Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kumbe jezi ingetupotezea msanii maarufu kutoka Tanzania . Lakini mzee aliongea kwa hisia sana.
Nipeni jembe nikalime.Habar wanaJF,
Aliyesema kuwa wanawake na mama zetu tusiwaamini hakukosea leo kwani huenda wazazi wetu wa kiume walio tulea sio baba zetu.
Leo Rikardo Momo amesema kuwa mzee Abdul sio baba yake Diamond na kusema kuwa yeye na Diamond wanachangia baba na baba yao anaitwa Mzee Salim Nyange.
Haya yote yanaweza kuwa sawa lakini kwanini Diamond anaitwa Naseeb Abdul na siyo Salim Naseeb Nyange? Hivi inawezekana baba mlezi kupewa hadhi ya ubin wa mtoto au ndio mama Diamond anataka amalize mchezo?
Na kama ni kweli Mzee Abdul sio baba yake Diamond huenda mama Diamond alikataliwa hii mimba na mzee Salim Nyange akaamua kumtupia zigo mzee Abdul na bila shaka mzee alikubali kiroho safi ila huenda alikuwa anaambiwa mengi na ndugu pamoja na rafiki.
Apa hii story sioni kama ina utofauti na story iliyopo kwenye mziki wa Stamina na Profesa Jay maana namuona Diamond anamlaumu Mzee Abdul kwa kutokumlea ilihali Mzee Abdul alijua Diamond siyo mwanae na bado akaendelea kuwa baba kwa uwezo wake.
Ila sijaamini kama Mzee Abdul sio baba yake mzazi Diamond sababu sio rahisi mtoto alelewe na baba wa kambo mpaka abadilishe jina la ubin wake pia na kuwapa mpaka watoto zake jina la babu yao feki walitumia kama babu yao.
Hizi ni faulo zinataka kuchezeka hapa Mama Diamond anataka kumaliza mechi.
======
Maneno ya Mama Diamond
Mama mzazi wa Diamond Platnumz akijibu kuhusu swali la Dida ambaye ni Mtangazaji wa Wasafi FM, ambaye aliuliza kuhusu uhusiano wa Diamond na Ricardo Momo, mama huyo amejibu kwa kuuliza ''Diamond na Ricardo mnawaonaje?, ambapo Dida alisema wanafanana.
Mama Diamond akaendelea kusema kuwa Baba mzazi wa Diamond anaitwa Salum Idd Nyange huku akidai kuwa Mzee Abdul ni baba mlezi wa Diamond kwani wakati wanaingia kwenye mahusiano alimwambia kuwa kuwa ana ujauzito na Mzee Abdul kusema kuwa ahusiki.
Mama huyo amedai kwamba mzee Abdul alimkataa Diamond tokea mimba na hakuwahi kuwa na mchango wowote kwa Diamond kuanzia vidudu mpaka Sekondari.
Mama Diamond amekuwa akimwambia mzee Abdul kwamba bora ungemkubali Diamond tokea mdogo sasa hivi ungekuwa na mtoto, na ndicho amekuwa akimwambia siku zote.
Baba Diamond atoa neno
Adai kuwa amesema mbele ya watanzania wote kuwa kuanzia wakati huo hamtambui tena Diamond kama mtoto wake kwa kuwa imeshatamkwa kuwa yeye si baba wa mtoto.
Na alipoulizwa kuhusu kupima vinasaba (DNA) ili kuipambania haki ya uzazi kwa Diamond alijibu kuwa mtoto hagombaniwi kama ilivyo mpaka wa nyumba haugombaniwi.
Mzee Abdul Amtaka Diamond Aache Kutumia Jina Lake
"Mtoto hagombaniwi… Mimi nimekubali siwezi nikapinga, atakancel jina langu, ataenda kuoneshwa kaburi la baba yake basi inatosha," alisema Mzee Abdul
By Jackline Mgeni 15 Jan, 2021 0
Mzee Abdul ambaye awali alikuwa anafahamika kama Baba yake mzazi Diamond amemtaka msanii huyo aache kutumia jina lake (Nasib Abdul) kwani sasa sio familia moja tena.
Suala hilo linakuja baada ya Sanura Kassim maarufu Mama Dangote ambaye ni mama mzazi wa msanii wa kizazi kipya, Diamond Platnumz kuweka wazi kuwa baba halisi wa Diamond si Abdul Juma bali ni Salum Iddi Nyange ambaye pia ni baba mzazi wa Ricardo Momo, Meneja wake msanii Lavalava.
Abdul Juma amekuwa kwa miaka mingi akifahamika kama baba wa msanii huyo wa Bongofleva.
Mama Dangote ameeleza hayo leo Ijumaa Januari 15, 2021 baada ya kupigiwa simu na Dida, mtangazaji wa kipindi cha Mashamsham kinachorushwa na redio ya Wasafi kueleza kuhusu uhusiano kati ya Diamond na Ricardo Momo aliyekuwa akihojiwa na redio hiyo.
Katika majibu yake, mama Dangote amesema Ricardo na Diamond ni ndugu na baba yao ni Nyange ambaye kwa sasa ni marehemu.
Akizungumza na Simulizi na Sauti baada ya kumalizika kwa mahojiano hayo, Mzee Abdul amesema amefurahi kusikia jambo hilo akidai kuwa sasa atakuwa huru kwani sasa anajua nafasi yake ndani ya familia hiyo.
“Kama muhusika akishakwambia hauhusiki basi mi naamini hamna haja ya kujiforce…mtoto hagombaniwi…mimi nimekubali siwezi nikapinga, atakancel jina langu, ataenda kuoneshwa kaburi la baba yake basi inatosha” Mzee Abdul akijibu swali la mtangazaji lilimtaka ajibu kama amekubali suala hilo kwasababu alikuwa hasaidiwi kama anavyodai ama kwa sababu ni kweli kwamba mtoto huyo siyo wa kwake.
“Nadhani mhusika ameshazungumza sawasawa kabisa,” amesema Abdul na alipoulizwa kama alikuwa anafahamu suala hilo alijibu, “hapana” Amesema kuanzia leo amekubali kuwa Diamond si mwanaye na kuongeza kuwa huenda ndio sababu msanii huyo alikuwa hanitimizii mahitaji yangu, “nashukuru sasa kwa kulijua suala hilo kwa undani na nampa big up sana kwa kuliongea hilo” aliongeza.
View attachment 1678472
Hata Mie nawashangaa ndio maana hata alivyokuwa alimkataa mama yake alifuata ya kuolewa Tu mtoto wake akawa anajitunzia mwenyewe. Wenye akili tulishamshtukia huyu Mzee angekuwa kweli ni Baba WA Dai na Dai anamtendea ndivyo sivyo na yeye alimkana asingejitokeza hadharani kujiabisha angekula Jiwe Tu. Kuna walakini mkubwa WA kauli matendo ya Mzee Abdul dhidi ya Diamond.Mnalazimisha sana Abdul awe baba yake Diamond
Basi sawa, na ndo mwisho wa Diamond huu manake kiki aliyokuwa anaitegemea ndo imeshatoweka!!Domo kamtumia sana mzee naona sasa wameamua kumtosa
Bila shaka kwenye mikataba pia ametumia jina hilo. Mzee kama akikomaa alifute kisheria sijui athari yake itakuwa ya namna gani!Hata kama ni Kiki ni upuuzi sasa Nasib Abdul mbona amechukua jina la MZee Abdul?
bikra hivi zipo kweli?Nikiwaambia muoe wanawake bikra mnaniona hamnazo, embu angalie kile kisa cha Muna Love yaani pale Daah!
Hamna athari yoyote kwa sababu sio kwamba Mzee Abdul hakufahamu jina lake linatumika! Suala kwanini litumike wakati sio mtoto wake, hiyo haiwezi kuwa issue!!!Bila shaka kwenye mikataba pia ametumia jina hilo. Mzee kama akikomaa alifute kisheria sijui athari yake itakuwa ya namna gani!
Wanaume huwa hatusemi mapungufu ya wake zetu ikiwa tumeachana nao! Kuna mambo mengine ni ya kiudhalilishaji kwa sababu kuyatamka hautomdhalilisha mwanamke bali unamdhlilisha mama wa mtoto wako na kuidhalilisha familia ya mwanamke nzima.Hata Mie nawashangaa ndio maana hata alivyokuwa alimkataa mama yake alifuata ya kuolewa Tu mtoto wake akawa anajitunzia mwenyewe. Wenye akili tulishamshtukia huyu Mzee angekuwa kweli ni Baba WA Dai na Dai anamtendea ndivyo sivyo na yeye alimkana asingejitokeza hadharani kujiabisha angekula Jiwe Tu. Kuna walakini mkubwa WA kauli matendo ya Mzee Abdul dhidi ya Diamond.
Unasema yupo kimya? Haya yote ameyasababisha mwenyeweHuyu mzee mnamuandama sana wakati yeye yupo kimya. Kwanini?
Wanaume huwa hatusemi mapungufu ya wake zetu ikiwa tumeachana nao! Kuna mambo mengine ni ya kiudhalilishaji kwa sababu kuyatamka hautomdhalilisha mwanamke bali unamdhlilisha mama wa mtoto wako na kuidhalilisha familia ya mwanamke nzima.
Zipo picha kadhaa wa kadhaa zinasambaa mitndaoni zikionyesha mzee akiwa na diamond tangu akiwa kichanga mpaka amekuwa kama wa miaka 10 au 12 hiviii..
Wanawake mna roho mbaya sana! Nimeyasikia na nimeyashuhudia kisa unagombana na mzazi mwenzako unamnyima mwanaume fursa ya kuwa na mwanae na kumlisha mtoto sumu tu kuhusu baba yake ijapokuwa wapo pia wanaokana malezi.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Babu tale kasema eti diamond ni mluguru....