1. Chawa bila kujali sekta ni janga lisilokuwa na tija.
2. Chawa huwa hawaoni wala kusikia dosari kuwahusu.
3. Kaulii hizi: "barabara ndefu haikosi kona" au "mwanamke mrembo hakosi kasoro," hazina maana yoyote kwao.
Makundi haya yanahusika:
a) Chawa wa mama: Hawa huwaambii kitu kumhusu bi mkubwa. Wao ni kusifu, kumshukuru na mapambio ya sifa kwa lolote.
b) Chawa wa Mwamba: Hawa nao huwaambii kitu kumhusu mwamba. Wao ni kusifu, kumshukuru na mapambio ya sifa kwa lolote. Mwamba hakosolewi. Kumkosoa mwamba, ni uhaini.
c) Chawa wa CCM: Hawa huwaambii kitu kuhusu CCM. Hakuna cha kukosoa. Yote ya CCM ni mema.
d) Chawa wa CHADEMA. Hawa huwaambii kitu kuhusu CHADEMA. Hiki chama hakikosolewi. Ukiwa na mawazo tofauti, ondoka.
e) Wafia Uislam: Hawa kwao dini ni uislam tu, tena ule wa kwao. Huwashangaa wengine wote na dini zao. Haiwaingii akilini iweje usiwe mwislam wa aina yao. Hawana uvumilivu na wengine. Mbingu na pepo wanayoijua ni ile yao tu, si ya wengine. Adui yao mkuu ni yeyote asiyekuwa mwislam na hasa mwisraeli.
f) Wafia Ukristo: Hawa wanaamini dini ni ukristo tu, tena ule wa kwao. Wanaamini Israeli ni taifa teule na kuwa tena si binadamu wa kawaida. Lolote afanyalo mwisraeli ni sawa tena dunia yote ilipaswa kuwasabiria. Hakuna ovu lolote dhidi ya Israel, na waarabu kwao, hawana haki yoyote.
g) Wajuaji: Hawa huamini kwenye lile tu wanaolijua wao. Wajuzi wa Kila kitu ni wao. Kwamba 'JF ina watu wa kada zote," haina maana yoyote kwao. Nafasi ya mafikara mapya hawana ila yale ya kwao tu. Kwamba "elimu ni bahari, elimu haina mwisho, tembea uone nk;" havina maana yoyote kwao.
4. Uchawa ni janga na chawa wenyewe ni wadudu wachafu.
5. Chawa ni chawa tu, bila kuupiga vita uchawa hakuna mabadiliko.
Tuungane kuupiga vita uchawa.