Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
.................Mkuu bora umeanzisha huu uzi hapa.
Juzi jumamosi nikiwa natoka home na mvua hizi maji yametuama hovyo naelekea stand za huku mitaani maeneo ya Mbezi Kimara bwana mdogo mmoja yupo na gari yake Mazda model siikumbuki ila ni hizi saloons za 9.7/10.5mill mimi napita pembeni mwa barabara huku nazungumza na simu sina hili wala lile mara pwaa!
Mimaji michafu suruali yote mpaka raba nilizokuwa nimevaa zimebadilika rangi zimekuwa tope na nilivaa cadet ya khaki simple nyeusi na nyeupe,wala hakujali na sababu barabara ina mashimo alikuwa anaenda speed ndogo sana but alishindwa hata kushusha kioo kuniambia samahani nachokumbuka aligeuka kidharau akanitazama kisha huyoo akenda zake huku seat ya kushoto amekaa mwanamke wake ameweka miguu kwenye dushboard wala hawakujali.
Sehemu yenyewe ni karibu na CCM wanakolaza magari sasa jamaa waliokuwa wamekaa pale picha waliiona wakaniambia bwana huyu jamaa gari yake huwa inalalaga hapa yeye kapanga kwenye nyumba ile palee!nikajisemea kimoyo moyo hakika Tanzania ukiwa na gari wewe ndo tajiri yaani amepanga chumba na sebule ananimwagia mimi maji machafu hata haonyeshi ubinaadam?any way niliacha likapita ila siyo vizuri tusidharauliane sana tunapohisi tuna mafanikio fulani wakati mwengine unaemdharau anaweza kuwa amekuacha mbali sana wanojua wakakucheka.
Hivi kuishi nyumba ya kupanga nako ni kujisifu? Uwe Area D, Kigamboni, au Masaki, kwa mwenye akili ni kitu kile kile.tusisahau na vijana waliopanga kinondoni, sinza na siku hizi tabata. [emoji16][emoji16][emoji16]
ungemtukana au ungeniitapo MkuuJana nilikua na-argue na malaya mmoja twitter, kisa ana followers elfu 25 anajiita motivational speaker, basi mimi nina followers chini ya 100 pamoja na a/c kua ina miaka zaidi ya 9 twitter, basi anajiona mkuuuubwa na mjaaanja kisa ana followers 25k na anatweet kwa iphone basi anajiona mjaaanja,unawaangalia unawaonea huruma.
Watu wa hivyo wanajiona wameyapatia sana maisha huku sisi tusio na followers wengi tukionekana hatuna kitu.
Watu wengine hovyo sana.
Yes JW wanatumia neno "RAIA" kama kejeli.Mzee wangu kastaafu long sana ila hili "RAIA" analitumia sana kwa watu kama kejeli
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] huwa wanatuonaje sijui wenye tecno spark 2
- Wanaojua kuzungumza Kiingereza hata kama wanazungumza Kiingereza "broken". Wote ni mashahidi, hawa hata hapa JF wapo. Siku zote hujihisi wao ni bora na maisha wameyapatia.
- Wanaomiliki matoleo mbalimbali ya simu za iPhone. Siongezi neno kuhusu kundi hili.
- Waliochukua mchepuo wa masomo ya sayansi walipokuwa sekondari na baadaye wakaenda vyuo vikuu kusomea kozi mbalimbali za uhandisi. Hawa hata ukiwakuta mtaani bila ajira, by default wanajihisi tayari wameyapatia maisha.
- Wenye followers kuanzia elfu 20, 30, 40 au zaidi kwenye mtandao wa Instagram. Hili ni kundi ambalo linajihisi limeyapatia sana maisha kwa kuwa na followers wengi. Wanafollow mastaa tu. kma wewe sio star usitegemee kama atakufollow back.
- Wahitimu vijana wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Siongezi neno kuhusu kundi hili.
- Vijana wa kitanzania ambao kwa wakati fulani waliwahi kuishi Marekani au Uingereza halafu kwa sasa wamerudi bongo kupambana na msoto wa maisha.
- Wanaomiliki gari jamii ya Vitz, IST na Altezza. Jeuri na mikwara yao barabarani inatupa picha halisi.
- Wanajeshi vijana miezi yao kwanza kwenye ajira jeshini halafu uwakute uraiani wamevaa zile gwanda zao.
Ongezea wengine unaowajua.
Karibuni.
We jamaa mpole sana, Aiseee! Yaani mtu anakumwagia maji machafu unaonyeshwa mpaka kwake halafu wewe unamuangalia tu..................Mkuu bora umeanzisha huu uzi hapa.
Juzi jumamosi nikiwa natoka home na mvua hizi maji yametuama hovyo naelekea stand za huku mitaani maeneo ya Mbezi Kimara bwana mdogo mmoja yupo na gari yake Mazda model siikumbuki ila ni hizi saloons za 9.7/10.5mill mimi napita pembeni mwa barabara huku nazungumza na simu sina hili wala lile mara pwaa!
Mimaji michafu suruali yote mpaka raba nilizokuwa nimevaa zimebadilika rangi zimekuwa tope na nilivaa cadet ya khaki simple nyeusi na nyeupe,wala hakujali na sababu barabara ina mashimo alikuwa anaenda speed ndogo sana but alishindwa hata kushusha kioo kuniambia samahani nachokumbuka aligeuka kidharau akanitazama kisha huyoo akenda zake huku seat ya kushoto amekaa mwanamke wake ameweka miguu kwenye dushboard wala hawakujali.
Sehemu yenyewe ni karibu na CCM wanakolaza magari sasa jamaa waliokuwa wamekaa pale picha waliiona wakaniambia bwana huyu jamaa gari yake huwa inalalaga hapa yeye kapanga kwenye nyumba ile palee!nikajisemea kimoyo moyo hakika Tanzania ukiwa na gari wewe ndo tajiri yaani amepanga chumba na sebule ananimwagia mimi maji machafu hata haonyeshi ubinaadam?any way niliacha likapita ila siyo vizuri tusidharauliane sana tunapohisi tuna mafanikio fulani wakati mwengine unaemdharau anaweza kuwa amekuacha mbali sana wanojua wakakucheka.
Uamuzi wa maana sanaWala....mistakes zipo mkuu mimi nilichukulia kibinaadam na ni mtaani ninapoishi sikutaka nifanane nae akili wote tuonekane mazombie nilimsikilizia labda atajishusha but sivyo nilivyotegemea.yupo tu jirani na kwangu so ipo siku atanipa heshima yangu sina haraka nae.
Kwa waliojenga nyumba kiasi wamepiga hatua mkuuVijana waliojenga nyumba, vijana wanaofanya kazi bank
HahahHa, wanakuja nazo za nini sasaHakuna watu wananishangaza kama hao wanaokuja night club na MacBook.
Nakazia hapaBaada ya kuyajua maisha jinsi yalivyo, yoyote aliyejenga nyumba kwa kutumia hela halali namuheshimu sana.
NAKAZIA HOJANAOMBA UTUTOE SISI WAHANDISI KTK HILO GROUP,SISI HATURINGI ILA WATU WANAVYOTUONA NA KUTUCHUKULIA TU MKUU.
BY THE WAY TUMESOMA PIA,SI SAWA KUTUCHANGANYA NA HAO WAMILIKI IPHONE NA FOLLOWERS PLUS KUISH MAREKANI.
Eng.Fasiliteta
[emoji23][emoji23][emoji23]Vijana waliojenga nyumba, vijana wanaofanya kazi bank
Hahaha [emoji23]Kuna majamaa flani jioni jioni utawaona wana kopo la maji ya kilimanjaro wamevaa vi pensi vya khaki na mashati ya form six.. mikononi wameshika simu kubwa huku wamening'iniza funguo kwenye luxi ya kaptula..
Hawa wanaona maisha wameyapatia kabisa
Sijawahi kuelewa kwanini wanakuja nazo kwakweliHahahHa, wanakuja nazo za nini sasa
Amesema huku kuna majukwaa tofauti kwahiyo unachagua mwenyewe jukwaa linalokufaaUnaizungumzia JF ipi mkuu?
JF hii ambayo topic ya kula mademu kimasihara inapata page 50 kwa siku mbili tu?
Unazingumzia JF ipi ambayo hakuna mashoga na makahaba
Jf ipi ambayo ni tofauti na fb,instagram na twitter?
Sikiliza mzee labda tofauti huku hatutupii picha zetu
Ila ujinga wa social media ni ule ule