Malengo ya Mbio za Mwenge yabadilishwa, Sasa hivi wanauzungusha tu na kufanya Matamasha

Wale wa mkwaja,kipumbwi,sakura,mikocheni,mwera,ushongo,bweni,bomani,mnyongeni,sokoni,boza,kigombe mpaka Kilale wamekula burudani bure. Usiku wakipigiwa na taarabu kijamvi basi ubovu na mashimo ya stand wanasahau
 
Hivi mwenge kwenda Pangani umemfuata Aweso au Wananchi ? yaani viongozi wa ccm wanajidanganya sana , aweso anadhani ule mwenge umemfuata yeye na familia yake .
 
Aweso anapiga kazi vizuri.
Hata hivyo, kwa ujumla wake, wanasiasa ni walaji (consumers) ambao hula kodi za wananchi (kwa sababu siyo wazalishaji, yaani producers kwenye jamii au taifa).
Ili tupate maendeleo endelevu, kodi zetu zinatakiwa zielekezwe kwa wazalishaji (wakulima, wafugaji, watoa huduma na wenye viwanda), walaji wanunue kwao au hata nje ya nchi. Tutapata walaji wengine kutoka nje ambao watatuletea utajiri.
Kosa kubwa tunalofanya ni kutumia kodi zetu kutengeneza walaji wakati uzalishaji wetu ni mdogo.
Tunatakiwa tuzalishe sana na walaji wa nje waje watuletee pesa (utajiri) ili taifa kwa ujumla wake liwe tajiri.
Kwa hiyo, wanasiasa wetu tuwalipe kidogo ili watu wengi wakimbilie kwenye uzalishaji badala ya ulaji.
 
Lengo ilikua nini mimi sijafahamu?
 
Halafu kauli mbiu ilikuwa iwe; "pigana kutokomeza rushwa"
Baadae dhamira ikawasuta wakachomoa hii kauli mbiu! 🤣 🤣
 
Hahaha. Mwenge wa uhuru hauna maana tena. Ni Ama tuuzime au turejee maandiko yake? Nani anaweza kuyaghani maandiko ya mwenge wa UHURU hadhaŕani hapo LUMUMBA? Dodoma bungeni au chamwino? Kizimkazi je wanaweza kughani maandiko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…