Malengo hasa ya kuzaa watoto wengi ni nini?

Malengo hasa ya kuzaa watoto wengi ni nini?

Kwa maisha ya sasa sioni kama kuna tija ya kuzaa watoto wengi ni bora watoto wachache ambao utaweza kuwapatia mahitaji yao ya msingi, chakula, malazi, mavazi, furaha na elimu bora.

Mbaya zaidi unakuta mtu ana watoto wengi ambapo yeye anateseka na watoto pia wanateseka kwa kukosa mahitaji yao msingi.

Unakuta mstaafu ana watoto watu wazima na familia zao ila bado yeye anaendelea kuzaa tu.

Ushauri zaa kiasi upate muda na fedha za wewe kujinafasi na mkeo.


Bwashee, kila mtu si anaishi anavyojua au? Mie nina watoto 3 tu, ingawa sielewi kwa nini mtu anakuwa na watoto wengi, siwezi wahukumu maana ni maisha yao.
 
Watoto wengi wana raha fulani ila wanatia umasikini! Mimi ninao wanne nachofanya ni tunakula na wanaenda shule basi! Hakuna cha kula bata sijui outings....lakini Kila nikirudi nyumbani nafill kama mtu fulani wa maana wakianza kudai hiki au kile.

Pamoja na kuwa nao wanne kuna mmoja niliyemzaa kabla ya kuoa napambana nimchukue!
 
Back
Top Bottom