Makundi yafuatayo yanategemewa kumpigia kura mgombea wa CHADEMA Tundu Lissu

Makundi yafuatayo yanategemewa kumpigia kura mgombea wa CHADEMA Tundu Lissu

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
15,842
Reaction score
31,076
Tukiwa tumebakiza siku moja pekee, ili tuingie kwenye uchaguzi mkuu, hapo kesho kutwa, nimejaribu kufanya tathmini na kuona ni makundi yapi yanaweza kumpa kura kwa wingi sana mgombea wa CHADEMA Tundu Lissu.

Makundi yafuatayo yanategemewa kumpigia kura Tundu Lissu:-

1. Mamilioni ya wanachama na wapenzi wa chama cha CHADEMA

2. Wanachama na wapenzi wa chama cha ACT Wazalendo.

3. Wafanyakazi bila kujali itikadi zao za kisiasa, walionyimwa kuongezewa mishahara yao kwa kipindi chote cha utawala wa awamu ya tano.

4. Wafanyakazi bila kujali itikadi zao za kisiasa, waliowekewa kikotoo kipya cha malipo, cha mifuko ya jamii, ambacho naweza kudiriki kuita kuwa ni "mauaji" kwa wafanyakazi hao.

5. Wafanyibiashara kwa maelfu, bila kujali itikadi zao za kisiasa, wamefunga biashara zao, baada ya TRA kuwafungia biashara zao, baada ya kuwakadiria kodi kubwa sana, ambayo wameshindwa kuzilipa.

6. Wafanyakazi kwa maelfu, bila kujali itikadi zao za kisiasa, wamefukuzwa kazi kwa madai ya kutimia vyeti feki.

7. Wananchi wa Kimara hadi Kibaha, bila kujali itikadi zao za kisiasa, waliobomolewa nyumba zao, bila ya kulipwa hata kidogo, ili kupisha upanuzi wa barabara nane, licha ya wakazi hao kupeleka suala lao mahakamani na mahakama hiyo kuwekea "court injunction" kesi hiyo.

Unaweza kuongezea makundi mengine, yatakayomnyima kura mgombea Urais wa CCM, John Magufuli na kumpigia kura mgombea Urais wa CHADEMA, Tundu Lissu.
 
@ Wakulima ambao tulilima mashamba yetu tukavuna tukahifadhi kusubiri Bei ichangamke. ili tupunguze machungu ya shamba. Akaja kutupangia pa kuuza na kutupangia bei

@ Wafanya biashara wa mawe/madini

@ Waandishi wa habari

@ CCM asilia
 
Lissu lazima ashinde uchaguzi huu. Nadhani ni kati ya vita ya haki na dhuruma

Ni vita ya Mungu na shetani.
Lissu angeshinda endapo tu, narudia, endapo tu angewahakikishia watanzania ya kuwa ana malinda kamili kwa kufanyiwa uchunguzi na jopo la doctors. Lakini bila ya hivyo hiyo fununu ya kwamba amefumuliwa malinda haimwachi salama.
 
Kwa kweli.. munadanganya kama vile munaweza shika mikono ya watu kuweka tiki.. boksi la kwanza tiki tiki kwa kwenda mbele.. kuangalia zaidi ya hapo tutapata maruweruwe..

Muhamie Mars.. huko mtapata mnayoota

Jumatano
Magufuli 2020💯

Haina ubishi..
 
Bila kusahau wafanyakazi wote na wahitimu waliolazimishwa kukatwa 15% ya basic zao nje ya mkataba.

Kazi hamfanyi,mnataka vya dezo.. mmepokea mikopo.. ni wajibu wenu kulipa.. "asie fanya kazi na asile" msemo wa Rais Magufuli..
Hamuoni aibu kutaka dezo dezo.. mkopo ni mkopo lazima ulipwe.
 
Back
Top Bottom