Sawa mkubwa. Imekuwaje sasa mkeo anavusha mpaka ndani bila woga. Nimeshawahi chepuka na wake za watu kama wawili suala la kupeleka watu kwao ilikuwa ni kitu ambacho hakiwezekani. Heshima bado ilikuwepo.
Kwasasa nimeoa ndoa halali ya kikristo kama unafikiri ni mtoto umekosea.
Maneno yangu kwamba hujakua yalitokana na comment yako
Umetamka hivi, ""utamuachaje rafiki aje kwako inaonekana hujiamini
""Umeshindwa kumcontrol mke wako
Nimenukuu kauli zako mbili hapo juu ndipo nikafika hatua ya kuamini ww ni mdogo
Acha nikusahihishe mkuu,
Ndugu zako na marafiki zako kuja kwako kukutembelea sio shida, sasa kama mm nimesafiri ndugu na marafiki wanakoma kuja kwako?
Umeacha binadamu wenye pumzi ya uhai ndani kwa miezi mitatu, watoto2 mke, hg etc, sasa rafiki zako kupita hapo kuwaona wanaendeleaje ni tatizo?
Mke kuzini ni suala la tabia halina uhusiano na rafiki kuja nyumbani,
Mm pia huwa naenda kuziona familia za marafiki zangu tulioshibana wanaposafiri kuwajulia hali
Pili, kuhusu ku mcontrol mke
Hapa ndipo nilipokushangaa, nawezaje kum control mke nipo safari? Nipo nje ya tanzania kwa miezi mitatu, namcontrol vipi mke hapo?
Matendo haya yamefanyika sipo, lakini hata hivyo mwanadam huwa anabadilika, kama ww hapo na mkeo mmeanza maisha vizuri baadae mmoja wenu anaweza kubadilika na kuwa mtu mbaya kiasi kuwa ukashangaa huyu ndie mlianza nae maisha pamoja!!!
Umedai huenda hatukufahamiana mapema, tulioana tu, nani kakudanganya kufahamiana sana wakati wa uchumba ni guarantee ya mke/mume kutobadilika kitabia? Yapo mambo mengi sana katika maisha yanayoweza kubadilisha mtu tabia, kila mtu anao uwezo wake wa kuhimili tamaa za mwili, yupo ambae mwisho wake ni wiki, mwezi, miezi,
Kwenye ndoa kuna vitu vingi sana
Uzinzi ni tatizo kubwa kwa sasa, wake za mabosi wanazini, wa mawaziri, wake za maskini na kadhalika, hakuna formula maalum ya usaliti,
Hivyo natarajia mtu yeyote mwenye ndoa kuvifaham vitu hivi, ndo maana kwa yale maandishi yako ya awali nikasema ni wazi huna ndoa na huna uzoefu wa maisha, hata hivyo umedai una ndoa tena ya kanisani, well siwezi kupinga, ila ni wazi unahitaji kujifunza mengi, utayajua mengi mbele ya safari yako ya ndoa
Vinginevyo huenda hukusoma mada vizuri ukaanza kuchangia tu mkuu
Good day