Uchaguzi 2020 Mama Maria Nyerere: Nimelazimishwa kuja kuongea, niliwaambia nimekuja kuongeza wingi wa watu, Mkutano wa CCM Musoma

Uchaguzi 2020 Mama Maria Nyerere: Nimelazimishwa kuja kuongea, niliwaambia nimekuja kuongeza wingi wa watu, Mkutano wa CCM Musoma

Mama ni jasiri kama mumewe. Kweli mkiishi pamoja muda mrefu mnafanana.

Hawa jamaa kwa madaraka tu wana uchu. Huyo mama anastahili kupumzika sasa. Wao sijui wametoa wapi - Msasani ama Butiama na kumsimamisha jukwaani! Shame on you.

Mama Maria hakupata kutoa hotuba za kisiasa hata wakati wa utawala wa mumewe. Sasa wanamsomba akamfanyie Magufuli kampeni! Hawana akili kabisa. Nadhani hawatarudia tena.

Musoma ndio ilivyo. Hakuna unafiki huko. Hata Waitara wanamchinjia mbali. Labda NEC imtangaze kwa nguvu tu.
unajua mkuu ngoma ikilia sana mwisho hupasuka. yaan mama mtu mzima yule wanaenda kumzoazoa na kumbwaga majukwaan akapige makele ya kampeni kisa tu wameona wanazidiwa kete na upinzani. hivi huyu mama atawaongezea kura ngapi ma ccm ambazo zitaakisa kiwango cha udhalilishaji mnaofanyia majukwaani? yan hii ni ushahidi mzuri sana wa kimazingira kuwa ma ccm yapo tiyar kufanya chochote kile hata kama ni kutoa uhai wa mtu ili tu yashinde kura..hayajali gharama kwa watanzania...mpaka kumdhalilisha mama wa Taifa kweli?!! kisa tu kura? ndiyo maana mama kaamua inatosha, enogh is enough...kawaambia ukweli...MSIMLAZIMISHEEEEE.
 
Kwali Nimeamini ccm ni chama cha kishetani
 
Yule mama kafikisha ujumbe,.
Ajabu kwenye taarifa ya habari ya ITV SAA 2 usiku leo hawakuweka hiyo clip ya leo, badala yake wameweka sijui ya wapi na ya link ambapo anasikika akiisifia serikali.

Kwa waliotazama taarifa hii watakubaliana nami!
 
hoja nzito ya kutupaisha hii
chorus: tumeibiwa kura
unajua mkuu ngoma ikilia sana mwisho hupasuka. yaan mama mtu mzima yule wanaenda kumzoazoa na kumbwaga majukwaan akapige makele ya kampeni kisa tu wameona wanazidiwa kete na upinzani. hivi huyu mama atawaongezea kura ngapi ma ccm ambazo zitaakisa kiwango cha udhalilishaji mnaofanyia majukwaani? yan hii ni ushahidi mzuri sana wa kimazingira kuwa ma ccm yapo tiyar kufanya chochote kile hata kama ni kutoa uhai wa mtu ili tu yashinde kura..hayajali gharama kwa watanzania...mpaka kumdhalilisha mama wa Taifa kweli?!! kisa tu kura? ndiyo maana mama kaamua inatosha, enogh is enough...kawaambia ukweli...MSIMLAZIMISHEEEEE.
 
Hayati baba wa taifa njoo uwaone CCM huku wanamsumbua mkeo wanamlazimishwa awapigie kampeni , wakati familia yako walishaitelekeza kitambo Leo wameona maji ya shingo ndio wanamlazimishwa Bibi yetu awapigie debe , wape laana hawa mwaka huu wakione Cha mtema kuni , wanataka kuiba na kifimbo chako kiwasaidie .
 
mamam maria.png
 
Imeonekana na kusikika katika vyombo vya habari tena mara nyingi sana m/kiti wa CCM akifanya mzaha mkubwa kwa wanawake ambapo mara nyingi imetafsiriwa kama dhihaka kwa wanawake. Kwa kiingereza wanamwita mtu kama huyo "sexist".

Je, mgombea wa CCM anaweza kuwa sexist? Ni sifa mbaya sana. Hadi Mama Maria Nyerere naye amekuwa mhanga wa jambo hili kwa kulazimishwa kusema asiyopenda, sijui ni mwanamke gani ataponea.

Nafikiri ni aibu sana na ni wakati muafaka kwa Mama na wahanga wengine wa sexism kuombwa msamaha.
 
Hiyo ni vote of no confidence.

Yani huyu mama kaiona historia ya nchi tangu kabla ya uhuru inatokea senuleni kwake ameshindwa hata kusema CCM Oyee, na Magufuli kafanya kazi nzuri?
 
Hahahaa bibi kasema yeye amekuja kama wenzake kujaza uwanja na kuongeza vichwa [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Ngoja tuendelee kuishi kama mashetani tutaelewana kidogo kidogo
 
HUO NI UNAFIKIKAKOJOE ULALE
...mmmmm, Comrade! Yako ni lugha Kali kwa Bibi wa Taifa ambaye pia ni Bibi yako wewe!
Unafiki wake ni Bibi, hebu fafanua!
Tena yeye ndiye katoa somo kabisa LA kuacha unafiki...kwa kueleza wazi kabisa kuwa amefika pale kwa kulazimishwa na ndio maaana hakuwa hata na LA kuongea!
Unafiki wake ni nini sasa hapo, Mkuu?
 
huyu aliyeandika post ndiyo mnafiki kaandika kishabiki sana bibi anabusara zake hawezi kutamka maneno kama ayo acheni ujinga wenu
 
Kuna watu hawana hata utu na heshima kwa wazee, mzee na mama kama huyo ni kumuacha apumzike nyumbani kwake acheze na wajukuu asisumbuliwe na siasa maji taka za nchi hii.
 
Wakuu mama Nyerere alipoamushwa kuja kuzungumza kwenye mkutano wa Ccm, katoa Kari ya Mwaka, kasema kuwa yeye hana LA kuongea Kwa sababu amelazimishwa kuja kwenye mkutano huu.

Kiukweli nimejiuliza inamaaana Ccm imekosa Watu had kumlazimisha mama wa watu kuja? Maaana amesema kuwa ameletwa kuja kuongeza idadi Ya vichwa na amelazimishwa kuja, mlio kwenye TV ni mashahid ni kauli yake mwenyewe
Huyu mama sidhani kama yupo pamoja na CCM...ipo siku atafunguka ukweli
 
Back
Top Bottom