Mama awashinda watoto wake Kesi ya Mirathi ya Nyumba Kariakoo

Mama awashinda watoto wake Kesi ya Mirathi ya Nyumba Kariakoo

Huwa kuna wakati inatokea ambapo hakuna mshindi bali losers wa viwango tofauti tofauti na hili nadhani ni that category (Kushitakiana kwao ndio ulikuwa mwanzo wa kupoteza) baada ya hapo ilikuwa ni mwendelezo wa cutting your losses.
 
Fatma Awadh mkazi wa Kariakoo amemshukuru Rais Samia na aliyekuwa waziri wa Ardhi Mhe. Jerry Silaa (sasa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari) baada ya kushinda kesi ya Mirathi ya Nyumba dhidi ya watoto wake.

Kesi hiyo iliyoanza 2006 imepata majibu baada ya kudumu mahakamani kwa miaka 18 ambapo Mama amewashinda watoto wake kwenye Mirathi ya nyumba iliyopo Kariakoo Dar es salaam.
View attachment 3170874
Usiwarithishe hata sumni!
 
Unaleta ujuaji na huruma za hivyo...huyo mama haki yake katika mirathi ni kupewa thumni ya mali zote za urithi(yaani kama sijakosea anatakiwa apewe theluthi ya mali yote) na sio kupewa mali yote yeye kama mke au mama wa hao watoto....daraja la mama ni kubwa lakini aliweka hilo daraja ndio huyo huyo aliyempa haki ya kupata thumni katika urithi,kama alitaka haki yake basi wangekusanya mali zote kama zinauzwa halafu yeye apewe theluthi tu ndio haki yake......usilete huruma za kibidamu Mwenyezi Mungu kisha fafanua kila kitu....tamaa za hiyo familia wameshindwa kugawana mirathi kwa sheria za Mwenyezi Mungu wamekimbilia mahakamani hatimae limegeuka hata huyo mama kapewa tu lakini ataadhibiwa kwa kudhulumu haki za watu.
Kata rufaa.
 
Hongera sana Mahakamankwa kutenda haki. Watoto watafute mali yao.
Hao ni watoto wajinga sana, mzazi anapokuwapo hai, hata awe mzazi mmoja, watoto wanabakia kama watoto na hutakiwa kumuheshimu mzazi aliyepo, isipokuwa endapo wazazi wote watakuwa wametwaliwa mbele za haki hapo ndipo mali huweza kuonwa lipi la kufanyika kwa watoto!
 
Hawa ni wale watoto walikuwa, hawakulelewa kimaadiii. Yani wamekuzwa kihunihuni tu na kujiona wa mjini, muda wote kushinda vijiweni. Na ndo wamo wengi humu jf, wanatukana watu hovyo hata wasiowajua na kujifanya wana vi-degree vyao vya mserereko. Na sjui kwa nini hawajiulizi iweje sasa hivi hivyo vidgree vimetapakaa hadi vijijini. Wamepata elimu mfu ya mserereko lakini leo wanaingia humu na visimu vyao vya mkpo wanaanza ku-argue ignorantly.

Kwa vyovyote iwavyo whether sheria ya dini au kabila, hauwezi kushindana na mzazi wako hadi kumpeleka mahakamani kisa mali za urithi. Huo ni ukosefu wa maadili na heshima kwa mzazi, eti kisa tu una vi-degree vyako uchwara unajua haki. Huyo mama labda hao siyo watoto wake wa kuzaa. Hivi unakubali vipi mama yako ateseke nyumba za kupanga kisa dini au mila imekupa rungu la kumnyang'anya mali. Mitoto haramu huyo.
 
Kama kesi imetolewa uamuzi na mahakama hapo shukurani kwa Samia na Silaa vinatokea wapi? au wao ndiyo wametoa hiyo hukumu kwa maelekezo yao?
 
Halafu kibenten Mario anakuja kufaidi mali ya baba

Ameshindaje kesi ya mirathi?
Wametumia sheria ya serikali au ya dini kama ni dini ya kiislamu sheria ya mirathi mama anatakiwa apewe thumni ya mali yote ya marehemu mumewe na sio kupewa nyumba nzima au mali zote!!!

Huruma zingine hazifai kufuata masheria ya kidunia na kutoa haki kwa asiyestahili kupata haki na kudhulumu wengine.
 
Alifanya hivyo, ataua kizazi chake...!!! Tunahitaji kizazi chake kinachotambua namna ya kutetea haki kutoka kwa wakorofi Hata kama wakorofi hao ni damu yako.
Kizazi chake kishakuwa batili Bora ampe Mungu kama wototo wote wameunga kumuumiza mama Yao hapo hamna kizazi tena
 
Hao hao unaowaita wavaa kobazi ndiyo wamiliki wa maghorofa mengi kuanzia Kariakoo, Upanga , Mnazi Mmoja na maeneo mengi ambayo ni potential.

Sasa hata ukiwaita majina yakupendazayo wala hawana muda na wewe wala hawakufahamu.
haaaaaaaaaaaa
 
Sikiliza hiyo clip; kwa kinywa chake anashuhudia kuwabeba mimba wote hao the foxes!
Aseeh ni changamoto kwenye issue za mirathi ebu wazazi wetu wakiwa na Mali au utajiri mwingi wajitahidi kuandaa wosia kwa yeyote anayemtaka.....

Nimeshuhudia familia nyingi hawazungumzi kwa sababu tuu ya Mali,

Nadhani hata humu Kuna kesi kibao zimeandikwa za wahanga .....

Tunahitaji elimu juu ya mirathi na wosia kwa upana ili kuondoa usumbufu wa kipumbavu kama huu..

Mwisho hata kama mzazi ana ukwasi na unaona hakushirikishi jifunze kuunda nawe juhudi za kutafuta vyako hata kama urithi utakufuata basi ukukute nawe una kitu chochote...
 
Hawa ni wale watoto walikuwa, hawakulelewa kimaadoli. Yani wamekuzwa kihunihuni tu na kujiona wa mjini, muda wote kushinda vijiweni. Na ndo wamo wengi humu jf, wanatukana watu hovyo hata wasiowajua na kujifanya wana vi-degree vyao vya mserereko. Na sjui kwa nini hawajiulizi iweje sasa hivi hivyo vidgree vimetapakaa hadi vijijini. Wamepata elimu mfu ya mserereko lakini leo wanaingia humu na visimu vyao vya mkpo wanaanza ku-argue ignorantly.

Kwa vyovyote iwavyo whether sheria ya dini au kabila, hauwezi kushindana na mzazi wako hadi kumpeleka mahakani kisa mali za urithi. Huo ni ukosefu wa maadili na heshima kwa mzazi, eti kisa tu una vi-degree vyako uchwara unajua haki. Huyo mama labda hao siyo watoto wake wa kuzaa. Hivi unakubali vipi mama yako ateseke nyumba za kupanga kisa dini au mila imekupa rungu la kumnyang'anya mali. Mitoto haramu huyo.
Wangekuwa wachaga kwa kisa hiki lingetukanwa kabila lote wallahi!
 
Wahuni sio watu unamshtaki Mama kwenye nyumba yake aisee ili iweje kama ni rahisi watafute zao wawe na nyumba hapo mtaa wa Livingstone waone kazi..
 
Ni mama yao wa kuwazaa ? ama ni Hawa mama wa kufikia ama wa kambo ?

Kama mama yao mzazi kabisa pengine nyumba hiyo inaweza kuwa Mali si ya mumewe bali ni ya wazazi wake

Mara nyingi nijuavyo Mali kama hiyo ingekuwa upande wa mume au baba wa hao watoto asilimia nyingi zingeenda kwa watoto lakini ki ujumla mambo ya urithi/mirathi ni magumu mno.
Ni mama yao mzazi mkuu. Hata hapo kwenye video amesema wazi kuwa hao ni watoto wake wa kuwazaa waliokaa tumboni kwake miezi 9 kila mmoja.

Anasema walikuwa 8 wawili wakafariki na kubaki 6 ambao ndio hao waliotaka kumdhulumu nyumba yake.
 
Back
Top Bottom