Mama mkwe anamhimiza mke wangu anichune; naomba ushauri

Asante sana kwa ushauri mkuu; nimeupokea. Wanawake ni viumbe wa ajabu sana.
 
Hii ni issue ndogo sana ni kukaa na mkeo kama mwanaume umweleze kuwa unajua kinachoendelea na umkanye umpe muda wa kubadirika labda kama analo tatizo lingine unatuficha.
 
Hii ni issue ndogo sana ni kukaa na mkeo kama mwanaume umweleze kuwa unajua kinachoendelea na umkanye umpe muda wa kubadirika labda kama analo tatizo lingine unatuficha.
Nikae mezani kudiscuss na nyoka? Hii haikubaliki.
 
Kweli kabisa mkuu. Kwa hayo mambo makuu niliyomtendea mke wangu na familia yake sikutarajia kama mama mkwe angenifanyia umafia kama huu.
Tuma aina ya message uliyoona... isije kuwa mama anamshauri mwanae asikae kizembe ahahakikishe anakuhimizia wewe mfanye maendeleo.. wewe ukaona ni shida. Kumbuka kuna maisha ya mbeleleni ya watoto wenu. Edit majina na namba weka hiyo message hapa tuitathmini, usije kuwa unaumia kumbe ni message ya kawaida ya kuhimiza maendeleo.
 
Ile meseji baada ya kugundua nimeisoma aliifuta mkuu
 
Ile meseji baada ya kugundua nimeisoma aliifuta mkuu
Labda nikuulize..statement aliyoandika mama mkwe wako ambayo wewe unasema ni kukuchuna, ilimaanisha kubenefit kutoka kwako (kifedha)au kimsaada? . Na hizo benefit zisihusu familia yako (mkeo, watoto na wewe), au zilikuwa kwa wazazi na familia ya mkeo tu?
Kama ilikuwa hivyo sawa, lakini kama ni kitu ambacho kita benefit familia yako pia, then utakuwa unakosea.
Nakupa mfano, mama anaweza kumwambia mwanae kuwa, wewe kama mama, jaribu kuwa na akiba ya pembeni ambayo itakusaidia siku mumeo akiwa hana hela, na akasisitiza kuwa akiba hii mumeo asiijue. Je utasema hii ni kuchunwa?
Maana ni kweli kuna siku unaweza kuwa huna hela, utasikiaje mkeo akatoa 4m akakuambia .. kiongozi hela hii lipia ada, nilikuwa nime save UTT.. Si unaweza muoa tena?
 
Baba mkwe hajulikani hajatajwa au kakaliwa kichwani kuna familia za kuangalia kabla ya kuoa
 
Piga chini haraka sana huyo atakufilisi kisha akuache nja panda.
 
Hao dawa yao kula wote wawili mtu na mama yake halafu Piga chini wote mtu na mama yake maana hawana akili
 
Brother relax, hiyo ni hulka ya asili kwa wanawake ( kutaka kuhudumiwa na kujiona wana haki hiyo). Ingekua ni meseji za baba mkwe wako hapo ungeshtuka, kumbuka kua mama mkwe naye ni mwanamke pia.

Wanawake hata baada ya kuolewa huamini kua familia yake ni ile aliyolelewa na kukulia nayo, ndio maana watoto wa kike ndio walezi wakuu wa wazazi wao wanapozeeka na sio wanaume.

Watoto wa kike wanabaki kua na familia mbili hata baada ya kuzeeka, ndio maana kitabu cha Mwanzo kuna mstari unasema "kwahiyo mwanaume atamuacha baba na mama yake ili kujenga familia na mkewe kuungana" je unadhani hayo ni makosa ya kisarufi?

Usimuhukumu mkeo, watoto ni wa kwako, na mke ni wa kwako pia wewe ndio mwenye maamuzi ya mwisho, hana kosa lolote, naye pia atakua anamuambia mwanao wa kike kama unae na ataolewa (Inshaallah) maneno hayo hayo, kwasababu ndio asili ya kua mwanamke.

Mke wangu mwenyewe huwa ana ichukulia familia yake kama ndo familia ya kwanza licha ya kua tuna watoto tayari. Pia punguza kushika shika simu ya mkeo, hakuna zuri utakalolipata zaidi ya huzuni.

Rudi home bro, wale ni wanao na yule ni mkeo. Mali yako. Yule ni mama mkwe tu, pambanua.
 
Mzalishe mkeo kila mwaka utakuja kunishukuru au na wewe ndo wale wa watoto wawili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…