6 Pack
JF-Expert Member
- Apr 17, 2022
- 2,819
- 5,996
Acha ujinga wewe, hao ni watoto wake wa kuzaa, wamekaa tumboni kwake miezi 9, hivyo kama kudhulumu angewadhulumu wakati akiwa hajawazaa kwa kutoa mimba zao.Ameshindaje kesi ya mirathi?
Wametumia sheria ya serikali au ya dini kama ni dini ya kiislamu sheria ya mirathi mama anatakiwa apewe thumni ya mali yote ya marehemu mumewe na sio kupewa nyumba nzima au mali zote!!!
Huruma zingine hazifai kufuata masheria ya kidunia na kutoa haki kwa asiyestahili kupata haki na kudhulumu wengine.
Hivi unaijua thamani ya mzazi uliekaa tumboni kwake miezi 9? Je akiwarudishia hiyo mirathi akawaomba na wao wamlipe kwa kukaa tumboni kwao miezi 9 halafu ndo wamzae kama alivyowazaa wao wataweza?
Bila yeye kuwazaa au kuwalea mpaka wakakuwa wakubwa hiyo mali wangeweza kuirithi? Yani mali au nyumba ndio isababishe ukasimame na mama yako mzazi mahakamani? Nyumba inaweza kuungua au ikaanguka kama lilivyoanguka lile jengo la juzi hapo kariakoo lkn mzazi atabaki kuwa mzazi miaka yote ya maisha yenu iwe kwa raha au kwa shida.