Malkia Elizabeth kalala kuzimu. Je, karma itachukua mkondo wake?

Unajuaje?. Vipi kuhusu Ben wetu?. Kwa vile mwisho wa siku wote lazima tuu tutakufa siku yetu ikifika, unawezaje kutofaitisha kifo cha laana ya karma na natural death?.
P
Nature death ni kifo chema kifo cha utulivu na kifo cha laaana ni kifo cha hatia
 
Maoni yangu Malkia yote aliyofanya alifanya kwa ajili ya watu wake kwa maana kwamba ni mzalendo wa nchi yake kupitiliza "utawapaje mbwa chakula cha watoto? Kiukweli hata sisi hayatuhusu ila tunajikuta mengi tunayasikia na kuyasoma !

Na formula ya ulimwengu ni ngumu kufanikiwa bila kumuumiza mwingine 😀😀 kwa hiyo haya ya waafrika walipigwa , wahindi wakalala njaa , South Africa wakaibiwa Dhahabu ! Ilikua ni kwa ajili ya Nchi yake ! Mtakumbuka hata hao wana wa israel walichokifanya mpaka kuipata kanaani watu waliumizwa sana !! Humo njiani na nchi haikua yao

Kiukweli nyakati zile ukishakua born town , unatafuta mshamba unamkamua hata sisi Africa tungetangulia tungewaliza vibaya mno , halafu walivyoona mambo yanabadilika wakaamua kuleta demokrasia.

Kwa issue ya Diana ni mambo yapo Mama mkwe na mkamwana japo hatufikagi huko kwenye kutoana roho !!

Msishangae bibi tukamkuta mbinguni ana taji na kakaa kwenye kiti cha dhahabu wadau 😀
 
Hawaji wanajua. Church of england ambae malkia ndie mkuu wao ni Kanisa la mashoga
Kwahiyo haya makanisa ya anglicana tunayoyaona waumini wake ni mashoga ok nilikua sijui
 
Refer karma kwenye Bible ... Nami nawapatiza wana maovu ya baba zao wa kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukizao
Huu ni uonevu mkubwa sana ,kama ndio Mungu yuko hivyo anatakua na ukatili wa kipumbavu ,yani umuumize mtoto mdogo kisa babu yake wa 4 huko alifanya kosa
 
Alifanyaje mkuu ,nimeona umemlundikia lawama lukuki lakini hujataja hata jambo moja alilofanya
 
Huu ni uonevu mkubwa sana ,kama ndio Mungu yuko hivyo anatakua na ukatili wa kipumbavu ,yani umuumize mtoto mdogo kisa babu yake wa 4 huko alifanya kosa
Hapana nadhani kuna kitu hujakielewa kuna heredity issues hapo, DNA kizalia nk
 
Wakuu Kamanda Moshi na Songambele nimerudi tena baada ya kusoma michango yenu na kutoka vyanzo vingine vya habari... Kuna mijadala mingi huko kwingine ama ya kumtetea ama kumhusisha malkia Elizabeth na biashara ya utumwa na udhalimu mwingine uliotendwa na taifa lake

Niliahidi kuomba radhi kama ikithibitika nimepotoka,,, sasa kwa sehemu naomba radhi na si kwa ujumla wake kwakuwa nilichokuja kuona ni kwamba pamoja na jitihada zake za kukomesha biashara ya utumwa lakini kuna mengi alishindwa kuyapigania pengine Kutokana na nafasi yake
1. Alishindwa kukataa kuvaa kofia ya kimalkia inayotuhumiwa kutengenezwa na vipande vya madini mbalimbali yaliyoporwa toka Afrika.. Na hapa isingewezekana akatae

2. Maisha ya pepo/bata ndani ya kasri la kifalme/kimalkia pamoja na ukwasi mkubwa waliokuwa nao kwa sehemu kubwa havitokani na jitihada binafsi nchini mwao bali kutokana na uporaji mkubwa ulliofanywa Afrika kipindi chote kabla na baada ya yeye kuwa malkia

3. Kuna udhalimu ndani ya 'royal family' lazima ufanyike ili kuilinda damu na kizazi chao na hili halikwepeki popote duniani na pengine kwa yoyote ule.. Kwenye hili tuhuma ni nyingi pia

4. Inawezekana kabisa nia yake ilikuwa thabiti lakini uwezo wa kutoa maamuzi alikuwa hana, hivyo kujikuta anakuwa sehemu ya kila baya taifa lake lililotuhumiwa kwalo
 
mie nilitaka urekebishe pale kuhusu India lakini utajiri wake si kweli kama umetoka Afrika, ukumbuke India, Ulaya na Amerika pia kuna madini kwa hiyo vito wenzetu waligundua miaka mingi saana kabla ya kuja Afrika. Ni kweli wanamapungufu yao lakini tusiwasingizie yale yasiyo ya kwao. Ukiangalia budget ya Tanzania kipindi kile 60% inatoka ulaya mwingereza ndiye aliyechangia kwa kiasi kikubwa kuliko nchi yeyote. Angalia biashara kabla enzi za Magu tulifanya biashara zaidi na uingereza kuliko yeyote.

Mshana kwanza mkubwa timiza ahadi yako ya kuomba radhi bila masharti yeyote na kutengeneza shutuma mpya. Ufalme karne iliyopita ulikuwa balaa lakini huyu mama kautia greece mno na tumeishi nao, kwa muda wake wafalme woote wanabadilika sasa, India kulikuwa na falme kibao waingereza walifuta zote na kusimamisha taarifa zao.

Changamoto za kibinadamu hawawezi kosa bhana.
 
Naomba radhi bila masharti yoyote Songambele nadhani hii sasa nitakuwa nimetimiza ahadi .. Zaidi tuendelee kuchimbua ukweli na uongo kwenye sakata zima la malkia mwendazake
 
Ile kofia yake ina madini yenye thamani ya Tsh billion moja na yaliporwa South Africa
Mkuu kuna moja inaitwa Kohinoor ilichimbwa India na akapewa Malkia
Na ndio iko kwenye kofia moja ya Malikia na ni kubwa sana
Hebu isome kidogo hiyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…