Sinywi pombe, sitembei na malaya, sibet wala sivuti sigara, unataka kuniambia sijakamilisha maisha? Tuache kutukuza haya mambo bhana.
Ulevi, umalaya na kubet kunaharibu maisha ya vijana wengi sana sasa hivi, wanatumikishwa bila kujijua. Jana kuna kijana kaja ofisini akanambia amekunywa dawa fulani saa tano asubuhi, anaweza kunywa pombe? Aliponitajia jina la dawa nikamwambia asubiri mpaka masaa 48 yapite akafadhaika sana, baada ya nusu saa akarudi anataka kujua madhara akiamua kunywa tu, nikamwambia kama umechoka kuishi kanywe.
Acheni umalaya
Acheni kubet
Acheni pombe
Hazina faida kwenu zaidi ya kuwatia hasara tu.