KERO Malori yanayoegesha barabarani Ubungo Maziwa kuelekea Kigogo ni kero kubwa

KERO Malori yanayoegesha barabarani Ubungo Maziwa kuelekea Kigogo ni kero kubwa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
WhatsApp Image 2026-10-15 at 17.42.09.jpeg

Kwa masikitiko makubwa, napenda kuwasilisha kilio cha wananchi kuhusu hali inayoendelea katika Barabara ya Ubungo Maziwa kuelekea Kigogo, ambapo malori makubwa yamekuwa yakipaki kandokando na hata sehemu ya barabara kwa muda mrefu, hali inayosababisha msongamano mkubwa wa magari, usumbufu kwa watumiaji wa vyombo vya moto, pamoja na kuhatarisha usalama wa watembea kwa miguu.

Kinachoumiza zaidi ni kuona sheria zikionekana kutumika kwa baadhi ya watu na kupuuzwa kwa wengine. Sio muda mrefu umepita tangu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mheshimiwa Albert Chalamila, atoe maelekezo na tahadhari kali kuhusu marufuku ya kupaki magari au vyombo vya moto kwenye barabara na maeneo yasiyoruhusiwa. Hata hivyo, hali inayoendelea katika eneo hili inaonekana kwenda kinyume kabisa na maelekezo hayo.

Wananchi tunajiuliza: Hali hii itaendelea mpaka lini? Kwa nini hatua stahiki hazichukuliwi wakati kero hii iko wazi na inaonekana kila siku?
WhatsApp Image 2026-10-15 at 17.42.23.jpeg

Barabara hizi zimejengwa kwa fedha za walipa kodi. Hivyo, si haki kuona wananchi wakinyimwa matumizi huru ya miundombinu yao kutokana na maslahi ya watu wachache. Tayari tunakabiliana na changamoto nyingi za maisha; kuongeza mateso ya foleni zisizo za lazima na hatari za ajali si jambo la kukubalika.

Tunaziomba mamlaka husika, ikiwemo Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, TARURA, TANROADS na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, kuchukua hatua za haraka na za kudumu ili kurejesha utaratibu katika eneo hili.

Wananchi tunahitaji kuona sheria zikisimamiwa kwa usawa bila upendeleo, kwa manufaa ya usalama na ustawi wa wote.
 
Back
Top Bottom