Makundi saba ya chawa kindaki ndaki yanayotatiza mabadiliko

1. Chawa bila kujali sekta ni janga lisilokuwa na tija.

2. Chawa huwa hawaoni wala kusikia dosari kuwahusu.

3. Kaulii hizi: "barabara ndefu haikosi kona" au "mwanamke mrembo hakosi kasoro," hazina maana yoyote kwao.

Makundi haya yanahusika:

a) Chawa wa mama: Hawa huwaambii kitu kumhusu bi mkubwa. Wao ni kusifu, kumshukuru na mapambio ya sifa kwa lolote.

b) Chawa wa Mwamba: Hawa nao huwaambii kitu kumhusu mwamba. Wao ni kusifu, kumshukuru na mapambio ya sifa kwa lolote. Mwamba hakosolewi. Kumkosoa mwamba, ni uhaini.

c) Chawa wa CCM: Hawa huwaambii kitu kuhusu CCM. Hakuna cha kukosoa. Yote ya CCM ni mema.

d) Chawa wa CHADEMA. Hawa huwaambii kitu kuhusu CHADEMA. Hiki chama hakikosolewi. Ukiwa na mawazo tofauti, ondoka.

e) Wafia Uislam: Hawa kwao dini ni uislam tu, tena ule wa kwao. Huwashangaa wengine wote na dini zao. Haiwaingii akilini iweje usiwe mwislam wa aina yao. Hawana uvumilivu na wengine. Mbingu na pepo wanayoijua ni ile yao tu, si ya wengine. Adui yao mkuu ni yeyote asiyekuwa mwislam na hasa mwisraeli.

f) Wafia Ukristo: Hawa wanaamini dini ni ukristo tu, tena ule wa kwao. Wanaamini Israeli ni taifa teule na kuwa tena si binadamu wa kawaida. Lolote afanyalo mwisraeli ni sawa tena dunia yote ilipaswa kuwasabiria. Hakuna ovu lolote dhidi ya Israel, na waarabu kwao, hawana haki yoyote.

g) Wajuaji: Hawa huamini kwenye lile tu wanaolijua wao. Wajuzi wa Kila kitu ni wao. Kwamba 'JF ina watu wa kada zote," haina maana yoyote kwao. Nafasi ya mafikara mapya hawana ila yale ya kwao tu. Kwamba "elimu ni bahari, elimu haina mwisho, tembea uone nk;" havina maana yoyote kwao.

4. Uchawa ni janga na chawa wenyewe ni wadudu wachafu.

View attachment 2951213

5. Chawa ni chawa tu, bila kuupiga vita uchawa hakuna mabadiliko.

Tuungane kuupiga vita uchawa.
Njaa ikiuma, na fulsa za, kupata ugari zikawa chache,hapo vijana wenye roho nyepesi lazima wawe machawa!
 
Ninachukua muda kukujibu kila hoja kwa maana ninaona unapoteza uelekeo, kujisahau na hata kuanza kutoa vitisho mbuzi. Ustaarabu ni kitu cha bure ndugu na hoja hupingwa kwa hoja.

'In red ni hoja zako. Kwenye kijani ni nukuu zako tokea maandishi yako ya awali kwenye uzi huu. Kwenye blue ni nukuu zangu tokea kwenye uzi huu unazoonekana kutaka kuzipotosha kwa makusudi."

Unajichanganya sana, tuliza kichwa chako aisee, nikisoma hiyo namba moja ulivyoijibu naona kabisa unazidi kujimaliza mwenyewe, sasa kuna tofauti gani hapo kati ya #1 kutoa maoni na #2 mawazo binafsi?!

1. Ulikiri mwenyewe kuwa andiko langu hili lilikugusa wewe binafsi.

Nitaonyesha nani baina yangu na wewe anaye jichanganya na bila shaka anayepaswa kutuliza kichwa chake aisee.

2. #1 na #2 kama nilivyoziandika, ziko tofauti:

"1. Kutoa maoni mtu aonavyo (free style) hakuwezi kuwa u chawa; hiyo ni haki ya msingi ya kila mwenye akili timamu.

2. Uchawa ni kukosa mawazo binafsi (kwa kesi yako) mwamba ni malaika na Chadema ilishuka kutoka mbinguni; hakipo cha kukosoa jana, leo, wala kesho"
.

Ikikupendeza zipitie tena kujiridhisha.

Kwani mtu akitoa maoni yake hapa huwa sio mawazo yake binafsi? una hakika huwa wanashawishiwa from outside? au wewe ni mpiga ramli humu JF! wewe ndie mwenye tatizo la kuingilia uhuru wa wengine kutoa maoni yao, uko gizani sana.

3. Mada hii inahusu:

"Makundi saba ya chawa kindaki ndaki yanayotatiza mabadiliko"

Haya uliyoandika wewe hapa umeyaokota wapi ndugu?

4.Mimi si mpiga ramli wala sijui kama mko wapiga ramli humu. La ramli ni lako. Kunihukumu kuwa ndiye mwenye tatizo si haki kwani wewe si Mungu wala malaika. Kama ni maoni tu ila kutokujua namna ya kujieleza, kwanini hudhani wengine pia tunaweza kuwa tunaona wewe ndiye mwenye tatizo, na yote mengine yanayofuata kama unavyo ni tuhumu wewe?!

Hata nawe huwa una tabia ya kumuona Lissu malaika, hujijui tu; au ndio stori ya nyani hajioni...na wala hayupo aliyekuita chawa, mimi nipo nakutazama tu unavyojiinua kunyooshea kidole wengine.

5. Ujasiri wa kunisemea unaupata wapi ndugu? Wapi uliwahi kuyasoma hayo uliyoyaandika hapa? Hayo ya nyani kutokujiona .. kwa nini hudhani yanaweza kuwa yanakuhusu wewe zaidi? Mtu hawezi kuniita chawa kwa sababu nitaonyesha pasipokuwa na shaka kuwa mimi siyo.

Kwani chawa hawajijui ndugu? Zingatia #1 pale juu, wewe ulishakiri mwenyewe kuwa ni chawa kwa mujibu wa tafsiri ya kwenye mada.

Kuhusu wewe kuniangalia ... kama unavyosema, kwa nini hudhani wengine nao wanaweza kuwa hawanioni kama unavyoniona wewe na labda wala hawaoni popote ninapo hata jaribu kujiinua? Au kwani wewe ni nani ndugu?

"Au hata kwanini hudhani unavyodhani waniona wewe mimi nami nakuona wewe hivyo labda hata hovyo zaidi?"

Mara nyingi tu nawakosoa Chadema humu ndani, lakini kukosoa kwangu lazima kuwe na sababu sio kukurupuka tu, au Mbowe ikitokea kuna sababu ya msingi kumkosoa, namkosoa, lakini sio kumkosoa hovyo ilimradi nikufurahishe wewe!.

6. Hebu linganisha haya na kauli yako hii:

Duh!, sasa hapo umeliacha kundi gani ambalo lipo JF?!

Kwa huo mtazamo wako, naona umetumaliza wote kwa kutuita machawa!.

Kwamba kwa kesi yako::
a) Mbowe ni Malaika

b) chadema imeshushwa tokea mbinguni.

Kumbe hukosoa vipi au wapi basi, kwa kukiri kwako huko? Wewe huoni unavyojichanganya na bila shaka ni muda wako wa kutuliza kichwa sasa?

Sio kumkosoa kienyeji tu kama ufanyavyo na wenzako kumtaka aachie ngazi wakati aliwekwa pale kihalali, kwanini mnaingilia uhuru wa mtu kujiamulia mambo yake? huu upungufu wako ajabu huuoni sijui una upeo wa aina gani!.

7. Wapi nimemkosoa yeyote kienyeji? Au wapi nimemtaka waye yote aachie ngazi? Wenzangu ni nani unaojaribu kuninasibu nao? Mimi na nani tumeingilia uhuru wa nani wapi wa kujiamulia? Wapi hata nimeingilia uhuru wa mtu kuwa chawa au la?

8. Wewe si Mungu wala malaika kujaribu kunihukumu au kumhukumu awaye yote. Kusema, "huu upungufu wako .." ni kutoa hukumu. Kama labda ni maoni yako ila kutokana na umbumbu tu wa kujieleza, kwa nini hudhani wengine nao wanaweza kuwa hawaoni hivyo au labda nami kwa maoni yangu nakushangaa: "huu upungufu wako ajabu huuoni au sijui una upeo wa aina gani!

Nakushauri tena, jifunze kuvumilia wenzio humu ndani, usijigeuze jaji wa mahakama ya jukwaa la siasa hapa JF. Narudia tena, hii assessment yako haina maana sababu hata nawe unaangukia kwenye moja ya hayo makundi uliyotaja pale juu, simply nawe ni chawa wa Lissu

9. Sina hakika kwa nini umeandika haya na wala hata kwa misingi ipi. Kama ni kutokana na mada huru hii:

mbona itakuwa ni jambo la kushangaza mno?!

Kuna jina la mtu ametajwa humu? Au wewe ni @lucas_mwashambwa au MK254 watani zangu wa jadi niliowataja seat ya mbele pale? Au wewe ni wao? Au unajua kwanini tunatajana nao na mara ngapi kwenye nyuzi zilizopo zisizokuwa na idadi?

Wewe ni nani kujipa kazi au mamlaka za kushauri watu na hapa ati umenizukia kihasara hasara kutaka kunishauri miye? Kama wewe ni jamaa mwingine tu humu JF, mbona itakuwa ni maajabu ya Mussa? Au kumbe, wenda wazimu utakuwa ni upi, kama huu siyo?

kwanini hudhani mwenye kuhitaji kushauriwa na/au kuaswa kujifunza kuwavumilia wengine ni wewe? Wapi nimejifanya jaji, mahakama au hata kujaribu kutoa hukumu? Kweli nyani haoni kundl*ule.

"Mara ngapi nimekukumbusha kuacha kuhukumu kwamba wewe si Mungu wala malaika?"

10. Assessment yangu Ina maana sana Kwa maana kama wewe unaangukia mle kama ulivyokiri mwenyewe ninao uhakika simp humo na wengi wengine hawamo mle. walioko mle ni mzigo na hawana mchango wowote kwa taifa hili.

11. Mimi ni chawa wa Lissu? Upo nje ya mada ndugu. Kwenye list kuna makundi 7 ambapo Lissu hayumo. Kama ungependa kumjadili Lissu na chawa wake kama wapo, si uanzishe uzi, ukiwa na hoja tutachangia?

Angalizo, kwa vile wewe si msemaji wangu, kulikoni kunisemea mimi hali miye sijamsemea mtu? Nikadhani unapaswa kujishangaa zaidi ya sana ndugu?!

Kuwa makini sana, you are creating a seed of your own destruction kwa "ego" yako, nimemaliza ukitaka fuata ushauri ukitaka acha, its your choice kama ilivyo choice ya wengine humu ndani kuandika kile watakacho, muhimu utambue wewe sio mwalimu wetu hapa.

Usinitishe ndugu. Kila mtu ana destiny yake. Aliyechagua kuwa chawa, "haya" aliyechagua kuwa si chawa, "haya!" Ukichagua kuwa chawa hiyo ni juu yako; ukiamua kuwa si chawa ni juu yako. Kama ilivyo kwangu naamini.

Makasiriko na vitisho ya nini sasa? Si ujivunie uchaguzi wako? Kwani kuna aliyekuchagulia? Si ulichagua mwenyewe?

Nani amekwambia yeye ni mwalimu wa mtu au anataka kuwa mwalimu au anahitaji hata wanafunzi?

Ninarudia, usinitishe ndugu!

Bure kabisa!
Nakushangaa umechukua muda mrefu sana kujibu, wakati jibu lako tayari nilishalifahamu kutokana na tabia na hulka yako!.

Una maneno mengi yasiyokuwa na maana, sasa naona unadai nakutisha! hujui hata tofauti ya ushauri na vitisho!.

• Tisho kwa kiingereza wanaita threat, meaning; statement of an intention to inflict pain, injury, damage, or other hostile action on someone... { kama hukubaliani na hii defination tazama ya kwako ujifunze}.

Kuna vitu obvious sana ungetakiwa ujiulize bahati mbaya huna upeo huo, simply hii mada yako sio jumuishi imekosa sifa zote, na assessment yako ni wrong sababu hata nawe unaangukia humo vile tu hujijui.

Endelea na wengine.
 
Mimi naamini kwa dhati kabisa kwamba adui nambari wani wa taifa hili ni CCM.

Naamini kwa dhati kabisa kwamba kama taifa, zimwi lililotufikisha hapa tulipo ni CCM.

Naamini kwa dhati kabisa CCM ni kambi ya walafi na waovu wasiolitakia mema taifa hili.

Fikiria vyama viwili vinavyounda serikali vinajiunga na kuwa chama kimoja lakini serikali zinabaki mbili. Huu nauita uendawazimU

Naamini kwa dhati kabisa kwamba njia pekee ya kujikwamua ni kwa kuipiga vita CCM..

Kama kwa imani yangu hii utaniita chawa najivuna kuwa chawa, si wa chama, si wa mtu bali wa Jamhuri ya Muungano Tanzania.
 
Nimeipenda hiyo paragraph yako ya mwisho. Inaendana na my first comment kwenye huu uzi.
 
Nakushangaa umechukua muda mrefu sana kujibu, wakati jibu lako tayari nilishalifahamu kutokana na tabia na hulka yako!.

Una maneno mengi yasiyokuwa na maana, sasa naona unadai nakutisha! hujui hata tofauti ya ushauri na vitisho!.

Kuna vitu obvious sana ungetakiwa ujiulize bahati mbaya huna upeo huo, simply hii mada yako sio jumuishi imekosa sifa zote, na assessment yako ni wrong sababu hata nawe unaangukia humo vile tu hujijui.

Endelea na wengine..

I) Bila shaka unadhani kukuvumilia kwangu kote ni ujinga wangu. Kwamba nimekuwa nikikuasa muda wote kujikita kwenye kutoa maoni kama maoni, na kuacha kunishambulia au kunihukumu; ila bado kama zuzu tu, umependa kuendelea hivyo unabated.

II) Kwa sababu hiyo, unaonekana huelewi wala kuonekana kutaka kuelewa; bila shaka huwezi kuelewa.

Kwamba ni ile wanasema "mbwa mzee hawezi kujifunza jina jipya!"

Nilidhani nikupuuze lakini kulikoni nikuache mjinga ukijidhania ndiwe mwenye busara? Kwa maana hii sasa tambua ninakuondolea uvivu:

Kutokea hapa sasa, ninakupa pamoja na tathmini yako halisi kama wewe, ukapate kujitambua, ukipenda.

Wito thabiti wa siku zote uko wazi: 'rudini shule mkasome, elimu haina mwisho na elimu ni uhuru!'

Umeandika leo:

1. Nakushangaa umechukua muda mrefu sana kujibu, wakati jibu lako tayari nilishalifahamu kutokana na tabia na hulka yako!.

Hapa unaonyesha wewe ni mbumbu mwenye ujuaji. Ujuaji Kwa maana yake kamili kama ilivyoelezwa kwenye mada. Hii ni kwa sababu zifuatazo:

Jana niliandika kwenye aya ya kwanza kabisa:

Ninachukua muda kukujibu kila hoja kwa maana ninaona unapoteza uelekeo, kujisahau na hata kuanza kutoa vitisho mbuzi. Ustaarabu ni kitu cha bure ndugu na hoja hupingwa kwa hoja.

i) Linganisha na hoja yako hiyo ya leo. Kisha ujiambie kushangaa kwako ni kwa kijinga kwani uliambiwa kwanini litakuwa andiko refu na litakuwa linafanya nini hata kabla ya habari yenyewe.

ii) "Kwamba ulijua majibu yatakuwa je, kuwa unanijua hulka na tabia", huo ni "ujuaji" kamili na sawia kama ulivyoelezwa kwenye mada:

g) Wajuaji: Hawa huamini kwenye lile tu wanaolijua wao. Wajuzi wa Kila kitu ni wao. Kwamba 'JF ina watu wa kada zote," haina maana yoyote kwao. Nafasi ya mafikara mapya hawana ila yale ya kwao tu. Kwamba "elimu ni bahari, elimu haina mwisho, tembea uone nk;" havina maana yoyote kwao.

iii) Hapa kwenye ujuaji zingatia wewe siyo Mungu, Shetani, Malaika, Jini, wala nabii; wala si mke wangu unijue mimi tabia au hulka zangu, ndugu.

2. Una maneno mengi yasiyokuwa na maana, sasa naona unadai nakutisha! hujui hata tofauti ya ushauri na vitisho!.

a) Aya yangu ya kwanza ilisomeka wazi:

i) Linganisha na ulichoandika hapo kuutambua tena umbumbu na ujuaji wako:

(a) sikuandika maneno yàngu bali hata nilikutaarifu mapema kuwa yaja majibu kwa hoja zako zote. Haina shaka mbumbu mjuaji hawezi kutofautisha "majibu" na "maneno;" ndiyo sababu labda ungehitaji hata kamusi kutafuta maana.

(b) Yaliyomo mle ni majibu ya hoja zako, moja moja bila kuachwa moja na bila nyongeza.

(c) Rejea kuisoma aya yako hii;

Kuwa makini sana, you are creating a seed of your own destruction kwa "ego" yako, nimemaliza ukitaka fuata ushauri ukitaka acha, its your choice kama ilivyo choice ya wengine humu ndani kuandika kile watakacho, muhimu utambue wewe sio mwalim wetu hapa.

Fumbo mfumbie mjinga ndugu:

(d) hiki ni kitisho mbuzi kama nilivyokiita kwa usahihi wake.

(e) Zingatia huna maadili (moral authority) yoyote wewe kama mbumbu mjuaji kumshauri yeyote mwenye kujua maana. Huo ushauri wako kama wauona ni mzuri si ujishauri mwenyewe ili ung'are zaidi?

(f) Hapa pigia mstari pia kichwani mwako: "ushauri wako siuhitaji jana, leo, wala kesho."

3. Kuna vitu obvious sana ungetakiwa ujiulize bahati mbaya huna upeo huo, simply hii mada yako sio jumuishi imekosa sifa zote, na assessment yako ni wrong sababu hata nawe unaangukia humo vile tu hujijui.

i) Mbumbu mjuaji kazini kwenye ubora wako:

a) Ni kawaida kwa mjuaji kujidhania anajua kila kitu tena kudhani vitu ni obvious sana na kuwashangaa wengine. Mjuaji hudhani hivyo vina apply kwa wengine, lakini si yeye.

(b) Ndugu, wewe ni mbumbu mjuaji usiyetambua uliyoyaandika yana kuhusu sana. Vipi nyani wewe kuona kun"u lako? Hapo ndipo asili haswa ya 3(g); kundi pendwa, kitinda mimba #7 lilipo, chawa specia,l na self made kama katika ubora wako.

(c) kwamba jinga juaji wewe usiyejitambua utakuwa na upeo upi? Kwa hakika wala si bahati mbaya kuwa hujitambui. Ujitambue vipi wakati ni wazi hata elimu yenyewe bila shaka ndiyo hivyo tena kama unavyojitanabaisha mwenyewe na arguments zako uchwara hizi?

(c) kuhusiana na mada yangu wewe huna credentials za kuifanyia assessment yoyote ndugu. Kwa hakika ni sawa na mwanafunzi wa darasa kwanza kutaka kuifanyia assessment paper ya daktari bingwa wa upasuaji ubongo kwenye maeneo yake ya kujidai.

Acheni kujipa majukumu na umuhimu msio kuwa nao!

(d) Hapo namba (c) nisiache kukupa angalizo: kujitahidi kutokusubiri kuonyeshwa na wengine kuijua nafasi yako ilipo. Ni aibu!

"Kumbuka yule aliyekwenda kukaa kwenye high table, kumbe hapaswi kuwa huko, bila kumsahau aliyekaa kwa walalahoi, kumbe ni wa high table."

(e) busara ni kitu cha bure, kulikoni kuwa wa mwanzo, kuanzisha dharau dhidi ya mtu usiye mjua?!

Bila kuacha kukwambia hiki ulichoandika hapa chini ni kuonyesha upuuzi mwingine zaidi tu:

4. Endelea na wengine.

Zingatia miye siwajibiki kwako!
 
Mimi naamini kwa dhati kabisa kwamba adui nambari wani wa taifa hili ni CCM.

Naamini kwa dhati kabisa kwamba kama taifa, zimwi lililotufikisha hapa tulipo ni CCM.

Naamini kwa dhati kabisa CCM ni kambi ya walafi na waovu wasiolitakia mema taifa hili.

Fikiria vyama viwili vinavyounda serikali vinajiunga na kuwa chama kimoja lakini serikali zinabaki mbili. Huu nauita uendawazimU

Naamini kwa dhati kabisa kwamba njia pekee ya kujikwamua ni kwa kuipiga vita CCM..

Kama kwa imani yangu hii utaniita chawa najivuna kuwa chawa, si wa chama, si wa mtu bali wa Jamhuri ya Muungano Tanzania.

Mkuu nichukue muda kidogo kulijibu kikamilifu bandiko lako lote lenye mlolongo wa sentensi zilizo za kweli; zingine zikiwa "ndani na zingine nje kabisa" ya mada.

1. Mimi naamini kwa dhati kabisa kwamba adui nambari wani wa taifa hili ni CCM.

Naamini kwa dhati kabisa kwamba kama taifa, zimwi lililotufikisha hapa tulipo ni CCM.

Naamini kwa dhati kabisa CCM ni kambi ya walafi na waovu wasiolitakia mema taifa hili.

Aya zako tatu hizo hapo juu, zote ni kweli na kweli tupu; ila katika context ya mada, nadhani utakubaliana nami hapa kuwa:

a) Chawa wa mama watapinga,
c) Chawa wa CCM watapinga,
g) Wajuaji nao, kama wa a) na c) hapo juu wanaweza kukushangaza zaidi, kuwa eti kumbe mjinga ni wewe na werevu ni wao.

Kwa aya zako tatu hizo ndani ya mada tuko pamoja:

i) Tusio na adui wa kudumu tunasimama na Dkt. Slaa

ii) Tutambuane: Wenye ujasiri au sababu za kuikabili CCM

iii) Lwaitama: Kwenye maslahi ya nchi, adui yetu ni CCM

Zingatia mauudhui ya mada:

"Makundi saba ya chawa kindaki ndaki yanayotatiza mabadiliko"​

2. Fikiria vyama viwili vinavyounda serikali vinajiunga na kuwa chama kimoja lakini serikali zinabaki mbili. Huu nauita uendawazimU

Naamini kwa dhati kabisa kwamba njia pekee ya kujikwamua ni kwa kuipiga vita CCM..

Ulichoandika hapa ni kweli na kweli tupu ila nje kabisa ya mada. Hata hivyo nijitahidi kukuburutia ndani kadri ya uwezo wangu.

Uwendakuzimu unaouongelea chimbuko lake ni la muda mrefu likiwagharimu wengi tangia 1964; Kina Karume, Jumbe, Maalim na wengi tukiwamo kina sisi leo; sote tu wahanga.

"Makundi saba ya chawa kindaki ndaki yanayotatiza mabadiliko"​

Mabadiliko tunayotaka ni yenye kuuhusu uwendakuzimu huu pia wenye kuanzia 1964 linalozaa kero yako hii; ambayo kwa hakika ni kero ya wengi. Ni wito wangu kuwa, tushirikiane ikiwamo dhidi ya wanaoyatatiza mabadiliko haya.

Kuhusu CCM kama pale awali tuko pamoja:

i) Tusio na adui wa kudumu tunasimama na Dkt. Slaa

ii) Tutambuane: Wenye ujasiri au sababu za kuikabili CCM

iii) Lwaitama: Kwenye maslahi ya nchi, adui yetu ni CCM

3. Kama kwa imani yangu hii utaniita chawa najivuna kuwa chawa, si wa chama, si wa mtu bali wa Jamhuri ya Muungano Tanzania.

Hapa ndipo uliponiacha hoi kiasi nakuwekea hapa chini kama yalivyo kwenye mada:

Makundi haya yanahusika:

a) Chawa wa mama: Hawa huwaambii kitu kumhusu bi mkubwa. Wao ni kusifu, kumshukuru na mapambio ya sifa kwa lolote.

b) Chawa wa Mwamba: Hawa nao huwaambii kitu kumhusu mwamba. Wao ni kusifu, kumshukuru na mapambio ya sifa kwa lolote. Mwamba hakosolewi. Kumkosoa mwamba, ni uhaini.

c) Chawa wa CCM: Hawa huwaambii kitu kuhusu CCM. Hakuna cha kukosoa. Yote ya CCM ni mema.

d) Chawa wa CHADEMA. Hawa huwaambii kitu kuhusu CHADEMA. Hiki chama hakikosolewi. Ukiwa na mawazo tofauti, ondoka.

e) Wafia Uislam: Hawa kwao dini ni uislam tu, tena ule wa kwao. Huwashangaa wengine wote na dini zao. Haiwaingii akilini iweje usiwe mwislam wa aina yao. Hawana uvumilivu na wengine. Mbingu na pepo wanayoijua ni ile yao tu, si ya wengine. Adui yao mkuu ni yeyote asiyekuwa mwislam na hasa mwisraeli.

f) Wafia Ukristo: Hawa wanaamini dini ni ukristo tu, tena ule wa kwao. Wanaamini Israeli ni taifa teule na kuwa tena si binadamu wa kawaida. Lolote afanyalo mwisraeli ni sawa tena dunia yote ilipaswa kuwasabiria. Hakuna ovu lolote dhidi ya Israel, na waarabu kwao, hawana haki yoyote.

g) Wajuaji: Hawa huamini kwenye lile tu wanaolijua wao. Wajuzi wa Kila kitu ni wao. Kwamba 'JF ina watu wa kada zote," haina maana yoyote kwao. Nafasi ya mafikara mapya hawana ila yale ya kwao tu. Kwamba "elimu ni bahari, elimu haina mwisho, tembea uone nk;" havina maana yoyote kwao
.

Makundi yaliyotajwa yako saba. Hapo la Imani yako kama ya ilivyo kwa la Imani yangu na za wengine zisizokuwa hizo hazimo humo!

Haipo shaka kuwa "hatumo humo, hayo makundi yana wenyewe na hivyo wewe kuitwa chawa haiwezekani!

Hoja yako hapa ni sawa na kushuku kama paka anaweza kuitwa mbuzi. Jibu la langu Kwa Hilo ni la wazi (swift) ni kuwa:

"Haiwezekani labda ajiite hivyo mwenyewe!"
 
Njaa ikiuma, na fulsa za, kupata ugari zikawa chache,hapo vijana wenye roho nyepesi lazima wawe machawa!

Hao wenye njaa Nyerere aliwaona:

IMG_20240402_054957.jpg
 
I) Bila shaka unadhani kukuvumilia kwangu kote ni ujinga wangu. Kwamba nimekuwa nikikuasa muda wote kujikita kwenye kutoa maoni kama maoni, na kuacha kunishambulia au kunihukumu; ila bado kama zuzu tu, umependa kuendelea hivyo unabated.

II) Kwa sababu hiyo, unaonekana huelewi wala kuonekana kutaka kuelewa; bila shaka huwezi kuelewa.

Kwamba ni ile wanasema "mbwa mzee hawezi kujifunza jina jipya!"

Nilidhani nikupuuze lakini kulikoni nikuache mjinga ukijidhania ndiwe mwenye busara? Kwa maana hii sasa tambua ninakuondolea uvivu:

Kutokea hapa sasa, ninakupa pamoja na tathmini yako halisi kama wewe, ukapate kujitambua, ukipenda.

Wito thabiti wa siku zote uko wazi: 'rudini shule mkasome, elimu haina mwisho na elimu ni uhuru!'

Umeandika leo:

1. Nakushangaa umechukua muda mrefu sana kujibu, wakati jibu lako tayari nilishalifahamu kutokana na tabia na hulka yako!.

Hapa unaonyesha wewe ni mbumbu mwenye ujuaji. Ujuaji Kwa maana yake kamili kama ilivyoelezwa kwenye mada. Hii ni kwa sababu zifuatazo:

Jana niliandika kwenye aya ya kwanza kabisa:

Ninachukua muda kukujibu kila hoja kwa maana ninaona unapoteza uelekeo, kujisahau na hata kuanza kutoa vitisho mbuzi. Ustaarabu ni kitu cha bure ndugu na hoja hupingwa kwa hoja.

i) Linganisha na hoja yako hiyo ya leo. Kisha ujiambie kushangaa kwako ni kwa kijinga kwani uliambiwa kwanini litakuwa andiko refu na litakuwa linafanya nini hata kabla ya habari yenyewe.

ii) "Kwamba ulijua majibu yatakuwa je, kuwa unanijua hulka na tabia", huo ni "ujuaji" kamili na sawia kama ulivyoelezwa kwenye mada:

g) Wajuaji: Hawa huamini kwenye lile tu wanaolijua wao. Wajuzi wa Kila kitu ni wao. Kwamba 'JF ina watu wa kada zote," haina maana yoyote kwao. Nafasi ya mafikara mapya hawana ila yale ya kwao tu. Kwamba "elimu ni bahari, elimu haina mwisho, tembea uone nk;" havina maana yoyote kwao.

iii) Hapa kwenye ujuaji zingatia wewe siyo Mungu, Shetani, Malaika, Jini, wala nabii; wala si mke wangu unijue mimi tabia au hulka zangu, ndugu.

2. Una maneno mengi yasiyokuwa na maana, sasa naona unadai nakutisha! hujui hata tofauti ya ushauri na vitisho!.

a) Aya yangu ya kwanza ilisomeka wazi:

Ninachukua muda kukujibu kila hoja kwa maana ninaona unapoteza uelekeo, kujisahau na hata kuanza kutoa vitisho mbuzi. Ustaarabu ni kitu cha bure ndugu na hoja hupingwa kwa hoja.

i) Linganisha na ulichoandika hapo kuutambua tena umbumbu na ujuaji wako:

(a) sikuandika maneno yàngu bali hata nilikutaarifu mapema kuwa yaja majibu kwa hoja zako zote. Haina shaka mbumbu mjuaji hawezi kutofautisha "majibu" na "maneno;" ndiyo sababu labda ungehitaji hata kamusi kutafuta maana.

(b) Yaliyomo mle ni majibu ya hoja zako, moja moja bila kuachwa moja na bila nyongeza.

(c) Rejea kuisoma aya yako hii;

Kuwa makini sana, you are creating a seed of your own destruction kwa "ego" yako, nimemaliza ukitaka fuata ushauri ukitaka acha, its your choice kama ilivyo choice ya wengine humu ndani kuandika kile watakacho, muhimu utambue wewe sio mwalim wetu hapa.

Fumbo mfumbie mjinga ndugu:

(d) hiki ni kitisho mbuzi kama nilivyokiita kwa usahihi wake.

(e) Zingatia huna maadili (moral authority) wewe kama mbumbu mjuaji kumshauri mtu yeyote ndugu mwenye kujua maana. Huo ushauri wako kama wauona ni mzuri si ujishauri mwenyewe ili ung'are zaidi?

(f) Hapa pigia mstari pia kichwani mwako: "ushauri wako siuhitaji jana, leo, wala kesho."

3. Kuna vitu obvious sana ungetakiwa ujiulize bahati mbaya huna upeo huo, simply hii mada yako sio jumuishi imekosa sifa zote, na assessment yako ni wrong sababu hata nawe unaangukia humo vile tu hujijui.

i) Mbumbu mjuaji kazini kwenye ubora wako:

a) Ni kawaida kwa mjuaji kujidhania anajua kila kitu tena kudhani vitu ni obvious sana na kuwashangaa wengine. Mjuaji hudhani hivyo vina apply kwa wengine, lakini si yeye.

(b) Ndugu, wewe ni mbumbu mjuaji usiyetambua uliyoyaandika yana kuhusu sana. Vipi nyani wewe kuona kun"u lako? Hapo ndipo asili haswa ya 3(g); kundi pendwa, kitinda mimba #7 lilipo, chawa specia,l na self made kama ilivyo kwenye mada, ilipo.

(c) kwamba jinga juaji wewe usiyejitambua utakuwa na upeo upi? Kwa hakika wala si bahati mbaya kuwa hujitambui. Ujitambue vipi wakati ni wazi hata elimu yenyewe bila shaka ndiyo hivyo tena kama unavyojitanabaisha mwenyewe na arguments zako uchwara?

(c) kuhusiana na mada yangu wewe huna credentials za kuifanyia assessment yoyote ndugu. Kwa hakika ni sawa na mwanafunzi wa darasa kwanza kutaka kuifanyia assessment paper ya daktari bingwa wa upasuaji kwenye maeneo yake ya kujidai.

Acheni kujipa majukumu na umuhimu msio kuwa nao

(d) Hapo namba (c) nisiache kukupa Angalizo, kujitahidi kutokusubiri kuonyeshwa na wengine kuijua nafasi yako ilipo. Ni aibu!

"Kumbuka yule aliyekwenda kukaa kwenye high table, kumbe hapaswi kuwa huko, bila kumsahau aliyekaa kwa walalahoi, kumbe ni wa high table."

(e) busara ni kitu cha bure, kulikoni kuwa wa mwanzo, kuanzisha dharau dhidi ya mtu usiye mjua?!

Bila kuacha kukwambia hiki ulichoandika hapa chini ni kuonyesha ni upuuzi mwingine zaidi tu:

4. Endelea na wengine.

Zingatia miye siwajibiki kwako!
Bado unaendelea kujaza maneno mengi yasiyo na maana, kitakuwa ndio kipaji chako naona.

Naamini umejifunza kutofautisha vitisho na ushauri, huo ujinga wako mwingine wa kuokoteza majibu yangu ya jana kisha kuyaleta kwenye majibu yangu kwako ya leo, wala usijue nakujibu kulingana na vile unavyokuja, naona nikuache nao.

Unachekesha sana unapodai natoka nje ya mada wakati nimekupa mpaka majibu ya ujinga wako wa leo toka google. Unaonekana mswahili usiyejielewa acha kujiona mwalimu hapa ndani, nimeshakuonesha nawe ni mjinga tu.

Usinune mimi ndio nimemaliza, next time unaweza kuja na mada inayoeleweka tukaenda sawa, sio hii ya kipuuzi tu, ujue na kuvumilia watu na misimamo yao hapa ndani, una maneno mengi bila reference yoyote umekuwa kama mwalimu wa ngonjera.
 
Bado unaendelea kujaza maneno mengi yasiyo na maana, kitakuwa ndio kipaji chako naona.

Naamini umejifunza kutofautisha vitisho na ushauri, huo ujinga wako mwingine wa kuokoteza majibu yangu ya jana kisha kuyaleta kwenye majibu yangu kwako ya leo, wala usijue nakujibu kulingana na vile unavyokuja, naona nikuache nao.

Unachekesha sana unapodai natoka nje ya mada wakati nimekupa mpaka majibu ya ujinga wako wa leo toka google. Unaonekana mswahili usiyejielewa acha kujiona mwalimu hapa ndani, nimeshakuonesha nawe ni mjinga tu.

Usinune mimi ndio nimemaliza, next time unaweza kuja na mada inayoeleweka tukaenda sawa, sio hii ya kipuuzi tu, ujue na kuvumilia watu na misimamo yao hapa ndani, wewe sio mwalimu wetu.

1. Haipo shaka kuwa dawa itakuwa imekuingia vilivyo:

GFfUGgLWkAAh9uE.jpeg

2. Aliwaona Ulimwengu:

FrmmsPmWIAMDMwY.jpeg

3. Hapo #2 dawa yake ni kushule tu ndugu zangu.

4. Bila kusahau adui yetu ni CCM:

Tutambuane: Wenye ujasiri au sababu za kuikabili CCM
 
hili neno chawa nadhani matumizi yake mnayakosea

1. Jina Hilo ni sahihi.

IMG_20240402_054957.jpg

2. Ukitaka kumwua nyani usimwangalie usoni.

3. Ukitaka kumwua mbwa mtafutie jina baya!

4. Chawa harufu yao ni mbaya.

Kwa hakika kama "skin tight" jina limewakaa!
 
1. Haipo shaka kuwa dawa itakuwa imekuingia vilivyo:

View attachment 2953667

2. Aliwaona Ulimwengu:

View attachment 2953683

3. Hapo #2 dawa yake ni kushule tu ndugu zangu.

4. Bila kusahau adui yetu ni CCM:

Tutambuane: Wenye ujasiri au sababu za kuikabili CCM
Hauna dawa yoyote, ni ujuaji wako tu naona majibu yangu huyaelewi, ngoja nitumie jibu la mwingine kukuonesha ulipokosea japo najua utabisha tena...

Soma tena comment ya Mag3 vizuri kuanzia alivyoanza mpaka alivyomaliza kwenye paragraph yake ya mwisho, simply amekuonesha udhaifu wa thread yako.

- Kwako chawa ni yeyote mwenye msimamo usioyumba kwenye jambo fulani, ukasahau anaweza kuwa na msimamo usioyumba kwa kuwa na sababu za msingi kutetea msimamo wake, hapo ndio kwenye kiini cha mapungufu ya uzi wako.

Ndio maana Mag3 kwa kuielewa mantiki ya uzi wako, amekuonesha sababu zake za kuiponda CCM all the time {ambazo kwako ni sawa na uchawa sababu hujali kama ana sababu za msingi kufanya hivyo}

Kisha mwishoni akakwambia hata kama ukimuona chawa kwa huo msimamo wake { coz anajua ndio mtazamo wako}, basi muone hivyo, huyu ameielewa mantiki ya uzi wako ambayo haiko sahihi na ndio ninayojitahidi kukuelewesha tangu jana sijui juzi ajabu hutaki kuelewa...

Wanaokuunga mkono hapa wana upeo sawa na wako, upeo ambao sio sahihi.
 
1. Ninayo heshima kuu kwake Mag3, andiko lake kama ilivyo ada, nimelijibu lote: hoja kwa hoja.

2. Kama una reference ya Mag3 rejea kwenye majibu yangu kwake, yote yamejibiwa mule.

3. Huna jipya.
 
Ninachukua muda kukujibu kila hoja kwa maana ninaona unapoteza uelekeo, kujisahau na hata kuanza kutoa vitisho mbuzi. Ustaarabu ni kitu cha bure ndugu na hoja hupingwa kwa hoja.

'In red ni hoja zako. Kwenye kijani ni nukuu zako tokea maandishi yako ya awali kwenye uzi huu. Kwenye blue ni nukuu zangu tokea kwenye uzi huu unazoonekana kutaka kuzipotosha kwa makusudi."

Unajichanganya sana, tuliza kichwa chako aisee, nikisoma hiyo namba moja ulivyoijibu naona kabisa unazidi kujimaliza mwenyewe, sasa kuna tofauti gani hapo kati ya #1 kutoa maoni na #2 mawazo binafsi?!

1. Ulikiri mwenyewe kuwa andiko langu hili lilikugusa wewe binafsi.

Nitaonyesha nani baina yangu na wewe anaye jichanganya na bila shaka anayepaswa kutuliza kichwa chake aisee.

2. #1 na #2 kama nilivyoziandika, ziko tofauti:

"1. Kutoa maoni mtu aonavyo (free style) hakuwezi kuwa u chawa; hiyo ni haki ya msingi ya kila mwenye akili timamu.

2. Uchawa ni kukosa mawazo binafsi (kwa kesi yako) mwamba ni malaika na Chadema ilishuka kutoka mbinguni; hakipo cha kukosoa jana, leo, wala kesho"
.

Ikikupendeza zipitie tena kujiridhisha.

Kwani mtu akitoa maoni yake hapa huwa sio mawazo yake binafsi? una hakika huwa wanashawishiwa from outside? au wewe ni mpiga ramli humu JF! wewe ndie mwenye tatizo la kuingilia uhuru wa wengine kutoa maoni yao, uko gizani sana.

3. Mada hii inahusu:

"Makundi saba ya chawa kindaki ndaki yanayotatiza mabadiliko"

Haya uliyoandika wewe hapa umeyaokota wapi ndugu?

4.Mimi si mpiga ramli wala sijui kama mko wapiga ramli humu. La ramli ni lako. Kunihukumu kuwa ndiye mwenye tatizo si haki kwani wewe si Mungu wala malaika. Kama ni maoni tu ila kutokujua namna ya kujieleza, kwanini hudhani wengine pia tunaweza kuwa tunaona wewe ndiye mwenye tatizo, na yote mengine yanayofuata kama unavyo ni tuhumu wewe?!

Hata nawe huwa una tabia ya kumuona Lissu malaika, hujijui tu; au ndio stori ya nyani hajioni...na wala hayupo aliyekuita chawa, mimi nipo nakutazama tu unavyojiinua kunyooshea kidole wengine.

5. Ujasiri wa kunisemea unaupata wapi ndugu? Wapi uliwahi kuyasoma hayo uliyoyaandika hapa? Hayo ya nyani kutokujiona .. kwa nini hudhani yanaweza kuwa yanakuhusu wewe zaidi? Mtu hawezi kuniita chawa kwa sababu nitaonyesha pasipokuwa na shaka kuwa mimi siyo.

Kwani chawa hawajijui ndugu? Zingatia #1 pale juu, wewe ulishakiri mwenyewe kuwa ni chawa kwa mujibu wa tafsiri ya kwenye mada.

Kuhusu wewe kuniangalia ... kama unavyosema, kwa nini hudhani wengine nao wanaweza kuwa hawanioni kama unavyoniona wewe na labda wala hawaoni popote ninapo hata jaribu kujiinua? Au kwani wewe ni nani ndugu?

"Au hata kwanini hudhani unavyodhani waniona wewe mimi nami nakuona wewe hivyo labda hata hovyo zaidi?"

Mara nyingi tu nawakosoa Chadema humu ndani, lakini kukosoa kwangu lazima kuwe na sababu sio kukurupuka tu, au Mbowe ikitokea kuna sababu ya msingi kumkosoa, namkosoa, lakini sio kumkosoa hovyo ilimradi nikufurahishe wewe!.

6. Hebu linganisha haya na kauli yako hii:

Duh!, sasa hapo umeliacha kundi gani ambalo lipo JF?!

Kwa huo mtazamo wako, naona umetumaliza wote kwa kutuita machawa!.

Kwamba kwa kesi yako::
a) Mbowe ni Malaika

b) chadema imeshushwa tokea mbinguni.

Kumbe hukosoa vipi au wapi basi, kwa kukiri kwako huko? Wewe huoni unavyojichanganya na bila shaka ni muda wako wa kutuliza kichwa sasa?

Sio kumkosoa kienyeji tu kama ufanyavyo na wenzako kumtaka aachie ngazi wakati aliwekwa pale kihalali, kwanini mnaingilia uhuru wa mtu kujiamulia mambo yake? huu upungufu wako ajabu huuoni sijui una upeo wa aina gani!.

7. Wapi nimemkosoa yeyote kienyeji? Au wapi nimemtaka waye yote aachie ngazi? Wenzangu ni nani unaojaribu kuninasibu nao? Mimi na nani tumeingilia uhuru wa nani wapi wa kujiamulia? Wapi hata nimeingilia uhuru wa mtu kuwa chawa au la?

8. Wewe si Mungu wala malaika kujaribu kunihukumu au kumhukumu awaye yote. Kusema, "huu upungufu wako .." ni kutoa hukumu. Kama labda ni maoni yako ila kutokana na umbumbu tu wa kujieleza, kwa nini hudhani wengine nao wanaweza kuwa hawaoni hivyo au labda nami kwa maoni yangu nakushangaa: "huu upungufu wako ajabu huuoni au sijui una upeo wa aina gani!

Nakushauri tena, jifunze kuvumilia wenzio humu ndani, usijigeuze jaji wa mahakama ya jukwaa la siasa hapa JF. Narudia tena, hii assessment yako haina maana sababu hata nawe unaangukia kwenye moja ya hayo makundi uliyotaja pale juu, simply nawe ni chawa wa Lissu

9. Sina hakika kwa nini umeandika haya na wala hata kwa misingi ipi. Kama ni kutokana na mada huru hii:

"Makundi saba ya chawa kindaki ndaki yanayotatiza mabadiliko"

mbona itakuwa ni jambo la kushangaza mno?!

Kuna jina la mtu ametajwa humu? Au wewe ni @lucas_mwashambwa au MK254 watani zangu wa jadi niliowataja seat ya mbele pale? Au wewe ni wao? Au unajua kwanini tunatajana nao na mara ngapi kwenye nyuzi zilizopo zisizokuwa na idadi?

Wewe ni nani kujipa kazi au mamlaka za kushauri watu na hapa ati umenizukia kihasara hasara kutaka kunishauri miye? Kama wewe ni jamaa mwingine tu humu JF, mbona itakuwa ni maajabu ya Mussa? Au kumbe, wenda wazimu utakuwa ni upi, kama huu siyo?

kwanini hudhani mwenye kuhitaji kushauriwa na/au kuaswa kujifunza kuwavumilia wengine ni wewe? Wapi nimejifanya jaji, mahakama au hata kujaribu kutoa hukumu? Kweli nyani haoni kundl*ule.

"Mara ngapi nimekukumbusha kuacha kuhukumu kwamba wewe si Mungu wala malaika?"

10. Assessment yangu Ina maana sana Kwa maana kama wewe unaangukia mle kama ulivyokiri mwenyewe ninao uhakika simp humo na wengi wengine hawamo mle. walioko mle ni mzigo na hawana mchango wowote kwa taifa hili.

11. Mimi ni chawa wa Lissu? Upo nje ya mada ndugu. Kwenye list kuna makundi 7 ambapo Lissu hayumo. Kama ungependa kumjadili Lissu na chawa wake kama wapo, si uanzishe uzi, ukiwa na hoja tutachangia?

Angalizo, kwa vile wewe si msemaji wangu, kulikoni kunisemea mimi hali miye sijamsemea mtu? Nikadhani unapaswa kujishangaa zaidi ya sana ndugu?!

Kuwa makini sana, you are creating a seed of your own destruction kwa "ego" yako, nimemaliza ukitaka fuata ushauri ukitaka acha, its your choice kama ilivyo choice ya wengine humu ndani kuandika kile watakacho, muhimu utambue wewe sio mwalimu wetu hapa.

Usinitishe ndugu. Kila mtu ana destiny yake. Aliyechagua kuwa chawa, "haya" aliyechagua kuwa si chawa, "haya!" Ukichagua kuwa chawa hiyo ni juu yako; ukiamua kuwa si chawa ni juu yako. Kama ilivyo kwangu naamini.

Makasiriko na vitisho ya nini sasa? Si ujivunie uchaguzi wako? Kwani kuna aliyekuchagulia? Si ulichagua mwenyewe?

Nani amekwambia yeye ni mwalimu wa mtu au anataka kuwa mwalimu au anahitaji hata wanafunzi?

Ninarudia, usinitishe ndugu!

Bure kabisa!

Masaa 48 yameisha, badala ya kushambulia Israel bado mnanyanyua haya mavitu

main-qimg-17512da37a0b1e02107ce7cc1999f006
 
Haipo vita ni ufafanuzi au kupeana taai maana waweza mcheka @lucas_mwahambwa au MK254 kumbe na wewe ni wale wale.

Hiiiiiiii ..III!

Masaa 48 yameisha, badala ya kushambulia Israel bado mnanyanyua haya mavitu

main-qimg-17512da37a0b1e02107ce7cc1999f006
 
Duh!, sasa hapo umeliacha kundi gani ambalo lipo JF?!

Kwa huo mtazamo wako, naona umetumaliza wote kwa kutuita machawa!.

Halafu hilo kundi la wajuaji naona linaingia kwenye hiyo quote ya Nyerere uliyoiweka hapo chini, hao ndio vijana Nyerere alitaka wawepo kwa mtazamo wangu, sio ndio mzee kila mahali..

Now, iweje wajuaji nao uwaite machawa?!

Tukatanabaisha kuhusiana na machawa wakiwamo wa mwamba, kama kawaida wakiwamo machawa yale yenyewe yakapinga.

imhotep, Proved, Retiree, GWAMAKA USWEGE, Erythrocytes, Tlaatlaah, waliomo na wasiokuwamo au nasema uongo?
 
Tukanabaisha kuhusiana na machawa wakiwamo wa mwamba, kama kawaida wakiwamo machawa yale yenyewe yakapinga.

imhotep, Robert hariel mtibeli, Proved, Retiree, GWAMAKA USWEGE, Erythrocytes, Tlaatlaah, waliomo na wasiokuwamo au nasema uongo?
Gentleman,
kubabaika na kung'ang'ana na dhana potofu zisizo na athari zozote kijamii, kisiasi au kiuchumi ni sawa na kuamuni uchawi na ushirikiana tu,

utachelewa sana kufika kwenye ndoto zako 🐒
 
Back
Top Bottom