Malumbano kuhusu bandari na uwekezaji utakaofanywa na DP yametosha. Tufunge mjadala, tuchape kazi

Malumbano kuhusu bandari na uwekezaji utakaofanywa na DP yametosha. Tufunge mjadala, tuchape kazi

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2012
Posts
20,561
Reaction score
24,428
Tuchapeni kazi, serekali yetu sikivu imesikia inafanyia kazi kwa umakini mkubwa maoni yote. Tufunge sasa mjadala huu imetosha, tunachelewa sana kwa mijadala isiyokwisha na ambayo pengine inaweza kuhatarisha Utaifa na umoja wetu watanzania kwani hata maadui wa Taifa wanaweza kupitia mlango huu huu kuivuruga nchi yetu.

FB_IMG_1689583064626.jpg

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.
 
View attachment 2690681

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.
Hatuwezi kamwe kunyamaza wala kunyamazishwa mpaka huu mkataba ufutwe
F1IsQK8WwAAiK0D.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuchapeni kazi, serekali yetu sikivu imesikia inafanyia kazi kwa umakini mkubwa maoni yote. Tufunge sasa mjadala huu imetosha, tunachelewa sana kwa mijadala isiyokwisha na ambayo pengine inaweza kuhatarisha Utaifa na umoja wetu watanzania kwani hata maadui wa Taifa wanaweza kupitia mlango huu huu kuivuruga nchi yetu.

View attachment 2690681

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.
"Wazanzibari wameuza bandari zetu na mgao wamepewa baadhi ya viongozi na mbaya zaidi wamewasambaza wabunge wa Tanganyika nayo ipo kama mipoyoyo inazunguka mikoani na majimboni bila kujua inasaidia kuuza rasilimali za nchi, kama vipi muuzaji si angetembea mwenyewe? " ni sio maneno yangu ni sauti ya mzee mmoja akichangia mjadala wa bandari ulioanzishwa kwenye basi la abiria kutoka Tanga kwenda Dar.
 
Tuchapeni kazi, serekali yetu sikivu imesikia inafanyia kazi kwa umakini mkubwa maoni yote. Tufunge sasa mjadala huu imetosha, tunachelewa sana kwa mijadala isiyokwisha na ambayo pengine inaweza kuhatarisha Utaifa na umoja wetu watanzania kwani hata maadui wa Taifa wanaweza kupitia mlango huu huu kuivuruga nchi yetu.

View attachment 2690681

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.
Futeni huo mkataba. Hii ngoma ndo kwanza inaanza mtajua hamjui
 
Inaonekana mleta hoja umezoea ubishi wa vijiwen simba na yanga.
Mambo ya .....ngoja tusubiri mechi.
Umeniaibisha.
Hebu jielimishe kidogo nini kimeleta mgogoro. Kifupi tu wenye akili, hekima na busara wapo katika vita dhidi ya ukoloni mamboleo.
Msaidie mwanao asipige kaburi lako teke mbelen hasa akielimika
 
Mkataba wa kipuuzi kabisa, Samia na Mbarawa ni wasaliti wakubwa sana kwa hii Tanganyika yetu.
 
War with a ghost,wastage of time,NEC imeshapitisha, kila kitakachoimbwa is useless ......! (Kuonyeshwa kamkataba kamoja tu tena kiungwana imekuwa shida, ukionyeshwa wa gas nio watu watazimia na kufa)[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]View attachment 2691592
Hapa baada ya kujifunga kwenye mtego wenyewe, sasa mnategemea huruma ya mwarabu kubadili vifungu vya mkataba wa hovyo mlivyoweka saini zenu wenyewe, huu ni upumbavu wa hali ya juu sana.
 
Tuchapeni kazi, serekali yetu sikivu imesikia inafanyia kazi kwa umakini mkubwa maoni yote. Tufunge sasa mjadala huu imetosha, tunachelewa sana kwa mijadala isiyokwisha na ambayo pengine inaweza kuhatarisha Utaifa na umoja wetu watanzania kwani hata maadui wa Taifa wanaweza kupitia mlango huu huu kuivuruga nchi yetu.

View attachment 2690681

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.
Tutaacha mjadala, mkataba huu mbovu na wa kipumbavu ukifutwa
 
Kwani mmeshazijibu hizi hoja?

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Back
Top Bottom