Mama mkwe kamtorosha Mke wangu, nifanye nini niko njia panda

Atafute pesa aone kama huyo mama mkwe hajamrudishia binti yake huku akimbembeleza kwa kumwambia Baba msamehe mwenzako mtengeneze maisha
Mkuu pesa ipo sema wana katabia kakutukuzwa wanataka niwatetemekee na imeshindikana
 
Atafute pesa aone kama huyo mama mkwe hajamrudishia binti yake huku akimbembeleza kwa kumwambia Baba msamehe mwenzako mtengeneze maisha
Tena Aki nrudisha, Jamaa awe bize na Mambo yake.
πŸ‘‰Awa ambie ana mengi ya kufanya, so ata waita akiwa freeπŸ˜‚πŸ€’
 
Ndio ninacho kisubiri na nitawashangaa sana kwasababu watamuitaje mtu ambae walimficha mbali na mtoto wake najua lazima wataenda tu kwasababu kwa sasa kinachofanya wawe hivyo ni wana tabia ya kujikweza sana na mm naikataa mazima
Tunza meseji zote za miamala na ukorofi wake.

Ipo siku zitakusaidia
 
Ulifanya Ujinga mkubwa sana kwenda kwenye hiyo familia baada ya mkeo kutoroka yani Hukutakiwa hata kufikiria kumtafuta...!! Usirudie kosa piga kimya endelea na mambo yako na Mkeo akirudi peke yake Usimpokeee kamwe mwambie sikutambui kama mke wangu rudi ulipotoka.
 
Problem
Solved Jipongeze
 
Nakili kwamba nilikosea sana lakini ndio kujifunza mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…