HATUA SABA ZA KUACHA KUVUTA SIGARA.
1. Elewa kwamba kuvuta sigara ni dhambi dhidi ya mwili wako na Mungu wako.
"Basi ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana." (Rumi 12:1).
"Wala ninyi si mali yenu wenyewe; Maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu." (1 Kor 6:19,20).
2. Kiri kwamba wewe ni mdhaifu na huwezi kuacha mwenyewe. Inawezekana umetafuta msaada kwa miaka mingi kama yule mwanamke aliyekuwa "akitokwa damu", au kama yule mtu aliyekuwa kando ya Birika la Bethzatha kwa miaka 38, inawezekana umehangaika sana ukijaribu kuacha kuvuta sigara (soma Yohana 5:5-8). Kubali kwamba wewe ni dhaifu. Kiri kwamba huwezi kufanikiwa wewe mwenyewe. "Pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote." (Yohana 15:5).
3. Amini kwamba japokuwa u mdhaifu, Yeye ana nguvu. Japokuwa huwezi, yeye ana uweza wote. Tunapoamua kuweka makusudi yetu dhaifu, yenye kusitasita chini ya makusudi yake yenye uweza wote, uwezo wote uliomo ulimwenguni utakuwa wetu (Flp. 4:13; 1 Yoh. 5:14,15).
4. Jitoe kwa Mungu pamoja na sigara zako zote ( Yos. 24:15; 2 Kor. 6:2).
5. Amini kwamba, sasa ushindi ni wako, kisha mshukuru Mungu sasa hivi kwa kukupa ushindi dhidi ya kuvuta sigara (1 Kor. 15:57; Mt. 7:7; 1 Yoh. 5:4). Unaweza kuwa na hamu ya sigara, kama matokeo ya athari za nikotini iliyobaki katika mfumo wa chembe chembe za mwili wako. Lakini si lazima uvute. Kuvuta ni suala la uamuzi. Kuna tofauti kati ya hamu na ushindi. Ushindi ni wako kwa njia ya imani katika Yesu Kristo.
6. Haribu sigara zako zote. Zitupe. Usibakize hata kidogo mahali ulipo. Jitoe kwa Mungu na umpinge Shetani (Yak. 4:7,8).
7. Amini kwamba sasa ushindi ni wako. Kudumisha ushindi huo, mshukuru Mungu kwa ajili ya ushindi huo! Msifu kwa kuwa umekombolewa, kisha fuata kanuni zilizoorodheshwa hapa chini ili kuiondoa nikotini mwilini mwako.
- Unapokuwa na hamu ya kuvuta sigara, vuta pumzi taratibu kwa kina hadi hamu inapokwisha.
- Kunywa bilauri 10 hadi 12 za maji kila siku kwa siku tano mfululizo.
- Pumzika kwenye maji ya uvuguvugu katika bafu kabla ya kulala.
- Panga kulala kwa saa zisiyopungua nane kila siku.
- Epuka kutumia kahawa na pombe.
- Fanya mazoezi ya kutembea kwa dakika 30 mara mbili kila siku.
Endelea kumsifu Mungu kwamba uweza wake ni mkubwa kuliko sigara (1 Yohana 4:4).
Nimekuletea mada hii muhimu ya kushinda kuvuta sigara mada nyingine ya pombe nenda fb ingia kwa majina Sospeter Magobo utajifunza mada nyingi zilizomo humo.
Mungu Akubariki wewe na wengine wote wanaotaka kushinda kutoka kwenye uraibu wa sigara, pombe, umalaya na kubet.