Malengo hasa ya kuzaa watoto wengi ni nini?

Kwa maisha ya sasa sioni kama kuna tija ya kuzaa watoto wengi ni bora watoto wachache ambao utaweza kuwapatia mahitaji yao ya msingi, chakula, malazi, mavazi, furaha na elimu bora.

Mbaya zaidi unakuta mtu ana watoto wengi ambapo yeye anateseka na watoto pia wanateseka kwa kukosa mahitaji yao msingi.

Unakuta mstaafu ana watoto watu wazima na familia zao ila bado yeye anaendelea kuzaa tu.

Ushauri zaa kiasi upate muda na fedha za wewe kujinafasi na mkeo.
Elimu Bora ndiyo ipi? Kwa namna moja ama nyingine utakua unamaanisha zile elimu za watoto wanao ongea ki-English siyo? Naamini hivyo na pole sana
 
"Emu liangalie linatumbua mimacho tu kuwachungulia wakubwa, toto gani lina tabia chafu hivi"..

Kumbe shida sio mtoto ila uamuzi wako wa kuzaa watoto watatu katika maisha ya chumba kimoja . Mkianza purukushani za usiku watoto wanashtuka
 
😂😂😂😂
 
Ndugu elewa kwamba jamii zetu nyingi zimetokea Mashambani kwa wakulima na wafungaji hivyo ili uwe na mali hauna budi ujikite kwenye kilimo sana na ufungaji kipindi msimu wa kilimo ukifika hivyo unaitaji nguvu kazi ya kulima na kuchunga mifugo

Hapo ndio dhana ya kuzaa watoto wengi ilikuja ili wazazi wapate vijana wa kuchunga ng'ombe na kufanya kazi za mashambani kwa gharama ndogo sana

Tujiulize wewe upo mjini unazaa watoto wengi wanakupa faida ipi mjini hakuna mashamba hakuna mapori yakuchungia

Kijijini mtoto wa miaka kumi na mbili ana tija kwenye familia ila mjini ni mzigo kwenye familia maana atachunga mifugo, au kufanya kazi za mashambani kama parizi nk
Huo ndio ukweli, mjini kuwa na watoto wengi ni anasa
 
Elimu Bora ndiyo ipi? Kwa namna moja ama nyingine utakua unamaanisha zile elimu za watoto wanao ongea ki-English siyo? Naamini hivyo na pole sana
pole sana wewe endelea kulala, mwanao wa elimu ya msingi hii ya sogea tukae unathubutu kulinganisha na elimu ya mtoto anaelipiwa zaidi ya milioni tatu kwa mwaka!!

Ukweli ni kwamba hakuna mzazi asiyependa mtoto wake asipate elimu hiyo unayoita ki- English!!
Mchawi hapa ni umasikini tu😃
 
Kwa maisha ya sasa sioni kama kuna tija ya kuzaa watoto wengi ni bora watoto wachache ambao utaweza kuwapatia mahitaji yao ya msingi, chakula, malazi, mavazi, furaha na elimu bora.

Mbaya zaidi unakuta mtu ana watoto wengi ambapo yeye anateseka na watoto pia wanateseka kwa kukosa mahitaji yao msingi.

Unakuta mstaafu ana watoto watu wazima na familia zao ila bado yeye anaendelea kuzaa tu.

Ushauri zaa kiasi upate muda na fedha za wewe kujinafasi na mkeo.
Daaa mm nina watoto 2 and nlitaman hata 10 inanikosesha furaha sana.
 
pole sana wewe endelea kulala, mwanao wa elimu ya msingi hii ya sogea tukae unathubutu kulinganisha na elimu ya mtoto anaelipiwa zaidi ya milioni tatu kwa mwaka!!

Ukweli ni kwamba hakuna mzazi asiyependa mtoto wake asipate elimu hiyo unayoita ki- English!!
Mchawi hapa ni umasikini tu[emoji2]
Ninafanya kazi ofc kubwa sana hapa nchini, na wote wenye akili mingi ndani yake wanao leta matokeo makubwa ni walio soma Kayumba, na wenye mbwembwe na wanaiba kila siku na kufukuzwa ni hao unao watengeneza na wewe nyumbani kwako ambao huku ofisini hawana uwezo wowote wa kazi zaidi ya kunyoosha ki English kwenye hamna, kaa kwenye ujinga, watoto wakuozee ndani na nje
 
binafsi sipendi wanangu waje kuteseka hivyo basi watoto wawili tu watanifaa
 
Mmetoka kwenye kukataa kuoa mmehamia huku haya msije kuchukia tu mwisho wa siku wasukuma na wapemba wakiwa wengi maana mpaka sasa hakuna waliowapiku hao!
 
Ndugu elewa kwamba jamii zetu nyingi zimetokea Mashambani kwa wakulima na wafungaji hivyo ili uwe na mali hauna budi ujikite kwenye kilimo sana na ufungaji kipindi msimu wa kilimo ukifika hivyo unaitaji nguvu kazi ya kulima na kuchunga mifugo

Hapo ndio dhana ya kuzaa watoto wengi ilikuja ili wazazi wapate vijana wa kuchunga ng'ombe na kufanya kazi za mashambani kwa gharama ndogo sana

Tujiulize wewe upo mjini unazaa watoto wengi wanakupa faida ipi mjini hakuna mashamba hakuna mapori yakuchungia

Kijijini mtoto wa miaka kumi na mbili ana tija kwenye familia ila mjini ni mzigo kwenye familia maana atachunga mifugo, au kufanya kazi za mashambani kama parizi nk
Nakazia
 
kama si watoto 30 basi mimi nisingekuwepo.

Wanawake wanne Jumla, baba alikuwa ni jembe kwa kweli
Kuna mzee mwenzangu kafariki mwezi uliopita kaacha watoto 56 kwa kina mama 7
Mimi vitoto 6 tu eti nami najiona nina watoto wengi
 
Unaweza kudhaa wawili, na wakafa wote ukajikuta na umri wa kuzaa umepita , dharula la ukubwani
 
Back
Top Bottom