Malalamiko ya Makato ya Deni la Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) Mwezi Juni, 2021

Nchi ngumu sana hii... Inakuaje!?? Yani mshahara unakuwa kama hisani...
Mambo yanakera sana hayaa..
 
Mkuu uzi ushaanzishwa hapo juu... Tuendelee kule..
 
madaraja hatujaoanda makato hayapungui,,yaani basi bora walioenda kwenye ujasiriamali huku serikalini kunakatisha tamaa
 
Dawa ya deni kulipa..nyie mlikua mnatulingishia sana na vibumu vyenu..kila wikendi pizza hut kutulingishia life la chuo na videmu vyenu...lipeni achani kulalama.

#MaendeleoHayanaChama
hahaha subiri povu hapa
 
Nakumbuka walitoa wanaodaiwa wote kwenye baadhi ya magazeti nchini nadhani ilikuwa 2016 kuna mdada mmoja humu nikamwambia aangalie kama jina lake halimo. Akaniambia BAK mie nilishamaliza kulipa siku nyingi lakini nitaangalia. Kuangalia kweli akalikuta jina lake na balance kubwa tu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ bahati nzuri anatunza rekodi zake vizuri hivyo akafuatilia na likafutwa ila ilichukua muda.

Hilo deni, bodi ni as if hawataki liishe. Hata ukimaliza kulipa na ukapewa barua ya kumaliza kulipa, siku moja ukijifanya kwenda kucheki tena unashangaa unadaiwa mamilioni. 😁
 
Dawa ya deni kulipa..nyie mlikua mnatulingishia sana na vibumu vyenu..kila wikendi pizza hut kutulingishia life la chuo na videmu vyenu...lipeni achani kulalama.

#MaendeleoHayanaChama
Hahaha,
Cha mto tunakiona. Aise.
 
Mimi imeongezeka laki 5 Ila kwenye statement ila kwenye slip iko vile vile
 
6% walisema wataanza kuitekeleza kuanza mwezi wa saba.

Hilo la kuongezeka deni mara mbili jitahidi utafute ufafanuzi kwa wahusika(HESLB)
Wanasema ongezeko LA deni linatokana na VRF before 1 May.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…