anamuunga mkono JK na ni chaguo lake uchaguzi mwakani what is wrong with that?
FMES,
Nothing wrong! nilitaka kujua tu maanake wewe huwa na habari za ndani.. kumbuka tu kuna makundi CCM, na yeye hawezi kuwapatanisha..hivyo leo najua Malecela kajipanga wapi..
- The ishu sio kuwapatanisha kwa sababu wakipatana atakayeumia ni sisi wananchi at large, waendelee kulumbana lakini kuwwe na amani ndani ya chama, ...... Rostam na Mwakyembe walikuwa wanagombea sehemu Singida ya mambo ya umeme, wasingegombana tungejuaje?
Respect!
Malecela angewaacha walumbane ili tujue yote, ya siri na dhahiri, nini kilichomshtua hadi kukimbilia 'kupatanisha'?! Tena so fast?
- Ndio kazi ya wazee wa chama na society, lakini ugomvi haujaisha!
Huo haukuwa ugomvi, ilikuwa ni katika kufichuliana maufisadi yao. Angewaacha wafichuane hadi wenyewe wajipeleke kwa pilato. Anatilisha sana mashaka Malecela kwa kukimbilia eti kupatanisha watu wenye element za ufisadi.
- Alichofanya ni kuwapa ujumbe wanaotaka kuleta vurugu, hawa pia waliwahi kutaka kufanya hizi vurugu mwaka 2000 infact ni wale wale, na sio siri inafahamika wazi kwamba hawana ubavu wa kutoka CCM kwa hiyo jana ametusaidia sana CCM as a chama.
Nilisema jana kuwa Mzee Malecela alikuwa na nia tatu kubwa jana alipoongea ingawa unaweza kuziminya zikawa mbili hivi;
1. Aliwapiga mkwara wanahabari ili waogope kumuandika JK.
2. Aliwapiga mkwara akina Mwandosya ili wasijitokeze 2010 kumpinga JK.
Sidhani kama alifanikiwa katika lolote kati ya hayo kwa sababu Malecela hana ushawishi kama aliokuwa nao Nyerere licha ya umri wake.
Upinzani wa kweli kwa JK sasa hivi uko humo humo ndani ya CCM na ameanza kulielewa hilo na ndio maana akamtuma Malecela kupiga mkwara.
Wanachotakiwa kufanya akina Mwandosya ni kujitokeza mapema ili kujenga umati nyuma yao ndani ya chama na nje ya chama. Ila kama watataka kusubiri mpaka 2010 ili wafanye maajabu ndani ya CC na NEC, basi wamekwisha.
Hawezi kushinda 2010.hana ubavu wowote sio heavy weight.- Eti Malecela hana ubavu lakini toka jana hapa tunalia na press ya Malecela?
- Mkuu unasema Mwandosya anaweza kushinda urais bila msaada wa Malecela are you serious au unatania? Mwandosya anaweza kushinda urais 2010? You got to be kidding me!
Hawezi kushinda 2010.hana ubavu wowote sio heavy weight.
- Strong point mkuu, ubarikiwe! naona hoja zimesha sasa.
FMES!
-Kiongozi wa CCM kama DK. Malecela, anawezaje kuwa neutral? Lini kiongozi wa Democrat aliwahi kuwa neutral kule US?
Unajua wakuu mnaharibu kitu kimoja tu ni kwamba mnashindwa kuwasiaida wananchi wa kawaida na hizi hoja, badala ya kcuhambua what the man said kuhusiana na taifa lao, mimi nimemuelea kwamba yeye ni member wa CCM ameongea kwa faida ya chama chake, na kuonyesha wazi kwamba angetaka Rais wa sasa achaguliwe tena na mimi ninasema ningependa DK. Slaaa apewe next uchaguzi, na wewe sema ungependa nani awe rais next,
Kiongozi wa CCM inatakiwa kuwa neutral na fair kwa wana CCM wenzake wakati wote.
Ni kweli kabisa Mkuu, kwamba kama member wa CCM, mwananchi huru na mtu mwenye hekima na busara, anatarajiwa kutoa maoni yake na ana haki ya kuyatoa maoni hayo wakati anapoona inafaa. Ila kisichoeleweka/kubalika ni yeye kulazimisha wanachama wenzake watambue na kukubali utamaduni kuwa Rais wa nchi (aliechaguliwa na CCM) ni lazima amalize vipindi viwili vya uongozi (wana CCM watake/wasitake). Nadhani hapo tunakubaliana tu kwamba si sahihi kwake kufanya hivyo.
Awali kasema ccm ni chama cha masikini. ni kweli nchi imeubariki umasikini? tunajivunia kuwa nao? Pili kasema kuwa Kikwete hana mpinzani 2010. na wanaojaribu wasahau. inamaanisha ile demokrasia ya miaka mitano mitano kwishnei?
- Ametufundisha kuwa wakweli na wawazi mbele ya jamii, badala ya mambo ya chini chini, sasa tuna demokrasia na tunatakiwa kuwa wakweli na mapema kwa machaguo yetu ya tunaowataka kugombea uongozi wa juu, na sababu..
FMEs!
Date::3/27/2009
Kigogo wa CCM aunga mkono kauli ya Malecela kuhusu Kikwete
Na Leon Bahati
Mwananchi
Fursa ya mwanachama mwingine kuomba nafasi hiyo ipo, lakini kulingana na culture (utamaduni) yetu, tunampa rais kuongoza kwa vipindi viwili, alisema Chiligati ambaye pia ni mbunge wa Manyoni Mashariki, akifafanua:
Hayo ni mazoea na ni culture yetu. Mzee (Ali Hasan) Mwinyi tulimpa nafasi akaongoza kwa miaka 10, Rais (Benjamini) Mkapa naye tukampa nafasi ya miaka 10.
[/B]
[/COLOR]