Sijui ni lini ngozi nyeusi tutarudi kuwa na nguvu hivi maana rasilimali zote tunazo na nguvu kazi tunazo ila kuna eneo tulipwaya hadi kuacha mwanya kwa hawa wazungu kutuburuza mpaka leo ila naamini ni jambo la wakati tu tukijitambua na kurudi katika misingi yetu ya asili bila ya kuendeshwa na western mentality and leadership style pamoja na kuungana tutarudi tunapotakiwa kuwa
Unapozungumzia matatizo ya mtu mweusi huwezi kabisa kuacha madhara ya dini za Wazungu na Waarabu.
Waislamu na Wakristo ni moja ya sababu kubwa sana kwenye matatizo ya Afrika lakini huwa tunawaacha nje na kukazania Biashara ya Utumwa na Ukoloni pekee. Ili kuelewa vizuri historia ni lazima uweka kila kitu mezani na uanze kuchambua kitu kimoja baada ya kingine. Waislamu wenye asili ya Kiarabu walivamia Afrika mnamo karne ya saba (7) na kuanza kueneza dini kwa makali ya upanga; watu weusi wengi walikufa kwa makali ya upanga na tamaduni za Kiafrika nyingi sana zilipotea. Leo hii ukienda nchi za Maghreb unakuta waarabu tu na wengine wanajitanabaisha kwamba wao ndiyo waliojenga mapiramidi ya Misri na kuiletea dunia yetu mbinu za Kilimo na umwagiliaji , Ujenzi, Utabibu, Hesabu, Utengenezaji wa meli na Ubaharia. Mwanahistoria wa Kigiriki
Herodotus anasema kwamba Mafarao walikuwa wanajua sana kufanya safari za baharini kwa namna ambayo hajawahi kuona.
Wengine ni Wakristo wa Ulaya.
Ambao wao waliona njia nyepesi kabisa ya kutawaala mtu ni kutumia imani. Maana baada ya dola la mrumi kuanguka mnao karne ya nne: Dunia nzima ilishuhudia ulaya ikiingia katika kipindi cha
The Dark Age, ambapo kulikuwa hakuna maendeleo makubwa sana na Kanisa ndiyo lilikuwa limeshika hatamu. Mpaka kuifikia Mkatabwa wa
Westphalia 1648 hadi karne ya
18 hadi
19 (The Renaissance) watu waliopanza kutumia akili zao kufikiria na kuanza kujitenga na uongo wa kidini ndipo Ulaya ikapiga hatua kubwa sana kwenye viwanda na mwishowe kutawala dunia nzima. Wazungu walikuja na mbinu zilezile zilizotumiwa na Kanisa Katoliki kutawala Ulaya kipindi chote cha The Dark Ages, wakaleta dini kwa nguvu kwa mwafrika. Wakasema majina na tamaduni zenu ni za kishenzi , wakaleta hadi na sala maalumu kwa ajili ya washenzi wote wa Afrika. Sasa lile giza la Ulaya la kutokea Karne ya 4 hadi 18 likahamia Afrika na ndiyo Bara letu likaitwa
The DARK CONTINENT.
Lakini leo hii wasomi wa Afrika walioko kwenye dini haya hawayaoni na wanarusha makombora kwa mzungu tu na kuacha dini zao pembeni. Trans-Atlantic Slave Trade ilifanywa na Waarabu wa Wafalme wa Kiislamu waliokuwa wanavamia jamii za kishenzi (Makafiri) na kuanza kuwauza kwa wazungu hasahasa Wafanyabiashara kutoka Uholanzi. Afrika ilipoteza nguvu kazi kubwa sana na rasilimali nyingi na mwishowe ikavaa tamaduni zisizokuwa za kwake. Hili ni tatizo kubwa sana kwa Afrika, leo hii mwafrika akiishi kama Muitalia, Marekani, Myahudi au Muarabu anasema ndiyo anafuata dini.
Kuna mambo mengi sana ambayo tunayafuata kwenye dini lakini kiukweli siyo mafundisho ya Kiroho bali ni tamaduni za Waitalia au Waarabu. Kama kuvaa kanzu kulikuwepo hata kabla Mtume hajazaliwa, hivyo siyo dini bali ni sehemu ya tamaduni ambayo imevaana na dini. Makanisa ya Kiafrika kuanzia yale ya waorthodoksi wa Abyssinia yalikuwa tofauti kabisa na makanisa ya kiroho ya leo hii ambayo yana masharti lukuki ambayo mimi sijawahi kuyaelewa hata siku moja.
NB: Mtu mweusi asipojifunza kutenga uongo wa mapokeo ya kidini na ukweli wake binafsi, ataishi miaka yake yote akiamini kwamba Wayahudi, Wazungu na Waarabu wako bora kuliko yeye na ndivyo maulana alivyoumba hii dunia. Ataridhika na kubweteka na kuamini tamaduni zake ni ushenzi kama ilivyo hii leo. Ndiyo maana Uchina na Korea baada ya vita ya pili ya dunia mwaka 1945 waliamua kuchoma moto kila aina ya upuuzi wa kijapan na wazungu na kupiga marufuku kabisa mafundisho ya kipuuzi ambayo yanahubiri kwamba kuna jamii fulani ni bora kuliko nyingine.
Tuna safari ndefu sana kufika tunakotakiwa kwasababu mpaka sana sisi hatujui hata tunakoenda.....
Ila hizi Dini za Mzungu na Mwarabu zimechangia sana kudumaa akili mtu mweusi......