Mama mwenye hali ngumu anakaa na binti mdogo mjamzito ambaye sio ndugu yake

Nasemaga kila siku humu, wazaramo pamoja na mapungufu yao ila, Kama kuna kitu wamefanikiwa ni kutokuwa na stress, huwa wanaridhika na vitu vidogo sana kwenye maisha
Wabarikiwe sana....hawa ndiyo wa kuoa na kuolewa nao.
Hakuna mbaba mzaramo humu ndani?🤦
 
Ukifanya jambo kwa nia njema, Mungu anakuwekea ulinzi automatically..
 
Shetani hilo.
 
Yes, mkuu. Watu wengi wa Pwani wakiwemo wazaramo na Wandengereko, licha ya watu kuwasema kuwa wanatabia za uswahili kupenda taarabu na singeli, ni watu wenye mioyo mema mnoo..
Sasa kupenda taarabu na singling ni kosa?? Si ndo asili yao?? Nyue wasukuma na wakurya mbons mnapenda ngoma zenu? Uswahili huku ndo asili yake!
 
Mwinyi sio mpemba ila maalim ni mpemba na kweli ni muungwana sana
Maalim alikuwa mpinzani safi sana. Muungwana, hatoi matusi jukwaani.

Ninamuomba Mwenye Mungu aendelee kumpa pumziko jema yule Mzee wetu..
 
Wengi ni wale wale tu na hali zao
Yes. Upo sahihi mkuu. Wengi ni wa kipato cha chini, lakini Mwenyezi Mungu amewapa mioyo iliyojaa upendo.

Kuna mama wa kizaramo alikuwa ni mama Lishe zamani wakati nipo mdogo. Alikuwa akimaliza kuuza chakula, ilikuwa lazima anibakishie wali na maharage. Si unajua tena sisi watoto wa uswazi tunavyopenda ubwabwa??

Mungu aendelee kumpa pumziko jema mama yule huko mbinguni..
 
Ningeomba utushirikishe na sisi tumsaidie japo kwa michango kidogo kwa kadri tutakavyo jaaliwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…