Malalamiko Katika Kura za Maoni kwenye Uchaguzi Mdogo Jimbo la Isimani, Iringa

Malalamiko Katika Kura za Maoni kwenye Uchaguzi Mdogo Jimbo la Isimani, Iringa

Joined
Sep 23, 2023
Posts
22
Reaction score
44
Baadhi ya wajumbe walioshiriki katika kura za maoni za uteuzi wa Mgombea Ubunge Jimbo la Isimani kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) wameibuka na malalamiko wakidai kutoridhishwa na mchakato uliotumika kuwashindanisha wagombea hao.

Wajumbe hao wamesema kuwa kuna viashiria vinavyoibua wasiwasi juu ya uwepo wa rushwa katika mchakato huo hali ambayo imeathiri matokeo yaliyopatikana kwa makada watatu walioongoza kura hizo za maoni.


Aidha wamelalamikia kukosekana kwa fursa kwa wagombea kujinadi sera zao mbele ya wajumbe katika kila kata, hali iliyopelekea wajumbe hao kutokuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu wagombea hao kabla ya kupiga kura kuteua mgombea atakayeiwakilisha CCM katika uchaguzi huo mdogo.

"Imekuwa jambo la kushangaza kuona baadhi ya wagombea wakipata ushindi wa kishindo ilhali wajumbe wengi hawawafahamu wala hawakusikia sera zao," amesema mmoja wa wajumbe aliyeshiriki zoezi hilo.

Kutokana na hali hiyo wajumbe hao wamekitaka Chama cha Mapinduzi kurejea mchakato huo kwa maslahi mapana ya Chama na wananchi wa Isimani wanaotarajia kuchagua muwakilishi wao ili kuhakikisha haki inatendeka na taratibu zote zinazotakiwa ikiwemo wagombea kujieleza na kujibu maswali ya wajumbe zinafuatwa kikamilifu.

Wamesisitiza kuwa kurejewa kwa kura hizo za maoni kutasaidia kurejesha imani ya wanachama na kuhakikisha kuwa mgombea atakayepatikana anawakilisha kweli matakwa ya wajumbe.
 
Wanyamaze mara moja. Kiwete alipoleta mgombea wake wa mfukoni walishangilia.
 
Vita mbinu, maneno ya mkosaji tu hayo.

Pamoja na hayo ni wazi hela imetumika kwenye kura ya maoni. Iringa (pamoja na Njombe) ni kubwa sana? alipotokea mshindi wa kura ya maoni Makete na Isimani ni mbali sana hawezi kufahamika pande zile bila ya rushwa.

If anything hilo jimbo nalo inabidi likatwe, Isimani ni kubwa kushinda mkoa wote wa Kilimanajaro.
 
Hakuna mtu ana muda na upuuzi wa ccm kwa sasa. Malizaneni wenyewe humo ndani.
 
Back
Top Bottom