Unajichanganya sana, tuliza kichwa chako aisee, nikisoma hiyo namba moja ulivyoijibu naona kabisa unazidi kujimaliza mwenyewe, sasa kuna tofauti gani hapo kati ya #1 kutoa maoni na #2 mawazo binafsi?!
Kwani mtu akitoa maoni yake hapa huwa sio mawazo yake binafsi? una hakika huwa wanashawishiwa from outside? au wewe ni mpiga ramli humu JF! wewe ndie mwenye tatizo la kuingilia uhuru wa wengine kutoa maoni yao, uko gizani sana.
Hata nawe huwa una tabia ya kumuona Lissu malaika, hujijui tu; au ndio stori ya nyani hajioni...na wala hayupo aliyekuita chawa, mimi nipo nakutazama tu unavyojiinua kunyooshea kidole wengine.
Mara nyingi tu nawakosoa Chadema humu ndani, lakini kukosoa kwangu lazima kuwe na sababu sio kukurupuka tu, au Mbowe ikitokea kuna sababu ya msingi kumkosoa, namkosoa, lakini sio kumkosoa hovyo ilimradi nikufurahishe wewe!.
Sio kumkosoa kienyeji tu kama ufanyavyo na wenzako kumtaka aachie ngazi wakati aliwekwa pale kihalali, kwanini mnaingilia uhuru wa mtu kujiamulia mambo yake? huu upungufu wako ajabu huuoni sijui una upeo wa aina gani!.
Nakushauri tena, jifunze kuvumilia wenzio humu ndani, usijigeuze jaji wa mahakama ya jukwaa la siasa hapa JF. Narudia tena, hii assessment yako haina maana sababu hata nawe unaangukia kwenye moja ya hayo makundi uliyotaja pale juu, simply nawe ni chawa wa Lissu.
Kuwa makini sana, you are creating a seed of your own destruction kwa "ego" yako, nimemaliza ukitaka fuata ushauri ukitaka acha, its your choice kama ilivyo choice ya wengine humu ndani kuandika kile watakacho, muhimu utambue wewe sio mwalimu wetu hapa.
Ninachukua muda kukujibu kila hoja kwa maana ninaona unapoteza uelekeo, kujisahau na hata kuanza kutoa vitisho mbuzi. Ustaarabu ni kitu cha bure ndugu na hoja hupingwa kwa hoja.
'In red ni hoja zako. Kwenye kijani ni nukuu zako tokea maandishi yako ya awali kwenye uzi huu. Kwenye blue ni nukuu zangu tokea kwenye uzi huu unazoonekana kutaka kuzipotosha kwa makusudi."
Unajichanganya sana, tuliza kichwa chako aisee, nikisoma hiyo namba moja ulivyoijibu naona kabisa unazidi kujimaliza mwenyewe, sasa kuna tofauti gani hapo kati ya #1 kutoa maoni na #2 mawazo binafsi?!
1. Ulikiri mwenyewe kuwa andiko langu hili lilikugusa wewe binafsi.
Nitaonyesha nani baina yangu na wewe anaye jichanganya na bila shaka anayepaswa kutuliza kichwa chake aisee.
2. #1 na #2 kama nilivyoziandika,
ziko tofauti:
"1. Kutoa maoni mtu aonavyo (free style) hakuwezi kuwa u chawa; hiyo ni haki ya msingi ya kila mwenye akili timamu.
2. Uchawa ni kukosa mawazo binafsi (kwa kesi yako) mwamba ni malaika na Chadema ilishuka kutoka mbinguni; hakipo cha kukosoa jana, leo, wala kesho".
Ikikupendeza zipitie tena kujiridhisha.
Kwani mtu akitoa maoni yake hapa huwa sio mawazo yake binafsi? una hakika huwa wanashawishiwa from outside? au wewe ni mpiga ramli humu JF! wewe ndie mwenye tatizo la kuingilia uhuru wa wengine kutoa maoni yao, uko gizani sana.
3. Mada hii inahusu:
"Makundi saba ya chawa kindaki ndaki yanayotatiza mabadiliko"
Haya uliyoandika wewe hapa umeyaokota wapi ndugu?
4.Mimi si mpiga ramli wala sijui kama mko wapiga ramli humu. La ramli ni lako. Kunihukumu kuwa ndiye mwenye tatizo si haki kwani wewe si Mungu wala malaika. Kama ni maoni tu ila kutokujua namna ya kujieleza, kwanini hudhani wengine pia tunaweza kuwa tunaona wewe ndiye mwenye tatizo, na yote mengine yanayofuata kama unavyo ni tuhumu wewe?!
Hata nawe huwa una tabia ya kumuona Lissu malaika, hujijui tu; au ndio stori ya nyani hajioni...na wala hayupo aliyekuita chawa, mimi nipo nakutazama tu unavyojiinua kunyooshea kidole wengine.
5. Ujasiri wa kunisemea unaupata wapi ndugu? Wapi uliwahi kuyasoma hayo uliyoyaandika hapa? Hayo ya nyani kutokujiona .. kwa nini hudhani yanaweza kuwa yanakuhusu wewe zaidi? Mtu hawezi kuniita chawa kwa sababu nitaonyesha pasipokuwa na shaka kuwa mimi siyo.
Kwani chawa hawajijui ndugu? Zingatia #1 pale juu, wewe ulishakiri mwenyewe kuwa ni chawa kwa mujibu wa tafsiri ya kwenye mada.
Kuhusu wewe kuniangalia ... kama unavyosema, kwa nini hudhani wengine nao wanaweza kuwa hawanioni kama unavyoniona wewe na labda wala hawaoni popote ninapo hata jaribu kujiinua? Au kwani wewe ni nani ndugu?
"Au hata kwanini hudhani unavyodhani waniona wewe mimi nami nakuona wewe hivyo labda hata hovyo zaidi?"
Mara nyingi tu nawakosoa Chadema humu ndani, lakini kukosoa kwangu lazima kuwe na sababu sio kukurupuka tu, au Mbowe ikitokea kuna sababu ya msingi kumkosoa, namkosoa, lakini sio kumkosoa hovyo ilimradi nikufurahishe wewe!.
6. Hebu linganisha haya na kauli yako hii:
Duh!, sasa hapo umeliacha kundi gani ambalo lipo JF?!
Kwa huo mtazamo wako, naona umetumaliza wote kwa kutuita machawa!.
Kwamba kwa kesi yako::
a) Mbowe ni Malaika
b) chadema imeshushwa tokea mbinguni.
Kumbe hukosoa vipi au wapi basi, kwa kukiri kwako huko? Wewe huoni unavyojichanganya na bila shaka ni muda wako wa kutuliza kichwa sasa?
Sio kumkosoa kienyeji tu kama ufanyavyo na wenzako kumtaka aachie ngazi wakati aliwekwa pale kihalali, kwanini mnaingilia uhuru wa mtu kujiamulia mambo yake? huu upungufu wako ajabu huuoni sijui una upeo wa aina gani!.
7. Wapi nimemkosoa yeyote kienyeji? Au wapi nimemtaka waye yote aachie ngazi? Wenzangu ni nani unaojaribu kuninasibu nao? Mimi na nani tumeingilia uhuru wa nani wapi wa kujiamulia? Wapi hata nimeingilia uhuru wa mtu kuwa chawa au la?
8. Wewe si Mungu wala malaika kujaribu kunihukumu au kumhukumu awaye yote. Kusema, "huu upungufu wako .." ni kutoa hukumu. Kama labda ni maoni yako ila kutokana na umbumbu tu wa kujieleza, kwa nini hudhani wengine nao wanaweza kuwa hawaoni hivyo au labda nami kwa maoni yangu nakushangaa: "
huu upungufu wako ajabu huuoni au sijui una upeo wa aina gani!
Nakushauri tena, jifunze kuvumilia wenzio humu ndani, usijigeuze jaji wa mahakama ya jukwaa la siasa hapa JF. Narudia tena, hii assessment yako haina maana sababu hata nawe unaangukia kwenye moja ya hayo makundi uliyotaja pale juu, simply nawe ni chawa wa Lissu
9. Sina hakika kwa nini umeandika haya na wala hata kwa misingi ipi. Kama ni kutokana na mada huru hii:
"
Makundi saba ya chawa kindaki ndaki yanayotatiza mabadiliko"
mbona itakuwa ni jambo la kushangaza mno?!
Kuna jina la mtu ametajwa humu? Au wewe ni @lucas_mwashambwa au
MK254 watani zangu wa jadi niliowataja seat ya mbele pale? Au wewe ni wao? Au unajua kwanini tunatajana nao na mara ngapi kwenye nyuzi zilizopo zisizokuwa na idadi?
Wewe ni nani kujipa kazi au mamlaka za kushauri watu na hapa ati umenizukia kihasara hasara kutaka kunishauri miye? Kama wewe ni jamaa mwingine tu humu JF, mbona itakuwa ni maajabu ya Mussa? Au kumbe, wenda wazimu utakuwa ni upi, kama huu siyo?
kwanini hudhani mwenye kuhitaji kushauriwa na/au kuaswa kujifunza kuwavumilia wengine ni wewe? Wapi nimejifanya jaji, mahakama au hata kujaribu kutoa hukumu? Kweli nyani haoni kundl*ule.
"Mara ngapi nimekukumbusha kuacha kuhukumu kwamba wewe si Mungu wala malaika?"
10. Assessment yangu Ina maana sana Kwa maana kama wewe unaangukia mle kama ulivyokiri mwenyewe ninao uhakika simp humo na wengi wengine hawamo mle. walioko mle ni mzigo na hawana mchango wowote kwa taifa hili.
11. Mimi ni chawa wa Lissu? Upo nje ya mada ndugu. Kwenye list kuna makundi 7 ambapo Lissu hayumo. Kama ungependa kumjadili Lissu na chawa wake kama wapo, si uanzishe uzi, ukiwa na hoja tutachangia?
Angalizo, kwa vile wewe si msemaji wangu, kulikoni kunisemea mimi hali miye sijamsemea mtu? Nikadhani unapaswa kujishangaa zaidi ya sana ndugu?!
Kuwa makini sana, you are creating a seed of your own destruction kwa "ego" yako, nimemaliza ukitaka fuata ushauri ukitaka acha, its your choice kama ilivyo choice ya wengine humu ndani kuandika kile watakacho, muhimu utambue wewe sio mwalimu wetu hapa.
Usinitishe ndugu. Kila mtu ana destiny yake. Aliyechagua kuwa chawa, "haya" aliyechagua kuwa si chawa, "haya!" Ukichagua kuwa chawa hiyo ni juu yako; ukiamua kuwa si chawa ni juu yako. Kama ilivyo kwangu naamini.
Makasiriko na vitisho ya nini sasa? Si ujivunie uchaguzi wako? Kwani kuna aliyekuchagulia? Si ulichagua mwenyewe?
Nani amekwambia yeye ni mwalimu wa mtu au anataka kuwa mwalimu au anahitaji hata wanafunzi?
Ninarudia, usinitishe ndugu!
Bure kabisa!