Malalamiko kuhusu utoaji huduma katika Zahanati ya Mkolowony Moshi DC

Malalamiko kuhusu utoaji huduma katika Zahanati ya Mkolowony Moshi DC

A

Anonymous

Guest
Tunaomba kuwasilisha malalamiko kuhusu hali ya utoaji wa huduma za afya katika Zahanati ya Mkolowony iliyopo Moshi DC.

Zahanati hiyo imeruhusu mtu ambaye si mtaalamu wa afya kutoa huduma kwa wagonjwa. Kinachotia wasiwasi zaidi ni taarifa kwamba mtu huyo anahusika hata katika kutoa sindano kwa wagonjwa, jambo linaloweza kuhatarisha usalama na afya za wananchi.

Aidha, kuna malalamiko kuhusu kutunzwa kwa siri za wagonjwa, ambapo taarifa binafsi za baadhi ya wagonjwa zinadaiwa kusambaa mtaani kinyume na taratibu za kitaaluma na maadili ya utoaji wa huduma za afya.

Tunaomba mamlaka husika zifuatilie suala hili, kufanya uchunguzi wa kina na kuchukua hatua stahiki ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma salama, zenye ubora na zinazozingatia maadili ya taaluma ya afya.
 
Back
Top Bottom