Malori zaidi ya 100 Himo yenye shehena ya mahindi yaamuriwa kuuza mahindi yao nchini badala ya kuyasafirisha Kenya

Malori zaidi ya 100 Himo yenye shehena ya mahindi yaamuriwa kuuza mahindi yao nchini badala ya kuyasafirisha Kenya

Malaro zaidi ya 100 kila Lori lina gunia 1000 aiseeee unaweza sababisha inflation.
 
Amri hiyo imetolewa na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Bw. Nurdin Babu kwa maelekezo ya Waziri wa Kilimo Bw. Bashe.

Bila shaka amri hii inatokana na zuio la Rais Samia kuzuia kuuza chakula nje ya nchi ili kukabiliana na upungufu wa chakula nchini na duniani kwa jumla.

Hoja hapa kwa nini serikali haikuwataarifu wafanyabiashara mapema ili kuwaepusha na hasara watakayopata kwa sababu ya gharama za usafiri? Kwa nini malori yaliyofika hapo Himo kabla ya zuio la Rais yasiruhusiwe kuendelea na safari?

Moja ya athari ya zuio hili ni kuwa bei ya mahindi itaporomoka sana kwa wakulima kutoka zaidi ya Shs. 800/= kwa kilo kwa sasa hadi kuwa chini ya Shs. 500/= kwa kilo!
Huo ni ujinga.

Anunue yeye mkuu wa mkoa au awalete wanunuzi kwa hao wafanyabiashara wa mahindi wayanunue mahindi yote.
 
Hii issue lazima italeta mgogoro kati ya Kenya na Tanzania, sababu wafanya biashara wa Kenya tayari walikua wamesha nunua mahindi kwaajili ya kupeleka kwao kabla ya kauli ya bi mkubwa.
Nafikiri hapa ilitakiwa busara ya kawaida itumike ili kutatua hili jambo na baada ya hapi basi amri ya mama ndipo iendelee kutekelezwa.
Kwenye suala la chakula hasa mahindi na mpunga busara ni kuzuia tu!
 
Mahindi hayapaswi kuzidi elfu 50 kwa gunia, mimi nalima na gharamaza za uzalishaji kwa gunia moja ni elfu 30 mpaka 35 ikizidi sana 40 sasa unakuja kuuza gunia laki hiyo si ni kumkufuru Mungu muumba mbingu na nchi?
Halafu unayasafirisha kwa nguvu za Mungu Muumba Mbingu na Nchi kutoka shambani hadi sokoni!
 
Hizo siyo akili bali kuwaumiza wakulima. Ruzuku yenyewe inatolewa kwa spana!

Chakula ni sehemu ya Usalama wa Taifa. Kwa namna yoyote haipaswi kufanyiwa mizaha.

Waongeze ruzuku kwa wakulima, mbolea irudi 35k kwa kilo 50, wajihalalishie makatazo yao ya kuzuia chakula.
 
Mahindi hayapaswi kuzidi elfu 50 kwa gunia, mimi nalima na gharamaza za uzalishaji kwa gunia moja ni elfu 30 mpaka 35 ikizidi sana 40 sasa unakuja kuuza gunia laki hiyo si ni kumkufuru Mungu muumba mbingu na nchi?
Kila gunia unapata faida ya elfu 10 baada ya miezi sita kuja kuvuna sishangai nchi yetu kila mtu amegeukia uchuuzi
 
Mahindi hayapaswi kuzidi elfu 50 kwa gunia, mimi nalima na gharamaza za uzalishaji kwa gunia moja ni elfu 30 mpaka 35 ikizidi sana 40 sasa unakuja kuuza gunia laki hiyo si ni kumkufuru Mungu muumba mbingu na nchi?
Umepigia gharama za usafirishaji na vibarua?? Au mwenzetu we mwanga mchawi?

Sent from my TECNO CI6 using JamiiForums mobile app
 
Serikali yenu Haina sera zinazotabirika kwenye Kilimo,Bashe alisema Serikali ikiwazuia Wananchi kuuza Nje atawajibika Kisiasa Hadi Sasa Yuko kimya..

Kumbukeni mwaka Jana wakati chakula kina bei mlikuwa mnamtukana Rais ndio kaamua acheze ngoma yenu.
Bashe Ni mnafiki mxur
 
Acha yazuiwe, kwanini mahindi yauzwe nje ya nchi wakati kuna uhaba wa chakula hapa nchini tayari.

Kama wanapata hasara inabidi Serikali iyanunue kwa hiyo bei wanayotaka wao ili tu yabaki TANZANIA
Ponit Kam laki 159 serekali iko tayar kununua
 
Tuliwaambia Tangu February zuieni chakula kwenda nje, tukaambiwa Sisi siyo wakulima tunaishi mjini. Mimi mjini huwa nakwenda kuhudhuria semina za waandishi tu. Nakaa ushambani kwenye Baridi la nyanda za juu. Najua wanaofaidika na bei si wakulima na watukati.
Walanguzi wanapofaidika na wakulima nao wanafaidika gunia kutoka elfu 40 hadi 80 ni mafanikio shambani mazao yakishuka watu watalima wachache na kufanya bei iendelee kuwa juu watu wanaoishi mjini wasijidanganye mazao yataendelea kupanda tena zaidi gharama za kilimo zipo juu sana hakuna mtu anayependa kuingia hasara mimi naona mazao kutoka nje ni fursa ya watu kuongeza kulima zaidi kuzuia mazao kwenda nje ni maamuzi ya kisiasa tu
 
HV ule mpango wa Kenya na mahindi ya gmo umefikia wapi .inamaana wakenya wengi wanapesa na wanaweza kumudu kununua unga elf 4000
 
Halafu watoto wa wakulima utawatibia wewe? Utawanunulia viatu na nguo?

Kuzuia chakula kwenda nje ni mwanzo wa umaskini mpya
Niwatibie nini? Nilikuwa natetea wakulima ila baada ya kuona hawajielewi nimewakacha..
 
Serikali zetu hizi ni miyeyusho sana
Kuna kipindi wakuu wa wilaya walikuwa wanaamua tu wilaya hii hakuna kutoa nafaka nje ya wilaya basi mnabaki mnahangaika tu hakuna pakuuza mazao yenu.

Hawajui kuwa wakulima wanategemea mazao hayo hayo kujenga, kusomesha watoto na matumizi binafsi ?
 
Hii nchi ni ngumu saana,mazao yakiruhusiwa yatoke nje..bei inapaa kias kwamba watu wanalalamika kununua maharage kilo 4000.

Serikali ikifunga mipaka pia mnalalamika..huwa mnataka nini hasa?
Serikali inatakiwa iwawezeshe wananchi wake walio wengi waondokane na umaskini wa kipato waweze kununua chakula kwa bei itakayompa faida mfanyabiashara na mkulima.
 
Back
Top Bottom