MzalendoHalisi
JF-Expert Member
- Jun 24, 2007
- 4,679
- 1,612
Field Marshall,
nakuheshimu, lakini usije ukawa unatumiwa ndugu yangu. hii ishu ya Mama Mongella inaonekana ni vita vya mwewe.
Ni mambo yaleyale ya Sumaye ana mashamba kumbe kila kiongozi mkubwa ana mashamba tena zaidi ya huyo Sumaye.
Mimi naamini hii habari/kashfa ina mkono wa Watanzania. Ni nani aliyepeleka taarifa kwamba Mama Mongela amepokea malipo toka Bunge la Tanzania? Ni nani aliyepeleka taarifa kwamba Mama Mongella kaajiri mkwe wake?
Ninavyoelewa mimi Mama Mongella siyo mtendaji wa kila siku wa
Bunge la AU.
Sidhani kama taratibu za kazi zinamzuia mkwe wa Mama Mongela kuajiriwa na Bunge la AU. Kitu ambacho ni makosa ni Mama Mongela kuajiri ndugu yake ktk Ofisi ya Spika wa AU.
Hata kama kachomewe, issue je ni kweli kala haya mapesa pasipo uhalali? Of course wanasiasa wote wana maadui, unachotakiwa ni kutokuwapa maadui zako nafasi. yeye kwa kuiba mahela hayo yote halafu maadui zake wakajua alitoa nafasi mwenyewe. Anakula gharama ya wanasiasa kutaka kutajirikia kwenye siasa tena uzeeni, wajinga kabisa hawa. Kuna umuhimu wa kuwahimiza vijana kufanya kazi za kitaalamu kabla ya kujiingiza mwili mzima kwenye siasa. Vinginevyo tutaendelea kuwa na mianasiasa mijizi tu Afrika!
Kitila,
Umeongea jambo muhimu sana hapa, hii ya kuwa na wanasiasa ambao hawajui kazi zingine zozote zaidi ya siasa.
Chapa kazi yako serikalini au private companies na kisha ndio jiunge na siasa.
Bila kujua ugumu na mikiki mikiki ya maisha huko makazini, ni ngumu sana kuwa na mafanikio makubwa kwenye siasa.
Pia siasa hapawezi kuwa mahali pa kutajirikia, utaishiwa kuwa fisadi tu.
Ukiangalia jinsi ofisi fulani zinavoajiri watu, kama benki kuu na hizi balozi.You begin to wonder kama Tanzania kuna "Equal Opportunity" maana kila sehemu Mkapa this, Malecela that,Sokoine this,Makamba that, Mwinyi this sio kwamba hatutaki hawa watu wafanye kazi lakini kuna level ya concentration fulani inaboa unapokuta kwenye ofisi moja huyu Mongella huyu Malecela unajiuliza hivi hapa last name ni qualification au vipi?
Mi nawasifu sana watoto wa viongozi wanaopiga mitikasi yao au waliokuwa katika sekta binafsi (bila ya kutafutiwa kazi na wazee wao)
Mkuu Pundit,
Heshima mbele, now what is your take kuhusu watoto wa viongozi kwamba wasifanye kazi za kuajiriwa serikalini? au kwenye mashirika kwa sababu ya majina ya baba zao? Mkuu time zimebadilika, zile enzi watoto wa viongozi wanakuwa walevi tu wavuta bangi sio leo tena mkuu, ninaweza kukuelewa kama kuna mtoto wa kiongozi ambaye ameajiriwa mahali kwa vitisho vya baba, lakini hiyo sio tabia za foreign mkuu, na ingekuwa believe me foreign asingeajiriwa mtoto wa masikini wangekuwa wote ni watoto wa wakubwa tu, unless tuna ushahidi wa mtoto fulani wa kigogo kulazimisha kuajiriwa mahali tunakuwa tunatafuta sababu tu ya our natinal misery at the wrong place,
Sio watoto wote wa viongozi wanaoweza kutafuta kazi zao wenyewe, kama vile ambavyo sio watoto wote wa masikini wanaoweza kujiajiri wenyewe, it works both ways, lakini haina maana mtoto wa kiongozi mwenye qualifications asiombe kazi serikalini au popote pale, kwa sababu itaonekana kuwa ni baba yake I mean ni hoja finyu sana. Zamani tunajua walikuwa wakipeana bila qualificatons, lakini sio sasa mchezo uliiisha siku nyingi, waacheni watoto wa viongozi wafanye kazi zao za kutafuta maisha, maana sasa tutakuwa tunalia wivu tu!
Kitila Mkumbo said:Kuna umuhimu wa kuwahimiza vijana kufanya kazi za kitaalamu kabla ya kujiingiza mwili mzima kwenye siasa. Vinginevyo tutaendelea kuwa na mianasiasa mijizi tu Afrika!
Kitila Mkumbo said:Hata kama kachomewe, issue je ni kweli kala haya mapesa pasipo uhalali? Of course wanasiasa wote wana maadui, unachotakiwa ni kutokuwapa maadui zako nafasi. yeye kwa kuiba mahela hayo yote halafu maadui zake wakajua alitoa nafasi mwenyewe. Anakula gharama ya wanasiasa kutaka kutajirikia kwenye siasa tena uzeeni, wajinga kabisa hawa. Kuna umuhimu wa kuwahimiza vijana kufanya kazi za kitaalamu kabla ya kujiingiza mwili mzima kwenye siasa. Vinginevyo tutaendelea kuwa na mianasiasa mijizi tu Afrika!
Waheshimiwa mnaosema Dk Shein ni Dull.. hebu waulizeni wanaotoa Daily Briefings Pale ikulu.
Ni bora wakutane na Muungwana JK mwenyewe kuliko Shein maana Dk Shein ni msomaji mahiri na hingia in details kwenye kila report inayopitia kwake bila unafiki wala woga.. unlike Muungwana!
So.. kwa ndugu mnaosema kwamba Nchi haiwezi ku-afford kuwa na mtu "Dull" kama Shein siwaelewi!
Labda kinachomponza ni ukimya na kutokuwa kimbelembele!
The Guy is Clean, Intelligent & Patriot!
I believe siku ikitokea mtu wa dizaini ya Dk Shein kuwa President ndo siku Nchi yetu na CCM vitabadilika!
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake Mpeni!
He is one of the bests in our current administration!
Wenzako wamezoea wanasiasa wenye midomo tena wale wenye uwezo wa kuhutubia kwenye majukwaa. Kwa TZ ili uonekane unaweza siasa lazima ukahutubia mkutano pale Manzese, Jangwani, etc kama hujafanya hivi wewe sio mwanasiasa, ni dull ndio maana hao akina Shein wanaonekana hamnazo lakini akina Makamba ndo wanazo. Mimi nakwambia ile nchi tuna kazi, kila mtu anahitaji kubadilika kuanzia Rais, sisi wenyewe hapa JF, wanafunzi, hadi kule kwetu kijijini. Safari ni ndefu lakini lazima twende madamu Mungu aliamua kutuweka katika ile ardhi, sio bure ana makusudi lazima tuyatimize.
ES
samahani, zile picha zilikuwa under the belt na haziendani na majibu yako ya kiistarabu uliyoyatoa japo yamekaa katika kuitetea Foreign ambako kumejaa tuhuma za Udini na ukabila na unduguzesheni
In that case nina edit ile post yangu ya mwisho
niwie radhi mzee yote ilitokana na kutokuwa na la kukujibu wakati ule lakini hiyo haindoi ukweli umekuwa ukiwatetea sana jamaa zako waliopo Foreign kwa amna mbali mbali na saa zingine huwa unaomba threads zihamishwe pale tuhuma zinapokuwa nzito zaidi na mfano ni ule wa Caro wa Ubalozi wetu London na mumewe kuuza bwimbwi na ulipoambiwa ulikuja juu. Kuhusu wakina Mahiga ndio usiseme
Mzee sie wengine tunao hao jamaa huko huko CCM lakini hatuishi kuwatoa nishai kila kukicha maana nchi yetu wote na hatuwezi kujidai tunaitakia mema nchi huku tunakuwa na double standards jamaa zetu wakituhumiwa kwa ubadhirifu
Nakuheshimu sana lakini saa zingine huo moyo wako wa kuwatetea hawa watu huwa inaboa haswa!
Lakini tuendelee na mjadala
Nimesikia kwa watu kuwa hii ni sifa na utamaduni wa wapemba, UAMINIFU, ndio maana wanafanikiwa kwenye biashara. Hebu watafutieni tuhuma za ufisadi kina Dr Salim Ahmed Salim na Marehemu Dr Omar Ali Juma kama mtapata hata moja.