Malalamiko hayatoshi tusinunue vocha

Malalamiko hayatoshi tusinunue vocha

Hii ya sasa hata haihitaji kuhamasisha mgomo yenyewe ni mgomo tosha,siwezi kutoa buku langu kwa Mb 450 et kwa wiki wakati huko mwanzo hiyo 1 Gb tu unatumia siku tatu tena hapo ndio kwa kujinyima nyima sasa Mb 450 tanunua mara ngapi?
 
Mimi vocha nitanunua na bando nitajiunga. Kwanza niseme wazi Bei iongezeke maradufu wajinga wapungue mitandaoni
Inaonekana wasio na uwezo wa kununua hivyo vifurushi ndo hao unaosema wajinga wapungue mitandaoni... Mkuu wewe ni masaburi
 
Ina maana wajinga hawana pesa ya kununua vocha?

Vipi kuhusu wanafunzi wa chini na wa juu wanaotegemea mitandao kusomea nao ni wajinga?
Hilo jamaa ni takataka... Mijitu mingine ilizaliwa chooni sijui?
 
Kabisa na ndio maana HAKUNA wajinga mitandaoni
nnchi gani kwanza maana nnchi nyingi wanatumia fiber na fiber ni bei rahisi na unakuta ipo kila mahali wao bando zao za kawaida wanazotumia ni zakupigiana sana sana maana akiwa jazini wifi nyumbani wifi kwenye usafiri wifii
 
Kwani MATAGA nao wanauziwa bei sawa na wanyonge mbona kama wote wanalalamika mimi nilidhani watoto wapendwa wa mfalme wanapata upendeleo?
 
Smart4n bila vocha ni kama Masai bila rungu.
Mimi narudi humu,sipendagi ujinga
IMG-20210402-WA0010.jpg
 
Tuweke bundle ili tuwaambie wengine wasinunue vocha.
 
Ongezeko jipya la bei za vifurushi bila shaka ni matokeo ya mazungumzo baina ya waziri mwenye dhamana na wamiliki wa mitandao ya simu.

Tuoneshe kupinga kwa vitendo tusinunue vocha tuziache simu zetu hewani bila vocha mpaka pale watakaposhusha gharama za vifurushi tunaumizwa kwa kweli.

Wenye mitandao watakosa fedha na hiyo itapelekea hata serikali kukosa fedha ambazo wanapata kama kodi lazima watakaa chini kuangalia upya vifurushi vya simu lakini kama tutakua tunalalamika halafu tunaendelea kununua vifurushi vyao hawatahangaika na sisi.
hahahahaaaaaaaaa, mimi nitanunua kwa bei yoyote
 
Bundle pumnzi ya smartphone,haya nani anataka kuiua ya kwake kwa kuinyima vocha
 
Tufufue matumizi ya posta. Tuandikiane barua. Posta wapunguze bei ya stampu. Tusipotumia simu kwa wiki moja watakoma!
 
Back
Top Bottom