Mama Mongella - Aghushi na Kutafuna Mamillioni Ya Pesa!

Mama Mongella - Aghushi na Kutafuna Mamillioni Ya Pesa!

Halafu ni tamaa tu dola sijui tu laki na nusu! Tamaa ya fisi na mazoea!

Achukuliwe hatua za kisheria kama akishindwa kulipa deni AU! Pia ajiuzulu! Ashikiwe tu bango- hakuna cha Utanzania- ukiwa Mla Rushwa- sheria ichukue mkondo wake!

Tumechoka na aibu Tz kila siku!
 
Field Marshall,

nakuheshimu, lakini usije ukawa unatumiwa ndugu yangu. hii ishu ya Mama Mongella inaonekana ni vita vya mwewe.

Ni mambo yaleyale ya Sumaye ana mashamba kumbe kila kiongozi mkubwa ana mashamba tena zaidi ya huyo Sumaye.

Mimi naamini hii habari/kashfa ina mkono wa Watanzania. Ni nani aliyepeleka taarifa kwamba Mama Mongela amepokea malipo toka Bunge la Tanzania? Ni nani aliyepeleka taarifa kwamba Mama Mongella kaajiri mkwe wake?

Ninavyoelewa mimi Mama Mongella siyo mtendaji wa kila siku wa
Bunge la AU.

Sidhani kama taratibu za kazi zinamzuia mkwe wa Mama Mongela kuajiriwa na Bunge la AU. Kitu ambacho ni makosa ni Mama Mongela kuajiri ndugu yake ktk Ofisi ya Spika wa AU.

Hata kama kachomewe, issue je ni kweli kala haya mapesa pasipo uhalali? Of course wanasiasa wote wana maadui, unachotakiwa ni kutokuwapa maadui zako nafasi. yeye kwa kuiba mahela hayo yote halafu maadui zake wakajua alitoa nafasi mwenyewe. Anakula gharama ya wanasiasa kutaka kutajirikia kwenye siasa tena uzeeni, wajinga kabisa hawa. Kuna umuhimu wa kuwahimiza vijana kufanya kazi za kitaalamu kabla ya kujiingiza mwili mzima kwenye siasa. Vinginevyo tutaendelea kuwa na mianasiasa mijizi tu Afrika!
 
TZ-Pride,Ogah,Field Marshall,

I have all reasons to believe that Dr.Shein is clean. He doesnt have a big role in the daily running of the government.

Usafi wake hauna maana kwasababu hawezi kushinda nomination ya CCM bila kusaidiwa na watu wachafu. ukiona CCM wanampigia debe mtu kama Shein ujue wanataka kumtumia tu huko mbele ya safari.

Mkandara,

kama Mama Mongella analipwa au anatakiwa kulipwa na Bunge la Tanzania basi inaonyesha huko AU anaenda kuongoza vikao tu.

kwa maana nyingine huyu siyo Mtendaji wa kila siku wa Bunge la AU. kwa msingi huo basi kuna uwezekano taratibu hazijakiukwa ktk kumuajiri mkwe wake huko AU.
 
Hata kama kachomewe, issue je ni kweli kala haya mapesa pasipo uhalali? Of course wanasiasa wote wana maadui, unachotakiwa ni kutokuwapa maadui zako nafasi. yeye kwa kuiba mahela hayo yote halafu maadui zake wakajua alitoa nafasi mwenyewe. Anakula gharama ya wanasiasa kutaka kutajirikia kwenye siasa tena uzeeni, wajinga kabisa hawa. Kuna umuhimu wa kuwahimiza vijana kufanya kazi za kitaalamu kabla ya kujiingiza mwili mzima kwenye siasa. Vinginevyo tutaendelea kuwa na mianasiasa mijizi tu Afrika!

Kitila,

Umeongea jambo muhimu sana hapa, hii ya kuwa na wanasiasa ambao hawajui kazi zingine zozote zaidi ya siasa.

Chapa kazi yako serikalini au private companies na kisha ndio jiunge na siasa.

Bila kujua ugumu na mikiki mikiki ya maisha huko makazini, ni ngumu sana kuwa na mafanikio makubwa kwenye siasa.

Pia siasa hapawezi kuwa mahali pa kutajirikia, utaishiwa kuwa fisadi tu.
 
Hii ni problem. Ukiangalia CV za viongozi wetu wa juu zimejaa ukada, ooh, niliwahi kuwa katibu wa chama kule na kule-hii ni feki, ndio maana wakiingia serikalini hawana vision zaidi ya mikakati ya kuiba kura. Halafu hawa hawawezi kukubali kushindwa uchaguzi kwa sababu wanajua wakitoka kwenye siasa hawana kitu kingine cha kufanya, watataabika wao na familia zao.

Wanasiasa wa namna hii pia hawawezi kukwepa ufisadi maana hawana ngao ingine. Mtu alianza na uchipukizi, then UVCCM, then serikali, what else can he do on earth apart from politics?
 
Ukiangalia jinsi ofisi fulani zinavoajiri watu, kama benki kuu na hizi balozi.You begin to wonder kama Tanzania kuna "Equal Opportunity" maana kila sehemu Mkapa this, Malecela that,Sokoine this,Makamba that, Mwinyi this sio kwamba hatutaki hawa watu wafanye kazi lakini kuna level ya concentration fulani inaboa unapokuta kwenye ofisi moja huyu Mongella huyu Malecela unajiuliza hivi hapa last name ni qualification au vipi?

Mi nawasifu sana watoto wa viongozi wanaopiga mitikasi yao au waliokuwa katika sekta binafsi (bila ya kutafutiwa kazi na wazee wao)

Mkuu Pundit,

Heshima mbele, now what is your take kuhusu watoto wa viongozi kwamba wasifanye kazi za kuajiriwa serikalini? au kwenye mashirika kwa sababu ya majina ya baba zao? Mkuu time zimebadilika, zile enzi watoto wa viongozi wanakuwa walevi tu wavuta bangi sio leo tena mkuu, ninaweza kukuelewa kama kuna mtoto wa kiongozi ambaye ameajiriwa mahali kwa vitisho vya baba, lakini hiyo sio tabia za foreign mkuu, na ingekuwa believe me foreign asingeajiriwa mtoto wa masikini wangekuwa wote ni watoto wa wakubwa tu, unless tuna ushahidi wa mtoto fulani wa kigogo kulazimisha kuajiriwa mahali tunakuwa tunatafuta sababu tu ya our natinal misery at the wrong place,

Sio watoto wote wa viongozi wanaoweza kutafuta kazi zao wenyewe, kama vile ambavyo sio watoto wote wa masikini wanaoweza kujiajiri wenyewe, it works both ways, lakini haina maana mtoto wa kiongozi mwenye qualifications asiombe kazi serikalini au popote pale, kwa sababu itaonekana kuwa ni baba yake I mean ni hoja finyu sana. Zamani tunajua walikuwa wakipeana bila qualificatons, lakini sio sasa mchezo uliiisha siku nyingi, waacheni watoto wa viongozi wafanye kazi zao za kutafuta maisha, maana sasa tutakuwa tunalia wivu tu!

Umekazana kutetea hiyo "foreign' yako lakini upo uchafu kibao katika kupata ajira za hapo. Vimemo mtindo mmoja pale. Kuna interview fulani miaka miwili iliopita, panel ya kuinterview ilishikwa na butwaa kuona majina kadhaa kwenye orodha..ambayo hayakuwepo kwa waliokuwa shortlisted..waliambiwa hayo yatoka kwa "mzee". Watu wale waliitwa kwenye interview bila kuomba..ku apply..mmh na wote(3) walipata kazi that time.

Mmoja ndugu yangu wa karibu..alikuwa bado anamalizia kozi lakini kazi kapata..kwa kimemo! Tetea lingine lakini si utaratibu wa uapatikanaji wa ajira kwenye taasisi za uma. Wengine victims wa hali hiyo..usitutoneshe vidonda ndugu yangu.
 
Kitila Mkumbo said:
Kuna umuhimu wa kuwahimiza vijana kufanya kazi za kitaalamu kabla ya kujiingiza mwili mzima kwenye siasa. Vinginevyo tutaendelea kuwa na mianasiasa mijizi tu Afrika!

..Nazir Karamagi,Iddi Simba, na Daniel Yona, without the scandals, wana-fit description of the kind of politician you want for Tanzania.

..Nini kimewatokea hawa mpaka wakafanya madudu tusiyoyatarajia?

..arghh!! mara nyingine ikifikiria nchi yetu unaweza kuwa mwendawazimu.

Kitila Mkumbo said:
Hata kama kachomewe, issue je ni kweli kala haya mapesa pasipo uhalali? Of course wanasiasa wote wana maadui, unachotakiwa ni kutokuwapa maadui zako nafasi. yeye kwa kuiba mahela hayo yote halafu maadui zake wakajua alitoa nafasi mwenyewe. Anakula gharama ya wanasiasa kutaka kutajirikia kwenye siasa tena uzeeni, wajinga kabisa hawa. Kuna umuhimu wa kuwahimiza vijana kufanya kazi za kitaalamu kabla ya kujiingiza mwili mzima kwenye siasa. Vinginevyo tutaendelea kuwa na mianasiasa mijizi tu Afrika!

..NDIYO, kachomewa. mimi nawaunga mkono wote mliamua kumlipukia huyu Mama. Lakini msisahau kuwasaka na hao waliomchomea. Mara nyingi huwa ni wabaya/wachafu zaidi.

..hivi unakumbuka aliyemchomea Sumaye kwa ile safari ya USA. Yeye amesafiri mara ngapi kwenda kuangalia mpira, au kucheza dansi, na kujitambulisha?
 
mimi huwa nashangaa watu wanaotetea uozo,tukubali tanzania yetu imeoza,kwa nini hawa viongozi wa muda mrefu wasingekuwa na makampuni ya maana ya kutoa ha ajira ya watu mia moja tu,kwanza wanauzoefu na wametembea nchi mbalimbali na kupata ufahamu wa kutosha na hivyo kuwa rahisi kwa wao kuwa na hizo biashara na kuajiri ngudu na watoto wao, lakini mpaka leo tunapigana vikumbo tu serikalini na kwenye mashirika ya umma, hii aridhi baada ya kuwauzia wazungu na waarabu tungejiuzia sisi wenyewe.

Bora waziri mkuu aliyeamua kuanzisha kioski cha simu na kufua nguo.
 
Umekazana kutetea hiyo "foreign' yako lakini upo uchafu kibao katika kupata ajira za hapo. Vimemo mtindo mmoja pale. Kuna interview fulani miaka miwili iliopita, panel ya kuinterview ilishikwa na butwaa kuona majina kadhaa kwenye orodha..ambayo hayakuwepo kwa waliokuwa shortlisted..waliambiwa hayo yatoka kwa "mzee".

Mkuu unayoyasema yanapaswa kuwa yametokea Mama Migiro, akiwa waziri, siku moja ninilikuwepo mkubwa mmoja akimuomba Mama Migiro, amuingize mtoto wake huko, jawabu alilolitoa Mama migiro kwa kigogo yule ilikuwa ni kwamba no way tena no chance, kwanza alimuambia kuwa serikali ime-freeze uajiri pale, kwa hiyo mkuu maneno yako si kweli, na kwamba hata serikali ikiruhusu kuna pannel maalum inayoajiri sio yeye waziri,

Miaka miwili iliyopita, serikali ilikuwa ime-freeze uajiri pale mkuu, ni tabia yangu kutetea ukweli bila ya kujali what, nilisema Mama Migiro, ndiye the only kiongozi safi alipochaguliwa na Muungwana, ilikuwa ni pamoja na kumsikia akimkatalia yule kigogo kumuajiri mtoto wake,

Mkuu Joka,

Mimi situmiwi na mtu yoyote, Mama Mongella, ni mshikaji wangu wa karibu sana kwa hiyo kungekuwa na chembe yoyote ya kutumiwa au kuchochewa na maaadui zake, basi ningekuwa wa kwanza kuzikumbati a hizo excuse ili nimtete, baada ya kupata hii ishu nimeongea na viongozi wengi na wamenihakikishia kuwa hii habari ni kweli, na the fact kwamba hata ilisemwa mbele ya rais wetu na hakuwa na la kusema, can you imagine wewe rais wa nchi mtu wako anashambuliwa mbele yako na huna la kujitetea?

Aibu sana mkuu, tena sana hapa hakuna utetezi, yeye mama ni kujiuzulu tu ili yasitoke mengine ya aibu zaidi maana najua kuwa wanayo na yapo. Mama ameharibu jina lake bila sababu ya msingi, ninajua njia zote chafu zilizotumika na Mandela, kumsaidia huyu mama kupata hii kazi ambayo ilikuwa clear kuwa ni ya Spika wa bunge la SA then, lakini zikafanywa mbinu ikiwa ni pamoja na rushwa mpaka huyu mama akapewa, sasa leo tunaongelea haya? ni aibu kubwa sana kwa taifa letu, pia ukizingatia kuwa huko UN nako kuna sooo la Mama Tibaijuka na undugunization,

Aibuuuu!
 
Waheshimiwa mnaosema Dk Shein ni Dull.. hebu waulizeni wanaotoa Daily Briefings Pale ikulu.
Ni bora wakutane na Muungwana JK mwenyewe kuliko Shein maana Dk Shein ni msomaji mahiri na hingia in details kwenye kila report inayopitia kwake bila unafiki wala woga.. unlike Muungwana!

So kwa ndugu mnaosema kwamba Nchi haiwezi ku-afford kuwa na mtu "Dull" kama Shein siwaelewi! Labda kinachomponza ni ukimya na kutokuwa kimbelembele! The Guy is Clean, Intelligent & Patriot!

I believe siku ikitokea mtu wa dizaini ya Dk Shein kuwa President ndo siku Nchi yetu na CCM vitabadilika!
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake Mpeni. He is one of the bests in our current administration!
 
Wajameni,
Kama mnakumbuka mama Mongela akiwa balozi wetu India wakati ule serikali ilikuwa likizo, kuna paspoti nyingi saana zilipotea na ziliuzwa kimagendo kwa wasomali na wanaigeria.
Hili linafahamika saana kwa wengi.
 
ES

samahani, zile picha zilikuwa under the belt na haziendani na majibu yako ya kiistarabu uliyoyatoa japo yamekaa katika kuitetea Foreign ambako kumejaa tuhuma za Udini na ukabila na unduguzesheni

In that case nina edit ile post yangu ya mwisho

niwie radhi mzee yote ilitokana na kutokuwa na la kukujibu wakati ule lakini hiyo haindoi ukweli umekuwa ukiwatetea sana jamaa zako waliopo Foreign kwa amna mbali mbali na saa zingine huwa unaomba threads zihamishwe pale tuhuma zinapokuwa nzito zaidi na mfano ni ule wa Caro wa Ubalozi wetu London na mumewe kuuza bwimbwi na ulipoambiwa ulikuja juu. Kuhusu wakina Mahiga ndio usiseme

Mzee sie wengine tunao hao jamaa huko huko CCM lakini hatuishi kuwatoa nishai kila kukicha maana nchi yetu wote na hatuwezi kujidai tunaitakia mema nchi huku tunakuwa na double standards jamaa zetu wakituhumiwa kwa ubadhirifu

Nakuheshimu sana lakini saa zingine huo moyo wako wa kuwatetea hawa watu huwa inaboa haswa!

Lakini tuendelee na mjadala
 
Waheshimiwa mnaosema Dk Shein ni Dull.. hebu waulizeni wanaotoa Daily Briefings Pale ikulu.
Ni bora wakutane na Muungwana JK mwenyewe kuliko Shein maana Dk Shein ni msomaji mahiri na hingia in details kwenye kila report inayopitia kwake bila unafiki wala woga.. unlike Muungwana!
So.. kwa ndugu mnaosema kwamba Nchi haiwezi ku-afford kuwa na mtu "Dull" kama Shein siwaelewi!
Labda kinachomponza ni ukimya na kutokuwa kimbelembele!
The Guy is Clean, Intelligent & Patriot!

I believe siku ikitokea mtu wa dizaini ya Dk Shein kuwa President ndo siku Nchi yetu na CCM vitabadilika!
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake Mpeni!
He is one of the bests in our current administration!

Wenzako wamezoea wanasiasa wenye midomo tena wale wenye uwezo wa kuhutubia kwenye majukwaa. Kwa TZ ili uonekane unaweza siasa lazima ukahutubia mkutano pale Manzese, Jangwani, etc kama hujafanya hivi wewe sio mwanasiasa, ni dull ndio maana hao akina Shein wanaonekana hamnazo lakini akina Makamba ndo wanazo. Mimi nakwambia ile nchi tuna kazi, kila mtu anahitaji kubadilika kuanzia Rais, sisi wenyewe hapa JF, wanafunzi, hadi kule kwetu kijijini.

Safari ni ndefu lakini lazima twende madamu Mungu aliamua kutuweka katika ile ardhi, sio bure ana makusudi lazima tuyatimize.
 
Askofu Mkuu Desmond Tutu, mwaka jana aliangua kilio na kuiuliza jamii ya Afrika Kusini "tumefikaje hapa? Hapa tunapopoteza moral bearing?" Nadhani hata sisi waTanzania itabidi tujiulize swali hilo. Sisi ambao tulikuwa tunaitana ndugu! Leo kila kukicha ni habari kama hizi! hii habari ni mbaya kutoka kokote utakakoiangalia. Kama kweli Mheshimiwa kafanya haya(unjustified sense of entitlement) au kama kuna watu wanampakazia (fitna n.k)! Tumefikaje hapa tulipo
 
Wenzako wamezoea wanasiasa wenye midomo tena wale wenye uwezo wa kuhutubia kwenye majukwaa. Kwa TZ ili uonekane unaweza siasa lazima ukahutubia mkutano pale Manzese, Jangwani, etc kama hujafanya hivi wewe sio mwanasiasa, ni dull ndio maana hao akina Shein wanaonekana hamnazo lakini akina Makamba ndo wanazo. Mimi nakwambia ile nchi tuna kazi, kila mtu anahitaji kubadilika kuanzia Rais, sisi wenyewe hapa JF, wanafunzi, hadi kule kwetu kijijini. Safari ni ndefu lakini lazima twende madamu Mungu aliamua kutuweka katika ile ardhi, sio bure ana makusudi lazima tuyatimize.
c863bf5b-1.jpg

with threads like this kweli tunahitaji kubadilika.
http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=8308
 
ES

samahani, zile picha zilikuwa under the belt na haziendani na majibu yako ya kiistarabu uliyoyatoa japo yamekaa katika kuitetea Foreign ambako kumejaa tuhuma za Udini na ukabila na unduguzesheni

In that case nina edit ile post yangu ya mwisho

niwie radhi mzee yote ilitokana na kutokuwa na la kukujibu wakati ule lakini hiyo haindoi ukweli umekuwa ukiwatetea sana jamaa zako waliopo Foreign kwa amna mbali mbali na saa zingine huwa unaomba threads zihamishwe pale tuhuma zinapokuwa nzito zaidi na mfano ni ule wa Caro wa Ubalozi wetu London na mumewe kuuza bwimbwi na ulipoambiwa ulikuja juu. Kuhusu wakina Mahiga ndio usiseme

Mzee sie wengine tunao hao jamaa huko huko CCM lakini hatuishi kuwatoa nishai kila kukicha maana nchi yetu wote na hatuwezi kujidai tunaitakia mema nchi huku tunakuwa na double standards jamaa zetu wakituhumiwa kwa ubadhirifu

Nakuheshimu sana lakini saa zingine huo moyo wako wa kuwatetea hawa watu huwa inaboa haswa!

Lakini tuendelee na mjadala

BRAZAMENI thanks for some epic Roman parallel stuff, Brutus style.

Brutus: If there be any in this assembly, any dear friend of Caesar's, to him I say that Brutus' love to Caesar was no less than his. If then that friend demand why Brutus rose against Caesar, this is my answer: not that I loved Caesar less, but that I loved Rome more. Had you rather Caesar were living and die all slaves than that Caesar were dead, to live all free men?
 
seriously huwa tunaambiwa ohh viongozi wetu inabidi wabadilike etc etc...sisi je?

Tunataka kubadilika?

au tunataka kurecycle hawa watawala?
 
Hivi mmeshasahau kuwa viongozi wetu ni reflection ya sisi wenyewe...? kama mnakubaliana na hilo basi ni lazima sisi tubadilike kwanza kabla ya kuwapata viongozi tunaowataka....
 
Nimesikia kwa watu kuwa hii ni sifa na utamaduni wa wapemba, UAMINIFU, ndio maana wanafanikiwa kwenye biashara. Hebu watafutieni tuhuma za ufisadi kina Dr Salim Ahmed Salim na Marehemu Dr Omar Ali Juma kama mtapata hata moja.

Umeniwahi mawazo yangu.

By the way huyu VC ndio kiongozi peke wa CCm alotulia anajua nini anafanya.mtizame the guy alivyokaaa kimya anawatazama tu wnavyopapatika na kugombea hiyo KEKI,mie naamini ipo siku CCM watajua faida ya Dr Shein
 
Kwa nini Vibaka Manzese huadhibiwa kwa mass action na watu kama mama Mongela wanaachwa tu- eti warudishe? Wizi sii wizi tu??
 
Back
Top Bottom