ram
JF-Expert Member
- Oct 5, 2007
- 9,326
- 8,505
Sijasikia huo mchango usharikani kwangu, ukija sitachanga, michango imekuwa mingi mno. Saa hizi sharika zingine haziwezi hata kujiendesha, kila sadaka inayokusanywa 25% inaenda dayosisi, huko dayosisi sijui kuna miradi gani jamani....Leo tuliitwa sehemu tukaambiwa Dayosisi ya mashariki na pwani ina deni la bilion 1.6
Haijulikani ni deni limetokana na nini. Hatukupewa kabisa nafasi ya kuhoji,. Yani imepigwa blaa blaa tu na kuambiwa tuchangie kulipa hilo deni.
Deni limegawanywa kila kituo yani sharika na mitaa, na inatakiwa liwe limelipwa ndani ya miezi 2.
Nmeumia sana kwasababu ni hela nyingi sana na ni mzigo kwa washarika ambao wanajithidi kuinua sehemu zao za kuabudia lakini wanabebeshwa zigo lingine ambalo halijulikani linatokana na nini,
Malasusa mimi nlikuwa nakuunga mkono sana ila kwa hili umenikwaza sana. Unawapa wakati mgumu sana Wainjilisti na wachungaji wako. Hebu fikiria Mwinjilisti au mchungaji anaenda kuwambia washarika tunatakiwa kulipa milioni 10 bila kuambiwa inatokana na nini?
Hapo makao makuu ya Dayosisi napo sijui pana shida gani maana katibu mkuu hajahudumu hata miaka 2 tayari tukasikia nafsi ya katibu mkuu iko wazi.
Mnatukosea sana! Hata kama mnapiga lakini hiyo ni too much.
Donda lingine ni sadaka ya mfuko wa elimu.... sijui ina kazi gqmi ile sadaka manake shule zenyewe sioni hata zikifanya vizuri