Makundi mbalimbali ya Watanzania wanaoichukia serikali ya Rais Magufuli na kwanini wanaichukia...

Makundi mbalimbali ya Watanzania wanaoichukia serikali ya Rais Magufuli na kwanini wanaichukia...

Acha hizo wewe,wanalipwa na tunajua.Kama hujui ni we we.Kwani Kabendera alikuwa halipwi na Rothschild.
Kampeni za wambea hizi😂. Na sisi tunalipwa sio mnafikiri Watanzania ni wajinga hivyo😂😂. Magu naye ataondoka siku tunapenda maendeleo lakini sio kinyanyasana.
 
Tumeshudia Rais Magufuli akitukanwa kwa sababu zisizo za msingi kabisa,tena wakati mwingine kwa kufanya mambo ya msingi ambayo kama nchi tunayahitaji.Tumeshuaudia pia akibezwa na kudharauliwa.Lakini ni akina nani hasa wanahusika na vitendo hivi ambavyo si vya kiungwana kabisa, vyenye nia ovu ya kumkatisha Rais tamaa?Nimewagawanya watu hawa kwenye makundi makuu manne Makundi hayo na sababu ni kama ifuatavyo:-

1.Watu hao inawezekana kabisa kuwa ni vibaraka wa mabepari na nchi za magharibi,waliotumwa kukejeli na kujifanya wanadharau kila jambo jema,ili serikali ya awamu ya tano,ionekane si lolote si chochote,na hatimaye kudharaulika na wananchi.Watu wa aina hii serikali inapofanikiwa katika jambo lolote,wanaona kama hawajafanikiwa katika kazi waliyotumwa kuifanya.Lakini naomba tukumbuke kwamba mti kwenye matunda ndio unaopigwa mawe,kwa hiyo Magufuli ana matunda!

2.Lakini wapo pia watu wa vyama vya upinzani,hasa CHADEMA.Hawa kama vibaraka,nao wanatetea matumbo yao,so ni lazima wakosoe kila kitu,ili kuhalalisha uwepo wao.Wasipo onyesha kwamba serikali inakosea na haina inachofanya,kwa hiyo tunahitaji mabadiliko,uwepo wao utakuwa hauna maana.

3.Wengine ni watu ambao wameguswa moja kwa moja na utendaji wa Magufuli kwa njia moja au nyingine,ambayo imechangia maslahi yao ya kiuchumi kuathirika.Hapa yako makundi mengi,na si rahisi kuyataja yote.Hata hivyo naomba nitaje makundi machache tu.
i).Hawa wanaweza kuwa wana CCM ambao walikuwa wanafaidika na mihela ya mafisadi waliokuwa wanaifadhili CCM.

ii).Watu waliokuwa na vyeti feki ambao walienguliwa katika kazi zao.

iii).Wafanyibiashara ambao walikuwa hawalipi kodi inavyotakiwa,na hivyo kuiibia serikali.

iv).Wafanyabiashara waliokuwa wanafanya biashara zenye utata na zisizo halali kama Bureau de Change,na sasa biashara zao zimeathirika au kufutiliwa mbali.

v).Watumishi waliokuwa wanaiibia serikali kwa mbinu zozote zile,na mbinu hizo sasa hazipo tena.

vi).Wauza madawa ya kulevya kwa sababu zilizo wazi.

vii).Watumishi wazembe na wasio na weledi.Hawa wanaona maisha ya kazi katika zama za Magufuli ni taabu sana.No wonder watumishi wengi wanatamani muda wao wa kustaafu ufike haraka.

viii)Watumishi waliohamishiwa Dodoma na kuacha miradi na majumba yao Dar es Salaam.

ix)Wafanyabiashara wa malori makubwa na mabasi,hasa wa ukanda wa Dar-Kigoma,Dar-Mwanza,Dar-Arusha,Tanga-Arusha.Hawa wanahofia biashara zao kuathirika baada ya ujio wa SGR na kuboreshwa kwa reli ya Dar-Arusha na Tanga-Arusha.Nadhani mnakumbuka incidence ambayo mmiliki wa mabasi ya kampuni fulani alishiriki kung'oa mataruma ya reli ya Moshi-Arusha.Episode ile ina-prove kwamba point hii ni kweli.

x)Ndugu wa makundi hayo hapo juu.

4.Wafuata upepo wasiokuwa na mawazo yao original,kwa vile hawana ufahamu wa kutosha,kwa hiyo wanadakia kila wazo hata baya,na hivyo kupotosha umma.

Naomba nimalizie kwa kusema tena,kwamba si rahisi kutaja makundi yote,kwa hiyo naomba kwa leo niishie hapo.
Huu upumbavu wako washirikishe wapumbavu wenzako wa Lumumba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Awamu hii sioni kundi wala mtu alienusurika kuumizwa au kuathiriwa na maamuzi ya serikali hata wewe muandishi unajua yote so stay cool wote tunachukia serikali sema hatuna uhuru wa kueleza yaliyo moyoni kwa sababu mbali mbali ikiwemo kulinda ugali,kifungo na kupewa ma kesi ya uhujumu uchumi.

Sent using Jamii Forums mobile app
86% ya wanaccm hawataki hata kumuona
 
Waungwana mmeamkaje?
Najua siku hizi dunia imekumbwa na kadhia ya wananchi kuwachukia viongozi wao. Sio tu Afrika bali hata nje ya Afrika tunaona kashkashi za RAIA kuwakataa viongozi wao wakuu hususani Marais.
Tukirudi Afrika Mimi naona Tanzania ndio inayoongoza kwasasa kumchukia Rais wao huku kila mmoja akiwa na sababu yake na wengine wakifuata upepo tu.
Magufuli unachukiwa sana na wananchi wako(sio viongozi wako). Viongozi wako huenda wanakupenda au wanakuchukia, Mimi ninachojua ni kwamba viongozi wako wateule wanakupenda, sasa kama ni wanafiki tu wanatetea ugali mimi halinihusu.
Na hao viongozi ndio washika mike kila siku kukutukuza that's why unadhani wanawasemea wananchi kiujumla na ukaamini kuwa unapendwa.
 
Unazungumzia wananchi gani wanaomchukia rais? Wewe andika ya kwako, achana na kampeni za kijinga kijinga. Kuna kundi linajiona limetengwa bila kutueleza wapi walitakiwa kuwa na sasa wametengwa.

Yaani hata wezi sasa wako mitandaoni, utadhani kura zinapigwa mitandaoni. Fanya kazi lipwa malipo halali. Achana na utapeli na wizi.
 
natamani kukuunga mkono ila kibaya umeandika usichokijua kwa kufatilia wanachosema jamiiforums. "behind the keyboard" ... kiuhalisia ukiingia mtaan kwa haraka zaidi nadhan magufuli ni rais anaekubalika zaid kwa hapa afrika mashariki na wananchi wake!.:

#mitazamo yako usiilete bila kufanya field case study yaan ukiamka kinachokujia kichwan tu unakiandika.
 
Msinge somba watu na malory kwenye mikutano yake
 
Rais Magufuli ni rais anayependwa mno na wananchi wake. Shida yenu mnafanya tathmini kwa kuangalia comments za bavicha humu jamiiforums. Nenda mitaani huko waliko wapiga kura.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
natamani kukuunga mkono ila kibaya umeandika usichokijua kwa kufatilia wanachosema jamiiforums. "behind the keyboard" ... kiuhalisia ukiingia mtaan kwa haraka zaidi nadhan magufuli ni rais anaekubalika zaid kwa hapa afrika mashariki na wananchi wake!.:

#mitazamo yako usiilete bila kufanya field case study yaan ukiamka kinachokujia kichwan tu unakiandika.
Una uhakika gani kuwa sijafanya research?
Au mapenzi yamekuzidi?
 
Msinge somba watu na malory kwenye mikutano yake
noope mkuu hyo si sababu ya msingi sana.. watanzania elite kama nyie ni wachache na ndo mnajua vitu vingi unlike wasio elite! ... na hawa wasio elite ndo hao idadi yao ni kubwa sana na ndo wakisikia magufuli wanashabikia tu, hvo kupeleka hoja ya mleta mada kutokua na mashiko ya kiuhalisia.

hata katika nyie wapo wanaomsapoti japo mguu nje mguu ndani. (hapa mm ni mmoja wao)
 
Waungwana mmeamkaje?
Najua siku hizi dunia imekumbwa na kadhia ya wananchi kuwachukia viongozi wao. Sio tu Afrika bali hata nje ya Afrika tunaona kashkashi za RAIA kuwakataa viongozi wao wakuu hususani Marais.
Tukirudi Afrika Mimi naona Tanzania ndio inayoongoza kwasasa kumchukia Rais wao huku kila mmoja akiwa na sababu yake na wengine wakifuata upepo tu.
Magufuli unachukiwa sana na wananchi wako(sio viongozi wako). Viongozi wako huenda wanakupenda au wanakuchukia, Mimi ninachojua ni kwamba viongozi wako wateule wanakupenda, sasa kama ni wanafiki tu wanatetea ugali mimi halinihusu.
Na hao viongozi ndio washika mike kila siku kukutukuza that's why unadhani wanawasemea wananchi kiujumla na ukaamini kuwa unapendwa.
Huo ndio ukweli. Ninekutana na wananch wa Ghana wakaniambia vipi habari za huko tanzania? Nikawambi habari ni mbaya. Na wao wanaijibu kuwa Rais maguduli alianzia vizuri lakini yunaona anakuwa dikteta kwa kukandamiza haki za kiraia na uhuru wa watu. Nilipigwa nabutwaa! Yaani habari mbaya za Magufuli waghana wanazijua kama vile wako ndani ishu za kubambikia watu kesi za uhujumu uchumi kwa kuwakomoa zote wanazijua. In fact anachukiwa na afrika nzima kwa sasa
 
Back
Top Bottom