Mama aliyedaiwa kufanya ukatili na video yake kusambaa mitandaoni akimpiga mtoto akamatwa

Wewe mbona kipigo kilikusaidia? Watoto wasiosikia mara moja moja unamtandika. Mbona wengi wananyooka tu.
Hapana, sina rekodi yakupigwa kama mwizi mkuu.
Sisi tulichapwa sio kupigwa kama jambazi.
Tulikuwa tukikosea saana, mzazi anakuita anakuonya na anakwambia ukakate fimbo nikuchape ili ukitaka kukosea tena ukumbuke hiki kiboko.

Unachapwa kwa staha na utaratibu
 
Ndio Matukio ambayo kitengo Cha polisi Cha intelligenjensia huwa kinajipatia maujiko.
 
Huyu mchukua video kwanini asitete huyo mtoto?
 
Wazazi wa siku hizi tumekuwa nyoronyoro sana! Biblia yenyewe inatuagiza tuwatandike sasa huyo kuguswa tu yamekuwa makelele! Mh. Gwajima mwachie huyo mama akaendelea na shughuli zake!
 
Reactions: I M
Nadhani hii ndio point ila huyu mama yeye anajipigia tuu randomly nadhani mtoto anatakiwa kuelekezwa. Sijawaelewa watu wanaosema kapigwa kidogo
 
Nadhani hii ndio point ila huyu mama yeye anajipigia tuu randomly nadhani mtoto anatakiwa kuelekezwa. Sijawaelewa watu wanaosema kapigwa kidogo
Ni ujinga.
Ndio maana watanzania wengi ni makondoo kwa vile wamelelewa kama wanyama.
Mimi ni mlezi bora sana, naelekeza, naonya kwa upole na ukali inapobidi...fimbo ni hatua ya mwisho tena fimbo ya staha na utu.

Huyu mwanamke angekuwa mke wangu yaani ilikuwa ndio kwaheri.

Unapiga mtoto kama kibaka?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…