Detective J
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 24,058
- 41,518
wana uwezo huo kabisa. bahati mbaya sio watanzania. na hawaishi tanzania .Yaani hao wenzetu huwa wanagoma kununua vocha?!!!
Mimi vocha nitanunua na bando nitajiunga. Kwanza niseme wazi Bei iongezeke maradufu wajinga wapungue mitandaoni
Mzee hii ingewezekana nyakati za Nyerere siku hizi watu wenye akili hawatumii simu kwaajili ya porojo ni OFISI chakufanya kupaza sauti kwa mamlaka waondoe huu ujingaWabongo ni macoward sana muda mwingine.....
Nasema sisi wanunua vocha tukiuchuna japo kwa siku 30 tu..... Utakuja kuona hiyo simu kama ndani ya wiki moja hawatakaa kurekebisha vifurushi na kurejesha vile tunataka....
Serikali pia inachangia hizi gharama kupandisha,, kodi iko juu kwa wafanyabiashara faida inayopatikana ni ndogo unategemea nini!!!Kwenye huu mgomo, tutaishia tu kusalitiana. Jambo la msingi Serikali iangalie kilio cha raia wake. Kama hakuna ulazima wa kuwaumiza, warudishe tu utaratibu kama zamani.
Ila kususia kabisa, sidhani! Mawasiliano kwa sasa ni jambo muhimu sana. Ingekuwa ni miaka ile ya 1990's tungeweza.
Kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ndio njia sahihi, na wakiona matumizi yame pungua wanaweza kuchukua hatua zitakazo tusaidia. Lakini kugoma kabisa ni njia ngumu kiutekelezaji kwa sababu wapo wanao tegemea vocha kutokana na shughuli zao.Ongezeko jipya la bei za vifurushi bila shaka ni matokeo ya mazungumzo baina ya waziri mwenye dhamana na wamiliki wa mitandao ya simu.
Tuoneshe kupinga kwa vitendo tusinunue vocha tuziache simu zetu hewani bila vocha mpaka pale watakaposhusha gharama za vifurushi tunaumizwa kwa kweli.
Wenye mitandao watakosa fedha na hiyo itapelekea hata serikali kukosa fedha ambazo wanapata kama kodi lazima watakaa chini kuangalia upya vifurushi vya simu lakini kama tutakua tunalalamika halafu tunaendelea kununua vifurushi vyao hawatahangaika na sisi.
Tungekua wote Ni Wana CHADEMA Hilo Ni Jambo rahisi mno. Tatizo Kuna wenzetu wa vyama vya kijinga, wao hata uwaambie wakale jalalani hakika watakwenda kula.Wabongo ni macoward sana muda mwingine.....
Nasema sisi wanunua vocha tukiuchuna japo kwa siku 30 tu..... Utakuja kuona hiyo simu kama ndani ya wiki moja hawatakaa kurekebisha vifurushi na kurejesha vile tunataka....
ukiweza ingia app store pakua free basic
Dah! itabidi tufanye hivyo lakini itachukua muda zaidi kuzoeaInawezekana kupunguza,mimi sio mpigaji sana wa simu,huma najiunga pale ninapokuta missed call au ujumbe muhimu tu,kwa hali ilivyo sasa nitapunguza zaidi matumizi,kuingia online mara tatu kwa wiki itanitosha kabisa..
Kwa vodacom wameshaiondoa
au ingia app store pakua free basic ndani ya free basic utatembelea web nyingi bila malipo ikiwemo jf,Wikipedia, BBC, BBC Swahili nk
Nchi za wenzetu bundle ni bei ghali ukilinganisha na sisi.
Ametumia freebasicsHii meseji ya kuhamashisha mgomo wa kununua vocha umetumia kifurushi (vocha) au umetumia hewa kuituma humu ndani??!!
the truth is wabongo hatuna umoja kabisa.Kumobilize wabongo tufanye kitu, ni shughuli, muulize Mange hana hamu na sisi.