A
Anonymous
Guest
Ningependa kuwasilisha malalamiko yangu kuhusu hali ya ufundishaji katika Chuo cha Dar es Salaam Institute of Technology (DIT), ambayo kwa maoni yangu imekuwa ikiwakwamisha wanafunzi wengi kupata ujuzi unaostahili.
Kumekuwa na matukio ambapo baadhi ya walimu hawafundishi ipasavyo kwa kipindi kizima cha semester (Mwalimu haingii darasani semester nzima), lakini wanafunzi bado hufanya mitihani ya mwisho. Hali hii imewahi kutokea na inaibua maswali kuhusu ufuatiliaji wa utekelezaji wa majukumu ya walimu.
Kwa kawaida semester huwa na takribani wiki 15, lakini kuna baadhi ya walimu wanaofundisha mara chache sana, wakati mwingine vipindi visivyozidi vitano kwa semester nzima. Pamoja na hilo, wanafunzi hupewa kazi, ambazo ni vigumu kuzitekeleza kutokana na uelewa mdogo walioupata darasani.
Pia mfumo wa ku acces (CA) ni mbovu kwasababu unategemeana na mood ya mwalimu siku husika. Na pengine mwalimu hufahamu kabisa kulingana na hichi nilichofundisha hiki kitu hakiwezekani hawa kufanya.
Matokeo yake ni kwamba wanafunzi wanajikuta wakihisi kama wananyanyaswa badala ya kupata elimu stahiki waliyoifuata chuoni. Mfumo huu unawaathiri wanafunzi kitaaluma na kuwanyima fursa ya kujifunza kwa ubora unaostahili.
Naiomba Wizara husika pamoja na mamlaka zinazosimamia elimu ya juu kufanya ufuatiliaji wa karibu kuhusu utekelezaji wa majukumu ya walimu na kuhakikisha kuwa ratiba za ufundishaji zinafuatwa ipasavyo. Pia kuwe na mifumo madhubuti ya kuwawajibisha walimu wanaoshindwa kutekeleza wajibu wao, ili wanafunzi wapate elimu bora na yenye viwango vinavyostahili.
Lichukulieni kwa ukubwa, ni vigumu sana mimi kuja kuandika hapa bila sababu za msingi, tunaumia nafsi zetu kimawazo.
Ninaamini hatua za haraka zikichukuliwa zitasaidia kuboresha mazingira ya kujifunza na kuongeza ubora wa elimu katika taasisi za elimu ya juu.