Malalamiko hayatoshi tusinunue vocha

Malalamiko hayatoshi tusinunue vocha

Yaani hao wenzetu huwa wanagoma kununua vocha?!!!
wana uwezo huo kabisa. bahati mbaya sio watanzania. na hawaishi tanzania .
ila wana umoja sana kiasi kwamba wanaweza ku force serikali isifanye jambo.

ila bongo ni kulalamika mitandaoni
 
Sudan wamepindua serikali sababu ya mkate, sisi tupindue serikali sababu ya bei ya internet tatizo sasa tunajijua
 
Nunua vocha, ila usijiunge 'bando la data'
 
Mimi vocha nitanunua na bando nitajiunga. Kwanza niseme wazi Bei iongezeke maradufu wajinga wapungue mitandaoni

Wewe ni mmoja wa wale walioteuliwa sio? Kiumbe kinapata laki tatu kikao kimoja kina shida gani!!! Futa comment yako mkuu.
 
Wabongo ni macoward sana muda mwingine.....

Nasema sisi wanunua vocha tukiuchuna japo kwa siku 30 tu..... Utakuja kuona hiyo simu kama ndani ya wiki moja hawatakaa kurekebisha vifurushi na kurejesha vile tunataka....
Mzee hii ingewezekana nyakati za Nyerere siku hizi watu wenye akili hawatumii simu kwaajili ya porojo ni OFISI chakufanya kupaza sauti kwa mamlaka waondoe huu ujinga

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
hapa mzee baba ni noma nia yao nikupunguza watu wanao kesha mutandaoni /ira kesho wanabadirisha maana watu weng tuna weka sm kweny beg/zinakua za kuchezea games
 
Kwenye huu mgomo, tutaishia tu kusalitiana. Jambo la msingi Serikali iangalie kilio cha raia wake. Kama hakuna ulazima wa kuwaumiza, warudishe tu utaratibu kama zamani.

Ila kususia kabisa, sidhani! Mawasiliano kwa sasa ni jambo muhimu sana. Ingekuwa ni miaka ile ya 1990's tungeweza.
Serikali pia inachangia hizi gharama kupandisha,, kodi iko juu kwa wafanyabiashara faida inayopatikana ni ndogo unategemea nini!!!
 
Ongezeko jipya la bei za vifurushi bila shaka ni matokeo ya mazungumzo baina ya waziri mwenye dhamana na wamiliki wa mitandao ya simu.

Tuoneshe kupinga kwa vitendo tusinunue vocha tuziache simu zetu hewani bila vocha mpaka pale watakaposhusha gharama za vifurushi tunaumizwa kwa kweli.

Wenye mitandao watakosa fedha na hiyo itapelekea hata serikali kukosa fedha ambazo wanapata kama kodi lazima watakaa chini kuangalia upya vifurushi vya simu lakini kama tutakua tunalalamika halafu tunaendelea kununua vifurushi vyao hawatahangaika na sisi.
Kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ndio njia sahihi, na wakiona matumizi yame pungua wanaweza kuchukua hatua zitakazo tusaidia. Lakini kugoma kabisa ni njia ngumu kiutekelezaji kwa sababu wapo wanao tegemea vocha kutokana na shughuli zao.
 
Wabongo ni macoward sana muda mwingine.....

Nasema sisi wanunua vocha tukiuchuna japo kwa siku 30 tu..... Utakuja kuona hiyo simu kama ndani ya wiki moja hawatakaa kurekebisha vifurushi na kurejesha vile tunataka....
Tungekua wote Ni Wana CHADEMA Hilo Ni Jambo rahisi mno. Tatizo Kuna wenzetu wa vyama vya kijinga, wao hata uwaambie wakale jalalani hakika watakwenda kula.
Ona Chadema tulivyokua na umoja, mmoja wetu akipigwa faini kwa kesi ya kubambikiwa ndani ya one hour milioni zimepatikana.
 
Inawezekana kupunguza,mimi sio mpigaji sana wa simu,huma najiunga pale ninapokuta missed call au ujumbe muhimu tu,kwa hali ilivyo sasa nitapunguza zaidi matumizi,kuingia online mara tatu kwa wiki itanitosha kabisa..
Dah! itabidi tufanye hivyo lakini itachukua muda zaidi kuzoea
 
Lile shirika la kulinda haki za walaji bado liko Tanzania? Mchakato wa bei za vifurushi ulitumia utaratibu gani? Walaji walihusishwa vipi? Walisikilizwa? Au ndio zile mentality za watatufanya nini hawa? Si chochote si lolote tuwaburuze tu.
 
Nchi za wenzetu bundle ni bei ghali ukilinganisha na sisi.

Hii comparison haina maana, kama mmarekani analipa USD 100 kwa mwezi (TZS 234,000) kwa ajili ya internet lakini median income ya nchi ni USD 31,000 kwa mwaka ( ~ TZS 72,000,000).

Sasa wewe unataka TZ tulipie bei hiyo wakati hiyo 234,000 ndo take home ya mtu?

Ukicompare bei compare na vipato vya nchi au sehemu husika ndo utapata uhalisia sio blind comparisons
 
Back
Top Bottom