Mama anamtetea mke wangu pamoja na kunisaliti

Swali dogo la kizushi:

Kitatokea nini ukijasikia huyu mpenzi wako wa sasa unayetaka kumuoa anakucheat?? Kama utapotezea, je ukimfumania?(Usinijibu kama ulimkuta bikira)
Adhabu ya uzinzi kwa mke inajulikana, unfortunately haina mbadala
Ni kumuacha hata ikijirudia mara ngapi, hata hivyo sio muhimu kujadili jambo ambalo halijatokea

Na ni jambo la kushangaza kusamehe mzinzi uki assume hata ukioa mwingine atafanya tu
 
Ukiomba ushauri wa jambo uwe tayari kupokea kila aina ya ushauri then wewe uko ndo utachuja Sasa wewe unaleta jambo ushauriwe harafu kumbe tayari umeshafanya maamuzi huko nikutujaribu ujinga.Amua uonavyo ni sahihi Ila nilikua najaribu kukupatia ushauri binafsi nilishapitia kwenye familia ya migogoro japo kweli haikusabishwa na jambo la uzinzi Ila mzee alivyoihandle lile tatizo mpaka Leo Hakuna mtoto mwenye mapenzi naye wote tuko kwa mama.
 

Kusamehe sio ujinga, sio upumbavu wala sio udhaifu bali kusamehe ni amri kutoka kwa Mungu kwa sababu Mungu anatutaka tuwasamehe wanaotukosea kama yeye anavyotusamehe sisi tunapomkosea.

Kusamehe kuna faida nyingi sana ikiwemo kuleta ahueni kwa watu ikiwemo kwa yule aliyokosea na aliyekosewa na pia inasaidia kuondoa mazingira ya chuki na kuleta upendo baina ya mkoseaji na alikosewa.

Hakuna kitu kinaitwa fate au destiny katika ndoa, bali the choices we make na matendo yetu ndio yanaweza kufanya ndoa zetu ziwe nzuri au mbaya, ziwe na furaha au karaha, ziwe na amani au vurugu.
 
 
Hivi wanawake wangewabaini wanaume na kuchukua hatua kama hizi familia au ndoa timilifu zingebaki ngapi. wanawake kusamehe kawaida wanaume kusamehe ni kituko
 
Reactions: nao

They say "A fool thinks himself to be wise, but a wise man knows himself to be a fool."
 
Adhabu ya uzinzi kwa mke inajulikana, unfortunately haina mbadala
Ni kumuacha hata ikijirudia mara ngapi, hata hivyo sio muhimu kujadili jambo ambalo halijatokea

Na ni jambo la kushangaza kusamehe mzinzi uki assume hata ukioa mwingine atafanya tu
Mkuu we binafsi sio mzinzi?
 
Kumbe ishu hapa ni kuwa HUMPENDI. Sasa nimekuelewa.

Fuata moyo wako utakacho na usipoteze muda kuomba watu ushauri kwa jambo ambalo umeshalifanyia maamuzi.

Naitakia Simba ushindi kwenye mechi yao ijayo na samaki wa bwawa la jangwani
 
Nimekupata, kuna walionielewa na baadhi nadhani bado, naomba nirudie au niweke sawa kwa mara ya mwisho

Ni hivi nimekuja jukwaani nikiwa tayari nna maamuzi kuhusu hatma ya ndoa yangu, kwamba nilishamuacha mke wangu tangu 2012, tunaishi tu kama vile tupo hostel, kila mmoja na yake, hivyo ndoa haipo tena, sasa inaelekea four yrs nilishasahau yote hayo, kutoa ushauri kuhusu eneo hilo ambalo sikuja kuomba ushauri kwalo ni kazi bure

Eneo lililonileta hapa ni kuhusu mwanamke huyu kukatalia kwangu pamoja na jitihada zote nilizofanya ndipo nikaja hapa mnipe mbinu nimtoeje, badala yake mmeacha hili nililowaomba ushauri mnaenda kwenye lile ambalo nimelitatua

Uzoefu wako kuhusu familia yenu ni mambo yanayozitokea familia nyingi but unfortunately hiyo ndio fate yenu, baba yenu aliamua kuchagua furaha yake over yours, it was his choice, hata mm nimechagua furaha yangu kwanza, alichokifanya mama watoto wangu ni kibaya sana na siwezi kuishi nacho eti kwa kuwa watoto watateseka, I will try to provide everything they need, education,food,clothing, etc, furaha ni matokeo, yao haiwezi kuwa muhimu kuzidi yangu mwenyewe
 
Kila la kheri.unaweza mwitia serikali ya mtaa ikakusaidia kumtoa hapo.
 
Umeanza vizuri ili uliposema na we ukaamua kuchukua msichana mwingine tena unakawa unalala nae kwako, sijaona tofauti kati yako na huyo mke wako.
 
Haya ni mawazo yako, bahati mbaya hayana sehemu kabisa katika ninachokiamini mm na watu wanaofikiri kama mm, hata biblia inaruhusu kumuacha mzinzi
Pia msamaha aulazimishwi, napingana nawe, kuna destiny na fate katika ndoa, ukilazimisha utapata matatizo
Since nimeshaamua kutosamehe then lets agree to disagree
 
kama ametubu na kujutia kosa lake, huna budi kumsamehe for the sake of your children. Akija mama mwingine anaweza akakuvuruga kuliko huyo.



ashasema, anasamehe dhambi zoote! lakini uzinzi a ah! hapana! hasamehi, hata mimi siwezi kusamehe uzinzi! rather nisamehe kesi ya kuua! lakini ya uzinzi hapana!.
 
Umeanza vizuri ili uliposema na we ukaamua kuchukua msichana mwingine tena unakawa unalala nae kwako, sijaona tofauti kati yako na huyo mke wako.

KWA HIYO, TUSEME NGOMA DROO?!, HAPANA MANZI AKE NDIE ALIANZA KUCHEPUKA!.
 
Km umefanya hayo yote umefanikiwa nini kifamilia zaidi ya kusambaratika tu suala la kutoa watoto kk sahau mbeleni ndio bomu lako kwani baadae utaonekana wewe ndio ttz ikifika fainali
 
Hata kulipiza kisasi haikupaswa iwe hivyo bali ungekuwa unachapa nje na usimuonyeshe kbs zaidi ungejua kuwa je bado anaendelea na mchepuko wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…