Mama awashinda watoto wake Kesi ya Mirathi ya Nyumba Kariakoo

Mama awashinda watoto wake Kesi ya Mirathi ya Nyumba Kariakoo

Hao hao unaowaita wavaa kobazi ndiyo wamiliki wa maghorofa mengi kuanzia Kariakoo, Upanga , Mnazi Mmoja na maeneo mengi ambayo ni potential.

Sasa hata ukiwaita majina yakupendazayo wala hawana muda na wewe wala hawakufahamu.
Na ndio hao hao mifisadi papa, wakwepa kodi wakubwa na wauza unga waliokubuhu na misijdah yao mikubwa kama chapati pajini.

Nyau de adriz
 
Acha ujinga wewe, hao ni watoto wake wa kuzaa, wamekaa tumboni kwake miezi 9, hivyo kama kudhulumu angewadhulumu wakati akiwa hajawazaa kwa kutoa mimba zao.

Hivi unaijua thamani ya mzazi uliekaa tumboni kwake miezi 9? Je akiwarudishia hiyo mirathi akawaomba na wao wamlipe kwa kukaa tumboni kwao miezi 9 halafu ndo wamzae kama alivyowazaa wao wataweza?

Bila yeye kuwazaa au kuwalea mpaka wakakuwa wakubwa hiyo mali wangeweza kuirithi? Yani mali au nyumba ndio isababishe ukasimame na mama yako mzazi mahakamani? Nyumba inaweza kuungua au ikaanguka kama lilivyoanguka lile jengo la juzi hapo kariakoo lkn mzazi atabaki kuwa mzazi miaka yote ya maisha yenu iwe kwa raha au kwa shida.
Peleka umbea wako huko.

Nyau de adriz
 
Ameshindaje kesi ya mirathi?
Wametumia sheria ya serikali au ya dini kama ni dini ya kiislamu sheria ya mirathi mama anatakiwa apewe thumni ya mali yote ya marehemu mumewe na sio kupewa nyumba nzima au mali zote!!!

Huruma zingine hazifai kufuata masheria ya kidunia na kutoa haki kwa asiyestahili kupata haki na kudhulumu wengine.
Serikali Haina dini acheni tamaa Kwa mgongo wa dini
 
Ni mama yao wa kuwazaa ? ama ni Hawa mama wa kufikia ama wa kambo ?

Kama mama yao mzazi kabisa pengine nyumba hiyo inaweza kuwa Mali si ya mumewe bali ni ya wazazi wake

Mara nyingi nijuavyo Mali kama hiyo ingekuwa upande wa mume au baba wa hao watoto asilimia nyingi zingeenda kwa watoto lakini ki ujumla mambo ya urithi/mirathi ni magumu mno.
Mume akifa automatic Mali zake zinahamia Kwa mke
 
Watoto kama hao wapo sana kwenye jamii zetu na wengi huwaombea wazazi watangulie mapema ili warithi mali ambazo hawajazitafuta wao, tufanyeni kazi kwa bidii kujitafutia vyetu binafsi. Na watoto pia tuwakuze na mentality ya kuwajibika kufanya kazi ili wajitegemee vinginevyo kina junia wataleta shida sana.
 
Ni mama yao wa kuwazaa ? ama ni Hawa mama wa kufikia ama wa kambo ?

Kama mama yao mzazi kabisa pengine nyumba hiyo inaweza kuwa Mali si ya mumewe bali ni ya wazazi wake

Mara nyingi nijuavyo Mali kama hiyo ingekuwa upande wa mume au baba wa hao watoto asilimia nyingi zingeenda kwa watoto lakini ki ujumla mambo ya urithi/mirathi ni magumu mno.
Mitoto 9 inagombea nyumba na mama ya mzazi wa kuwazaa yeye mwenyewe; mzee mjane asiye na hili wala lile! By any means, hakuna sheria yoyote iwe ya kidini au kisekula inayotakiwa kuhalalisha uhuni wa aina hiyo. Huyo bibi kikongwe mjane aende wapi sasa! Mahakama imetenda haki japo kwa kuchelewa mno 20 yrs kupata haki is not acceptable.
 
Acha ujinga wewe, hao ni watoto wake wa kuzaa, wamekaa tumboni kwake miezi 9, hivyo kama kudhulumu angewadhulumu wakati akiwa hajawazaa kwa kutoa mimba zao.

Hivi unaijua thamani ya mzazi uliekaa tumboni kwake miezi 9? Je akiwarudishia hiyo mirathi akawaomba na wao wamlipe kwa kukaa tumboni kwao miezi 9 halafu ndo wamzae kama alivyowazaa wao wataweza?

Bila yeye kuwazaa au kuwalea mpaka wakakuwa wakubwa hiyo mali wangeweza kuirithi? Yani mali au nyumba ndio isababishe ukasimame na mama yako mzazi mahakamani? Nyumba inaweza kuungua au ikaanguka kama lilivyoanguka lile jengo la juzi hapo kariakoo lkn mzazi atabaki kuwa mzazi miaka yote ya maisha yenu iwe kwa raha au kwa shida.
ukisikia hivyo huyo ni mama wa kambo siyo wa kuwazaa wenyewe.
 
Fatma Awadh mkazi wa Kariakoo amemshukuru Rais Samia na aliyekuwa waziri wa Ardhi Mhe. Jerry Silaa (sasa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari) baada ya kushinda kesi ya Mirathi ya Nyumba dhidi ya watoto wake.

Kesi hiyo iliyoanza 2006 imepata majibu baada ya kudumu mahakamani kwa miaka 18 ambapo Mama amewashinda watoto wake kwenye Mirathi ya nyumba iliyopo Kariakoo Dar es salaam.
View attachment 3170874
Watanzania hata mahakama ikitoa haki anashukuriwa rais.
 
Back
Top Bottom