Malecela avunja ukimya!

Malecela avunja ukimya!

FMES,
anamuunga mkono JK na ni chaguo lake uchaguzi mwakani what is wrong with that?

Nothing wrong! nilitaka kujua tu maanake wewe huwa na habari za ndani.. kumbuka tu kuna makundi CCM, na yeye hawezi kuwapatanisha..hivyo leo najua Malecela kajipanga wapi..
 
FMES,

Nothing wrong! nilitaka kujua tu maanake wewe huwa na habari za ndani.. kumbuka tu kuna makundi CCM, na yeye hawezi kuwapatanisha..hivyo leo najua Malecela kajipanga wapi..

- Alichofanya ni kuwapa ujumbe wanaotaka kuleta vurugu, hawa pia waliwahi kutaka kufanya hizi vurugu mwaka 2000 infact ni wale wale, na sio siri inafahamika wazi kwamba hawana ubavu wa kutoka CCM kwa hiyo jana ametusaidia sana CCM as a chama.

- The ishu sio kuwapatanisha kwa sababu wakipatana atakayeumia ni sisi wananchi at large, waendelee kulumbana lakini kuwwe na amani ndani ya chama, mimi sina tatizo na hilo kwa sababu sasa tunajua kwua Rostam na Mwakyembe walikuwa wanagombea sehemu Singida ya mambo ya umeme, wasingegombana tungejuaje?

Respect!
 
- The ishu sio kuwapatanisha kwa sababu wakipatana atakayeumia ni sisi wananchi at large, waendelee kulumbana lakini kuwwe na amani ndani ya chama, ...... Rostam na Mwakyembe walikuwa wanagombea sehemu Singida ya mambo ya umeme, wasingegombana tungejuaje?

Respect!

Malecela angewaacha walumbane ili tujue yote, ya siri na dhahiri, nini kilichomshtua hadi kukimbilia 'kupatanisha'?! Tena so fast?
 
- Ndio kazi ya wazee wa chama na society, lakini ugomvi haujaisha!

Huo haukuwa ugomvi, ilikuwa ni katika kufichuliana maufisadi yao. Angewaacha wafichuane hadi wenyewe wajipeleke kwa pilato. Anatilisha sana mashaka Malecela kwa kukimbilia eti kupatanisha watu wenye element za ufisadi.
 
- DK. Malecela hawezi kuwapatanisha kwa sababu hawa wana ishus za siku nyingi sana, alichofanya ni kuwatuliza kidogo ili uchaguzi upite kwanza otherwise malumbano ndio kwanza yameanza haya, tutayajua yote soon yaliyojiri na yasiyojiri kumbuka ni el aliyeko nyuma ya yote, kwa sababu the real beef ni kati ya Mwakyembe na el, sio ra.

FMES
 
- Alichofanya ni kuwapa ujumbe wanaotaka kuleta vurugu, hawa pia waliwahi kutaka kufanya hizi vurugu mwaka 2000 infact ni wale wale, na sio siri inafahamika wazi kwamba hawana ubavu wa kutoka CCM kwa hiyo jana ametusaidia sana CCM as a chama.

Nilisema jana kuwa Mzee Malecela alikuwa na nia tatu kubwa jana alipoongea ingawa unaweza kuziminya zikawa mbili hivi;

1. Aliwapiga mkwara wanahabari ili waogope kumuandika JK.
2. Aliwapiga mkwara akina Mwandosya ili wasijitokeze 2010 kumpinga JK.​

Sidhani kama alifanikiwa katika lolote kati ya hayo kwa sababu Malecela hana ushawishi kama aliokuwa nao Nyerere licha ya umri wake.

Upinzani wa kweli kwa JK sasa hivi uko humo humo ndani ya CCM na ameanza kulielewa hilo na ndio maana akamtuma Malecela kupiga mkwara.

Wanachotakiwa kufanya akina Mwandosya ni kujitokeza mapema ili kujenga umati nyuma yao ndani ya chama na nje ya chama. Ila kama watataka kusubiri mpaka 2010 ili wafanye maajabu ndani ya CC na NEC, basi wamekwisha.
 
- Eti Malecela hana ubavu lakini toka jana hapa tunalia na press ya Malecela?

- Mkuu unasema Mwandosya anaweza kushinda urais bila msaada wa Malecela are you serious au unatania? Mwandosya anaweza kushinda urais 2010? You got to be kidding me
!
 
Hawezi kushinda 2010.hana ubavu wowote sio heavy weight.
 
- Strong point mkuu, ubarikiwe! naona hoja zimesha sasa.

FMES!

Mhhh, kama David na Goliati vile. Kama Obama Na Clinton vile. Kama ........ Kuna mtu kaandikiwa awe Marais mwaka 2010 na kama mtu si Kikwete, basi mwakani mtauona ubavu wake na muanze kushangaa, ahhh mbona sisi hatukufikiria hilo. Tatizo kila mtu anafikiri njia zilezile za miaka nenda na miaka rudi. Mtu akiacha uvivu na kukaa usiku na mchana kufikiri nini afanye, basi atakuja/watakuja na njia nzuri ya kufanya na kushinda.

Juu ya Malecela, naona tunazunguka palepale. Wewe unaona sikio la tembo na mie naona mguu wa tembo, ila mwisho wa siku kila mtu kaona tembo (Demokrasia). Unaweza kunifkiri utakavyo. Mzee Malecela kama naweza kusema mabaya yake tena hata mbele yake kwa kutumia MGONGO wa utani wa makabila ni kwamba, aliniangusha kwenye sehemu mbili. Moja kubwa sana ni ile ya USAFIRI. Ya pili ni ile Nyerere alisema (kama ni kweli). Ila kama binadamu ukipima hayo mawili matatu na ukaangalia mangapi kafanya, basi wengi tu Tanzania walie kuja kumfikia. Heri asiiharibu hiyo historia yake. Sasa hivi Tanzania wengi wanaona kinachoendelea.
 
-Kiongozi wa CCM kama DK. Malecela, anawezaje kuwa neutral? Lini kiongozi wa Democrat aliwahi kuwa neutral kule US?

Kiongozi wa CCM inatakiwa kuwa neutral na fair kwa wana CCM wenzake wakati wote.

Unajua wakuu mnaharibu kitu kimoja tu ni kwamba mnashindwa kuwasiaida wananchi wa kawaida na hizi hoja, badala ya kcuhambua what the man said kuhusiana na taifa lao, mimi nimemuelea kwamba yeye ni member wa CCM ameongea kwa faida ya chama chake, na kuonyesha wazi kwamba angetaka Rais wa sasa achaguliwe tena na mimi ninasema ningependa DK. Slaaa apewe next uchaguzi, na wewe sema ungependa nani awe rais next,

Ni kweli kabisa Mkuu, kwamba kama member wa CCM, mwananchi huru na mtu mwenye hekima na busara, anatarajiwa kutoa maoni yake na ana haki ya kuyatoa maoni hayo wakati anapoona inafaa. Ila kisichoeleweka/kubalika ni yeye kulazimisha wanachama wenzake watambue na kukubali utamaduni kuwa Rais wa nchi (aliechaguliwa na CCM) ni lazima amalize vipindi viwili vya uongozi (wana CCM watake/wasitake). Nadhani hapo tunakubaliana tu kwamba si sahihi kwake kufanya hivyo.
 
Kiongozi wa CCM inatakiwa kuwa neutral na fair kwa wana CCM wenzake wakati wote.

Ni kweli kabisa Mkuu, kwamba kama member wa CCM, mwananchi huru na mtu mwenye hekima na busara, anatarajiwa kutoa maoni yake na ana haki ya kuyatoa maoni hayo wakati anapoona inafaa. Ila kisichoeleweka/kubalika ni yeye kulazimisha wanachama wenzake watambue na kukubali utamaduni kuwa Rais wa nchi (aliechaguliwa na CCM) ni lazima amalize vipindi viwili vya uongozi (wana CCM watake/wasitake). Nadhani hapo tunakubaliana tu kwamba si sahihi kwake kufanya hivyo.

- Mkuu amelazimisha akiwa kama nani? mbona mnapenda kukuza maneno hivi, yeye ameongelea chama chake cha CCM na wewe ongelea chama chako cha siasa,

- hii fear inatoka wapi kwa sababu ya maneno ya mzee mmoja tu amabye maepitwa na wakakti, hana akili, ni mzee na balh! baln! sasa vilio vyote hivi ni vya nini kwa sababu ya mzee asiye na lolote kwa taifa?

FMES!

Awali kasema ccm ni chama cha masikini. ni kweli nchi imeubariki umasikini? tunajivunia kuwa nao? Pili kasema kuwa Kikwete hana mpinzani 2010. na wanaojaribu wasahau. inamaanisha ile demokrasia ya miaka mitano mitano kwishnei?
 
..maneno ya Mzee Malecela hayana tofauti na kusema Raisi wa Tanzania ana-serve term moja ya miaka 10.
 
Awali kasema ccm ni chama cha masikini. ni kweli nchi imeubariki umasikini? tunajivunia kuwa nao? Pili kasema kuwa Kikwete hana mpinzani 2010. na wanaojaribu wasahau. inamaanisha ile demokrasia ya miaka mitano mitano kwishnei?

- Ametufundisha kuwa wakweli na wawazi mbele ya jamii, badala ya mambo ya chini chini, sasa tuna demokrasia na tunatakiwa kuwa wakweli na mapema kwa machaguo yetu ya tunaowataka kugombea uongozi wa juu, na sababu.

- Hata chama cha Democrat cha US huwa kinachukuliwa kama chama cha masikini, kwa hiyo sio ajabu kwa CCM kuchukuliwa hivyo.

- Na mimi ninasema hivi anayefaa kuwa rais uchaguzi ujao ni Dr. Slaaa wengine wote wasahau maana hawataweza watasarambatika, kuna tatizo na mawazo yangu haya mkuu?

Wakuu tukubali kwamba sasa Tanzania tuna Democracy, kila mwananchi ana haki ya kusema mawazo yake wazi bila kubughudhiwa.

FMEs!
 
- Ametufundisha kuwa wakweli na wawazi mbele ya jamii, badala ya mambo ya chini chini, sasa tuna demokrasia na tunatakiwa kuwa wakweli na mapema kwa machaguo yetu ya tunaowataka kugombea uongozi wa juu, na sababu..

FMEs!

Big Nooo! Mkuu FMEs
Malecela ametufundisha kuwa WANAFIKI ili mradi ya kwetu binafsi yametunyookea.
  1. Kama Kikwete alipoingia madarakani nchi ilikuwa haina umeme na sasa hivi hali ni mbaya zaidi je hayo ni mafanikio yanayohitaji kuzawadiwa?
  2. Kama Kikwete alipewa ripoti ya Bunge juu ya rushwa ya Richmond lakini hadi leo hajashughulikia madondoo yake, je huu ni utendaji unaohitaji kuzawadiwa mvua 5 nyingine??
  3. Kama hali ya elimu imezidi kuwa mbaya, hospitali hazifai mpaka upelekwe India, SA, UK n.k., vyuo vikuu ndio usiseme, je haya yanahitaji zawadi?
  4. Kama imeshindikana kuwashughulikia wala rushwa wa, EPA, BOT, RadarGate n.k., ambao habari zao zimezagaa kila kona ukiachia hao wachache anaotumia kututengenezea viini macho, je hii sio failure??
  5. Kama mpaka leo nikitaka kwenda Mwanza ni lazima nipitie Kenya, je haya ni maendeleo??
  6. Kama inakuwa nafuu kwa mfanyabiashara wa Tanzania kuingizia mizigo yake bandari za Durban au Mombasa badala ya bandari ya Dar es salaam, je huku ni kwenda mbele au ndio twafa hivyo??
Je, ina maana kwenye milioni 40 ya waTZ au milioni 4 ya wanaCCM hakuna anayeweza kuwa mtendaji bora kuliko alivyotenda Kikwete?

Ingawa namheshimu sana Mzee Malecela, lakini emetudhihirishia wazi kuwa kwake yeye, maslahi binafsi ni bora mara 100% kuliko maslahi ya nchi.
 
Date::3/27/2009
Kigogo wa CCM aunga mkono kauli ya Malecela kuhusu Kikwete

Na Leon Bahati
Mwananchi

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Itikadi na Uenezi, John Chiligati ameunga mkono tamko lililotolewa na mwanasiasa mkongwe ndani ya chama hicho, John Malecela kuwa atakayeomba nafasi ya kuteuliwa kuwa mgombea wa urais mwaka 2010, kumpinga Rais Jakaya Kikwete atakuwa anajisumbua.

Chiligati alisema hayo huku baadhi ya wanachama wa chama hicho wakipinga vikali kauli hiyo, wakiielezea kuwa inakandamiza demokrasia na ni kinyume na katiba ya chama hicho.

Katika mahojiano na gazeti hili jana, Chiligati alisema kuwa pamoja na kwamba katiba ya chama hicho inatoa uhuru wa mwanachama yeyote kugombea, mazoea yaliyojengeka ndani ya chama hicho ni kwamba rais aliyopo madarakani anapaswa kukaa madarakani kwa kipindi cha miaka 10, mfululizo.

Rais Kikwete anatarajia kumaliza kipindi chake cha miaka mitano mwaka ujao na kwa mujibu wa maelezo ya Chiligati pamoja na Malecela, chama kinapasa kumpitisha tena ili amalizie ngwe yake ya mwisho ya miaka mitano mingine.

“Fursa ya mwanachama mwingine kuomba nafasi hiyo ipo, lakini kulingana na ‘culture’ (utamaduni) yetu, tunampa rais kuongoza kwa vipindi viwili,” alisema Chiligati ambaye pia ni mbunge wa Manyoni Mashariki, akifafanua:

“Hayo ni mazoea na ni ‘culture’ yetu. Mzee (Ali Hasan) Mwinyi tulimpa nafasi akaongoza kwa miaka 10, Rais (Benjamini) Mkapa naye tukampa nafasi ya miaka 10.”

Alitetea kauli ya Malecela kwamba alikuwa anaelezea jambo ambalo ni chimbuko la hali halisi iliyojengeka ndani ya CCM na nafasi nzuri ya mwanachama mwenye lengo la kumpinga Rais Kikwete kuwania nafasi hiyo kutafakari kabla ya kufanya uamuzi.

“Mzee (Malecela) alikuwa anaelezea uhalisia kwamba mtu akijaza fomu atakuwa anajisumbua,” alisema Chiligati ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Kwa mujibu wa katiba ya CCM, itakapofika wakati wa uchaguzi, Rais Kikwete sawa na wanachama wengine, atapaswa kwenda kuchukua fomu kuomba nafasi hiyo na kuchambuliwa na vikao mbalimbali ndani ya chama.

Kulingana na maelezo ya Chiligati pamoja na Malecela, wanachama watakaoenda kuchukua fomu sanjari na Rais Kikwete, watakuwa wanapoteza muda kwa sababu hawatapewa nafasi hiyo.

Chiligati alipoulizwa kulikoni utaratibu kama huo ufanyike wakati ambapo inafahamika wazi atakayeteuliwa kwenye nafasi hiyo, alisema taratibu zote zitafanyika kwa haki lakini ni wazi kwamba Mungu amempa binadamu busara ya kupima mambo, hivyo ni juu ya kila mwanachama kutafakari kila jambo kwa makini.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi nyumbani kwake Sea View, Malecela aliwataka wanachama wa CCM kutojisumbua kuomba kuteuliwa kugombea nafasi hiyo ya rais kwa sababu wataambulia patupu.

Hata hivyo, mmoja wa makada wa CCM aliyewahi kutamka hadharani kuwa ataomba nafasi hiyo, John Shibuda, Mbunge wa Maswa, alisema kauli iliyotolewa na Malecela haijabadili nia yake.

“Mimi siwezi kugombana na watu kwa suala ambalo liko wazi kikatiba,” alisema Shibuda akifafanua kuwa alichosema Malecela ni maoni yake na wala yasiwakatishe tamaa wanachama wa CCM wanaokusudia kuomba nafasi ya kuteuliwa kuwa mgombea wa rais kupitia chama hicho tawala.

“Kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni yake. Lakini mimi naangalia katiba (ya CCM) inasemaje. Katiba ndiyo inayotuongoza. Naomba wanachama wenye lengo la kuomba kuteuliwa wagombea wanafasi hiyo, wajitokeze, wasikatishwe tama na maoni hayo,” alishauri Shibuda.

Ingawa namheshimu sana Mzee Malecela, lakini emetudhihirishia wazi kuwa kwake yeye, maslahi binafsi ni bora mara 100% kuliko maslahi ya nchi. [/SIZE][/B][/COLOR][/QUOTE]

Nashauri tuyataje maslahi binafsi ya Malecela katika safu hii, na mimi naanza:

-JK alimteua kuwa mjumbe wa kudumu katika CC bila ridhaa ya chama ili kumpangusa machozi ya kukosa urais. Kawaida Makamu angekuwa mjumbe NEC ingetosha.
-JK alikubali ushauri wa Melecela kumgeuka Lowassa na kumtapeli. Awali walikubaliana aandike barua ya kujiuzuru lakini sisikubaliwe. Kwa ushauri wa Malecela, JK akaikubali.
-Wabaya wa Malecela katika mtandao wanashughulikiwa na JK, kwa hiyo mzee huyo anachekelea.
-JK kufuata ushauri wa Malecela unamharibia mambo ndani ya chama. Yakiharibika, Malecela anacheka pia na kutumabia yeye ndiye angefaa na siyo JK. Wengine ongezea.
 
Date::3/27/2009
Kigogo wa CCM aunga mkono kauli ya Malecela kuhusu Kikwete

Na Leon Bahati
Mwananchi

“Fursa ya mwanachama mwingine kuomba nafasi hiyo ipo, lakini kulingana na ‘culture’ (utamaduni) yetu, tunampa rais kuongoza kwa vipindi viwili,” alisema Chiligati ambaye pia ni mbunge wa Manyoni Mashariki, akifafanua:

“Hayo ni mazoea na ni ‘culture’ yetu. Mzee (Ali Hasan) Mwinyi tulimpa nafasi akaongoza kwa miaka 10, Rais (Benjamini) Mkapa naye tukampa nafasi ya miaka 10.”

[/B]
[/COLOR]

Hawa kweli wamefilisika kisiasa. Hawana lolote la kuongea kuhusu ni kipi alichofanya Kikwete kama Rais wa Tanzania ambacho kinastahili kumpa tena nafasi ya kupewa tena awamu nyingine. Wamekalia kutoa kauli ya 'utamaduni wetu' tu!!!!! 🙁 Huu utamaduni wa ndani ya CCM hausaidii nchi yetu hasa pale Rais aliyekuwa madarakani anaonyesha dhahiri kwamba hana uwezo wa kuiongoza nchi. Utamaduni huu umepitwa na wakati na kuna kila sababu ya kuupiga vita kwa nguvu zetu zote.
 
Back
Top Bottom