Mama Diamond: Mzee Abdul alinikuta nina mimba ya Naseeb (Diamond) na aliikataa. Ricardo Momo na Diamond ni ndugu, baba yao ni Salum Idd Nyange

Mama Diamond: Mzee Abdul alinikuta nina mimba ya Naseeb (Diamond) na aliikataa. Ricardo Momo na Diamond ni ndugu, baba yao ni Salum Idd Nyange

Nimeitizam ile intvw ya Mzee Abdul na Mama yake D.
Kuna maswali mengi inabidi huyu mama ayajibu.
1.Kabla ya umauti kumkuta mzee Nyange,alikiwa anajua Nasib mwanae au nae alimficha?
2.Amesema D si mtoto wa mzee Abdul,bali alikuwa baba mlezi na mwanzo mzee Abdul aliikataa Mimba,sasa inakuwaje mtu anaye ikataa mimba awe baba mlezi.....????
3.Situation ya mimba ya Diamond kupatikana ilikuwaje kuwaje?

Alafu hata huyo mzee Abdul naye dish limeyumba,anasema Diamond hamsaidii jana kwa kinywa chake akihojiwa na SnS amesema Diamond huwaga anamsaidia na anampa hela zina range laki 2 mpaka 1mil,sasa najiuliza kwa nini alikuwa anasema uwongo akihojiwa na vyombo vya habari ?

Alafu inaonekana ana mmaindi Shamte,anadai haiwezekani yeye apate kidogo,wenzake wapate kingi.......😀😀😀.
Intavyuu ya Likado ilijieleza....Baba alimtambulisha Naseeb kwa Momo 1999 kabla hajawa Diamond....hiyo picha inajibu maswali nani baba halali.....Nyange hana haja ya DNA
 
Haiitaji ata DNA kumtambua mond na abdul. Sura tu zitamuumbua,, mond kafanana sana na abdul
labda tuseme huyu dingi sio Nyange ni Mond kabla hajawa na hela
Screenshot_20210116-082103.png
 
Hujafa hujambika, wababa wanaoamua kulea mimba na WATOTO wa wenzao wawalee kwa mapenzi Kama WATOTO wao
 
Ila huyu mzee kwa jinsi anavyopenda kamera kuna uwezekano mwezi mzima huu akawa anahojiwa na YouTube channels mbalimbali,ambazo hazi msaidii zaidi ya kumchoresha.
Mzee Abdul nadhani ana tatizo la IQ. Kama ni mm ningesema siongei na media yoyote unless waje na hela ya kutosha.

Yeye anaongea tu na kila kanjanja, wao wanapa content, wanapiga hela ilhali yeye wanamwacha hivyo hivyo.
 
Mzee Abdul nadhani ana tatizo la IQ. Kama ni mm ningesema siongei na media yoyote unless waje na hela ya kutosha.

Yeye anaongea tu na kila kanjanja, wao wanapa content, wanapiga hela ilhali yeye wanamwacha hivyo hivyo.
Aise ulichosema na mm nlikuwa nafikiria hivyo hivyo maana anawapa faida tu media uchwara

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Maneno machache tu.
Si kwa ubaya Mwenyezi Mungu kama ikimpendeza amchukue mja wake huyo Mzee Abdul ni imani yangu kivuli chake kitasalia na tutajionea mengi zaidi. Huwezi mdhalilisha mzee wa watu kiasi hiko kisa Mali za mtoto. Kwann usiseme mwanzoni huko kuwa yule sio baba mzazi wa Daimond? Inshallah mm niko upande wa mzee Abdul namuombea kwa M/mungu tabu zote alizopata kuilea mimba ya huyo Diamond pamoja na kumlea pindi alipozaliwa lkn leo anatukanwa licha ya changamoto za kulea kama tujuavyo wazazi wengi. Mwanaume kukubali kulea mimba isiyo yake hiyo ingetosha kabisa kumpatia haki zote za kuwa baba pamoja na msaada muhimu. YES MUNGU MUWEZA NA MUUMBA WA MBINGU NA ARDHI ATAONESHA MFANO KWA DHARAU ZA NAMNA HII AMIN.
Kama nimekuelewa sana mkuu
 
Huyu mzee anawakilisha wanaume wengi wanaopitia manyanyaso kutoka kwa mke akishirikiana na mtoto/watoto! Na hii hutokea tu pale mwanamke anapoamua kuwa mbinafsi baada ya mtoto/watoto kupato kipato kizuri.

Hatari kubwa ni kwamba huyu mzee atakuwa kwenye dimbwi kubwa la mawwzo pengine na msongo wa mawazo maana inaonekana kabisa kwamba huemda hata kula yake, malazi na hata kula kwake ni kwa kubahatisha sana ilhali mke na mwanae wanatumbua maisha bila kumfikiria kabisa.

Yani inashangaza sana hata mfagiaji wa nyumbani kwa Diamond atakuwa anaishangaa familia ya Diamond kumtekeleza baba yao ilhali mfagizi tu maisha yake ni supa.


Anyway kama kweli kuna KIAMA basi wachache sana watasalimika.


Ianzishwe movement mzee afunguliwe account bank ili kwa mwanaume yeyote asiyeridhishwa na anayoyapitia mwanaume mwenzetu tumchangie chochote aongeze siku za kuishi.
 
Sheria ipi hebu tuwekee hapa tujifunze.
Sheria ya Mtoto (The Law of the Child Act) inasema kila mtoto ana haki ya kuitwa kwa ubini wa baba ake. Kumnyima mtoto kuitwa kwa ubini wa baba ake ni kumnyima mtoto haki yake ya msingi. Mtoto hawezi kuitwa kwa majina ya mtu mwingine bila huyo mtu kumu-adopt kisheria mtoto huyo.

Na kwa utaratibu ukianza clinic ile kadi ya clinic inaandikwa jina la baba na hata kwenye tangazo la kuzaliwa. Sasa huyu bi maza yeye anaruka kama bisi haeleweki wakati interview za zamani walikua wanasema Dai alikua anaenda kudai hela za ada kwa mzee Abdul ananyimwa ndio chanzo cha yy kumchukia baba yake. Sasa hizo ada kwa nini asingekua anaenda kudai kwa mzee Nyange.
 
Hello JF,

Kama mnavyojua mwanamke akipata mimba ana uhakika mimba ni yake...

Ila kwa wanaume mimba hakuna guarantee ya kujua ni yake/ingawa kuna DNA testing siku hizi...

Swala la partenity ni suala linalowanyima usingizi wanaume...

Jambo ambalo lilikuwepo tangu zamani,

Mpaka leo it is believed wanaume wengi kuchepuka ni katika harakati za kutaka maximizing their chances of being a father, sababu kuzaana ndio lengo kuu la kuwepo sisi duniani.

Anyway,

nilichotaka kusema leo,

ingawa wanawake tunapenda ubuyu but watakaoongea sana kwenye hii ishu ya Diamond ni wanaume! lol

Tutegemee nyuzi nyingi za wakaka humu kuhusu hili... 🤣 🤣 🤣

Mama Diamond kagusa pale panapouma...

A reminder of their worst nightmares!

Wanaume wa humu tulieni tu dawa iwaingie🤣🤣

************* Diamond, is either uwaache wote baba zako au uwe nao wote, ukijifanya kuchagua mmoja over the other,the public wont forgive you. Anyway its your life.

Leo nimejiskia tu kuandika chochote....lol
 
Back
Top Bottom