwenye matunda ndio unaopigwa mawe,kwa hiyo Magufuli ana matunda!

2.Lakini wapo pia watu wa vyama vya upinzani,hasa CHADEMA.Hawa kama vibaraka,nao wanatetea matumbo yao,so ni lazima wakosoe kila kitu,ili kuhalalisha uwepo wao.Wasipo onyesha kwamba serikali inakosea na haina inachofanya,kwa hiyo tunahitaji mabadiliko,uwepo wao utakuwa hauna maana.

3.Wengine ni watu ambao wameguswa moja kwa moja na utendaji wa Magufuli kwa njia moja au nyingine,ambayo imechangia maslahi yao ya kiuchumi kuathirika.Hapa yako makundi mengi,na si rahisi kuyataja yote.Hata hivyo naomba nitaje makundi machache tu.
i).Hawa wanaweza kuwa wana CCM ambao walikuwa wanafaidika na mihela ya mafisadi waliokuwa wanaifadhili CCM.

ii).Watu waliokuwa na vyeti feki ambao walienguliwa katika kazi zao.

iii).Wafanyibiashara ambao walikuwa hawalipi kodi inavyotakiwa,na hivyo kuiibia serikali.

iv).Wafanyabiashara waliokuwa wanafanya biashara zenye utata na zisizo halali kama Bureau de Change,na sasa biashara zao zimeathirika au kufutiliwa mbali.

v).Watumishi waliokuwa wanaiibia serikali kwa mbinu zozote zile,na mbinu hizo sasa hazipo tena.

vi).Wauza madawa ya kulevya kwa sababu zilizo wazi.

vii).Watumishi wazembe na wasio na weledi.Hawa wanaona maisha ya kazi katika zama za Magufuli ni taabu sana.No wonder watumishi wengi wanatamani muda wao wa kustaafu ufike haraka.

viii)Watumishi waliohamishiwa Dodoma na kuacha miradi na majumba yao Dar es Salaam.

ix)Wafanyabiashara wa malori makubwa na mabasi,hasa wa ukanda wa Dar-Kigoma,Dar-Mwanza,Dar-Arusha,Tanga-Arusha.Hawa wanahofia biashara zao kuathirika baada ya ujio wa SGR na kuboreshwa kwa reli ya Dar-Arusha na Tanga-Arusha.Nadhani mnakumbuka incidence ambayo mmiliki wa mabasi ya kampuni fulani alishiriki kung'oa mataruma ya reli ya Moshi-Arusha.Episode ile ina-prove kwamba point hii ni kweli.

x)Ndugu wa makundi hayo hapo juu.

4.Wafuata upepo wasiokuwa na mawazo yao original,kwa vile hawana ufahamu wa kutosha,kwa hiyo wanadakia kila wazo hata baya,na hivyo kupotosha umma.

Naomba nimalizie kwa kusema tena,kwamba si rahisi kutaja makundi yote,kwa hiyo naomba kwa leo niishie hapo.
Ongeza hapo kundi la watumishi wa uma wasio na madaraka wanaotegemea mshaara na tangu aingie jamaa hakuna nyongeza wala madaraja ambayo ni haki yao.

Weka pia watumishi ambao walisomeshwa kwa mkopo wa bodi ya mkopo na kuongezewa makato ya mkopo kufanya maisha kuwa magumu zaidi. Badala ya kuongeza mshaara serikali ikaona iongeze makato. Makundi saddist ni mengi kuliko wanaofurahia maisha awamu hii.

Siku nyingine ulete pia makundi ya wanaofurahia life kipindi hiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio kwl mtoa mada...yote uliyoyazungmza ama kuyandika..nikulize wewe. Je idadi ya wanaokosa ajira inakurdhisha?je mwenendo wa kuporomoka kwa sekta binafsi unakufurahisha? Je mwenendo wa democrasia kwenye taifa letu unakufurahisha? Je Sera ya kilimo kuhusu uzalishaji na masoko unakufurahisha? Je mfumo wa kuadhibu watu ama kwa kupoteza au kufungulia kesi za uhujumu uchumi watu paspokufuata sheria kunakufurahisha? Semeni ukweli ili system ijifunze inapokosea nchi hii ni yetu sote hakuna atakayeondoka nayo akifa!!
Kumbukeni tunahtaji kutenda mema ili vzazi vyetu vije vijifunze ustaarabu wetu!!! areafiftyone,

Sent using Jamii Forums mobile app
Je kuwa na sera za majukwaani (nyuma ya mikamera) kuna furahisha, kuwa na sera ambazo hazidumu kuna furahisha., kukataa habari za kiuchunguzi kuna furahisha n.k
 
Back
Top Bottom